Kubadilisha ADA hadi Shilingi za Kenya kwa kutumia Yellow Card

Mara nyingi, watu katika nchi zenye uchumi duni zaidi duniani wanapata faida nyingi zaidi kutokana na zana za kifedha zilizogatuliwa za blockchain. Hata hivyo, changamoto moja kwa watumiaji hawa wapya kwenye blockchain ni kuelewa ubadilishanaji wa crypto, kwa sababu njia zinazopatikana hutofautiana kulingana na nchi.

Kenya, katikati mwa Afrika, ni sehemu mojawapo ambayo ni nzuri kwa zana za kifedha za Web3. Hata hivyo, uchunguzi wa hivi majuzi kuhusu jinsi ya kubadilisha $ADA hadi Shilingi ya Kenya uliibua ushauri ufuatao:

"Tafuta mtu mtandaoni ambaye anataka kununua $ADA yako, na ukutane naye mahali pa umma, kama kona ya barabara."

Chaguo hili sio endelevu!

Katika maabara ya Lido Nation iitwayo Ngong Road Blockchain Lab huko Nairobi, Kenya, mwandishi wa blockchain na mfasiri Sallyanne Atieno alichukua mambo mikononi mwake. Alitafiti zana zipi zinazopatikana nchini Kenya, na akaandika mwongozo huu wa Jinsi ya Kubadilisha $ADA hadi sarafu ya nchi, Shilingi za Kenya (Ksh).

Ili kubadilisha ADA yako kuwa shillingi za Kenya, unahitaji kuwa na vitu hivi 3:

  • Pochi la Cardano
  • Akaunti ya Yellow Card
  • Nambari inayotumika ya Mpesa

Hatua za kubadilisha ADA kwa shilingi za Kenya

Tutachukulia kuwa tayari una pochi la Cardano, na nambari inayotumika ya Mpesa. (Ikiwa unahitaji pochi la Cardano, angalia maagizo hapa)

Kitu cha mwisho unachohitaji ni akaunti ya Yellow Card. Hapa kuna hatua za kuunda akaunti:

  1. Nenda kwa Yellowcard.io
  2. Bofya kwenye “jisajili” ili kuunda akaunti

Yellow_card

  1. Jaza maelezo yanayohitajika. Kumbuka kutumia majina yaliyopo kwenye kitambulisho (Kitambulisho cha Taifa) na kuongeza namba ya simu ambayo imesajiliwa kwa huduma za Mpesa.

Details

  1. Thibitisha nambari yako ya simu na anwani yako ya barua pepe baada ya kujaza maelezo yanayohitajika

Verify_Step_1 Verify_Step_2

  1. Ukifika mahali unapoombwa kuunda PIN, hakikisha umeunda ambayo unaweza kukumbuka kwa urahisi. PIN hii itatumika kuidhinisha kuingia kwenye akaunti yako na kufanya shughuli kutoka kwa akaunti yako ya Yellow Card

PIN

Mara tu unapojiandikisha, hivi ndivyo kiolesura chako kitakavyoonekana

Signed_Up

  1. Kwenye kona ya juu kulia, kuna pau za urambazaji. Kwanza, utahitaji kutuma ADA kutoka kwa pochi yako ya Cardano hadi kwenye akaunti yako ya Yellow Card. Utafanya hivyo kwa kubofya “crypto” kisha usogeze chini na uchague chaguo la Cardano (ADA).

Send_Ada

  1. Ibofye na kisha uchague kupokea

Receive_ADA

Kutakuwa na ibukizi ya anwani ya kupokea. Inakili. Kisha nenda kwenye pochi lako la Cardano na ubofye “Tuma”. Bandika anwani katika sehemu ya “Pokea anwani”, na ukamilishe hatua nyingine za shughuli ili kutuma kiasi cha ADA unachotaka kuhamishia kwenye Yellow Card. Ipe dakika chache shughuli ikamilike na ADA itaakisi katika akaunti yako.

Kinachofuata ni kuuza ADA kwa Shilingi za Kenya.

  1. Bofya kwenye pochi kwenye upau wa urambazaji na upande wa kushoto, bofya kwenye mkoba wa Cardano ADA

ADA_Wallet

  1. Bofya kwenye kitufe cha kununua / kuuza na uchague “uza”. Andika kiasi cha ADA unachotaka kuuza kisha ubofye kwenye kagua na uthibitishe.

Review Confirm

Weka PIN yako ili kuidhinisha shughuli

Authorize

Kisha ADA yako itauzwa na Shilingi za Kenya zinazolingana zitaonekana katika pochi yako ya Shilingi ya Kenya. Pochi hili la Shilingi za Kenya inaundwa kwa ajili yako pindi mauzo yako ya ADA yatakapochakatwa. Pakia upya ukurasa ili uweze kuiona. Itakuwa upande wa kushoto wa skrini yako, juu ya pochi ya Cardano ADA.

Kenyan_Shillings_Wallet_1 Kenyan_Shillings_Wallet_2

  1. Nenda kwenye pochi yako ya Shilingi ya Kenya na uibofye na utaona vitufe vya kuweka na kutoa. Bonyeza kitufe cha kuondoa. Kisha utaombwa uthibitishe maelezo yako kwanza kabla ya kuendelea na uondoaji. Jaza maelezo yote ambayo yatajumuisha picha ya Kitambulisho chako cha Taifa na selfie yako miongoni mwa mambo mengine. Ukimaliza, utapokea barua pepe ya uthibitishaji inayokiri uthibitishaji huo.

Confirmation_1 Confirmation_2 Confirmation_3

Hapa kuna barua pepe ya uthibitishaji

Verification

  1. Baada ya kupokea barua pepe ya uthibitishaji, rudi kwenye akaunti yako, bofya pochi, bofya pochi ya Shilingi ya Kenya kisha ubofye toa. Ikiwa unatumia simu ya rununu, utakuwa na chaguzi mbili za kutoa, moja ni kutumia pesa za rununu na nyingine ni kwa kutumia akaunti ya benki. Ikiwa uko kwenye kompyuta, kutakuwa na chaguo la akaunti ya benki pekee. Ikiwa huna akaunti ya benki, ningekushauri kwamba upakue programu ya Yellow Card kwenye simu yako na uingie ili uweze kutoa pesa kupitia simu ya mkononi.

Njia ya uondoaji utakayochagua huamua muda utakaochukua ili kupokea pesa zako na kiasi cha ada kitakachotumika kwa shughuli. Utoaji wa pesa kwa simu huchukua dakika chache na ada ni kati ya 1.4% -1.7% huku uondoaji wa akaunti ya benki huchukua takriban masaa 24-48 na ada ya kutoa ni Shilingi 80 za Kenya.

Withdraw

Kwa uondoaji wa akaunti ya benki, utahitajika kujaza maelezo yako ya benki kama ifuatavyo

Bank_Details

Kwa uondoaji wa pesa kwa simu, utapata ujumbe wa uthibitisho wa Mpesa.

Ikiwa ungependa kumtumia Sallyanne ADA kama shukrani kwa kazi hii muhimu, tuma kwa AdaHandle $Sallyanne

Get more articles like this in your inbox

Was the article useful?

Or leave comment
Share
Commenter avatar

Thank you for sharing this information. It is very useful and informative. I appreaciate the fact that it eliminates middlemen which can help reduce cost and improve efficiency. Much appreciated from Nairobi Kenya.

avatar
You can use Markdown
avatar
You can use Markdown
close

Playlist

  • EP2: epoch_length

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 3 se. 24
    Darlington Kofa
  • EP1: 'd' parameter

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 4 se. 3
    Darlington Kofa
  • EP3: key_deposit

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 3 se. 48
    Darlington Kofa
  • EP4: epoch_no

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 2 se. 16
    Darlington Kofa
  • EP5: max_block_size

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 3 se. 14
    Darlington Kofa
  • EP6: pool_deposit

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 3 se. 19
    Darlington Kofa
  • EP7: max_tx_size

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 4 se. 59
    Darlington Kofa
0:00
/
~0:00