Tangazo: LidoNation yazindua Cardano Blockchain Lab nchini Kenya

Lido Nation inajivunia kutangaza uzinduzi wa Ngong Road Blockchain Lab huko Nairobi, Kenya!

Mwaka jana, Lido Nation iliungana na kundi la vijana waliohitimu chuo kikuu, ambao walifanya kazi nasi tulipoanza kuchunguza jinsi mpango wa ushirikiano na mafunzo unavyoweza kuonekana nchini Kenya. Darlington alianzisha programu ya ushauri wa wasanidi pamoja na vijana wawili, na Stephanie aliongoza “mradi wa majaribio” na kikundi kingine ili kutafsiri baadhi ya makala yetu katika lugha ya Kiswahili, mojawapo ya lugha rasmi ya Kenya.

Mradi wa utafsiri wa Kiswahili ulisababisha mojawapo ya mapendekezo yetu ya kwanza yaliyofadhiliwa kwenye Project Catalyst- ili kutafsiri tovuti yetu yote kwa lugha ya Kiswahili! Katika awamu itakayofuata ya project catalyst, juhudi za pamoja za washauri wa wasanidi programu na timu yetu mpya ya utafsiri zilisaidia kupata kura za NDIYO kwenye pendekezo letu kuu la project catalyst kufikia sasa, ili kuanzisha Maabara rasmi ya Cardano nchini Kenya.

The Ngong Road Blockchain Lab pia iliwezeshwa kupitia ushirikiano na Friends of Ngong Road (FoNR), Ngong Road Children’s Foundation (NRCF), na mpango mpya wa mafunzo wa TechMates ulioanzishwa. FoNR/NRCF hutoa elimu na usaidizi kwa vijana wa Nairobi ambao vinginevyo wasingeweza kupata elimu bora. TechMates ni programu mpya ya mafunzo iliyoanzishwa, inayofanya kazi kusaidia kuzindua wahitimu wa programu katika taaluma zao katika ulimwengu wa teknolojia. Ni vijana katika mpango huu ambao wanazindua maabara pamoja nasi.

“Pata maelezo zaidi kuhusu project catalyst, Friends of Ngong Road, na Techmates - katika viungo vilivyo hapa chini!) “ Katika kipindi cha miezi tisa zijazo, tutakuwa tukiendeleza na kupanua programu zetu kwenye Maabara. Washiriki katika Maabara ni wakandarasi wanaolipwa na Lido Nation (inayofadhiliwa kupitia Project Catalyst), kwa hivyo wanaweza kutenga wakati na bidii kujifunza na kukua pamoja nasi.

“Programu ya ushauri wa wasanidi itakaribisha vikundi vipya vya washauri; Darlington ataendelea kuongoza programu hii, lakini pia tutategemea washiriki wetu waliobobea kutenda kama washauri, na kuanza kuchukua majukumu ya uongozi kwa vikundi vya siku zijazo. Washauri wanaomaliza programu watakuwa wamepata ujuzi muhimu wa kupanga programu za blockchain, ambazo zitafungua fursa nyingi za kazi kwao. “ Mpango wa kutafsiri utaendelea pia, na kisha kuanza kubadilika kadiri timu ya sasa ya utafsiri “inapojihusisha” na utafsiri wa Lido Nation katikati ya majira ya joto. Ingawa utafsiri umekuwa kipaumbele chao cha kwanza, timu ya kutafsiri pia imepewa jukumu la kufanya “utafiti” kuhusu Cardano. Mafunzo haya kwa sehemu kubwa ni ya kufahamisha ujuzi wao wa utafsiri, lakini pia itawasaidia kuwatayarisha kwa ajili ya majukumu yao yanayofuata wakiwa na Maabara na zaidi. Mradi wao mpya wa kwanza utakuwa kuandika nakala asili za Cardano - kwa kutumia lugha ya Kiswahili! Watatoa tafsiri za Kiingereza pia, lakini tunafurahi kuweza kuanza kutoa maudhui ya Kiswahili kwanza kwa hadhira yetu mpya na inayokua barani Afrika.

Lengo letu linalofuata ni kuanza kuunda fursa za kazi kwa timu hii ya “Community Building” ndani ya mfumo wa ikolojia ya Cardano. Tunatengeneza mtaala ambao utawafundisha washiriki wa maabara jinsi ya kushiriki katika kazi ya kulipwa ndani ya jamii ya Cardano, tukianza na Ushauri wa Jamii kwa project catalyst. Kazi hii si lazima iwe rahisi, lakini inaweza kufikiwa kwa yeyote aliye tayari kuwekeza muda na juhudi. Katika siku zijazo, timu hii inaweza kusaidia kuwapa mafunzo washiriki wapya wa Maabara kuhusu kazi hii. “Pata habari zaidi kuhusu maabara kwa kuifuata kwenye Twitter: @NgongRoadLab

Pia tutakuwa tukituma sasisho za mradi hapa LidoNation.com - Viungo hapa chini“ Kila moja ya programu zetu kwenye Maabara ni mwanzo tu - tunatumai kila mtu ambaye anashiriki nasi kwenye Maabara atapata ukuaji wa kibinafsi na kupata fursa mpya kibinafsi. Pia tunatumai kuona ukuaji wa ufahamu na ushiriki katika Cardano, kwani washiriki wa Maabara wanaweza kuwa viongozi wa ndani kati yao. Tunajivunia kazi ambayo TechMates wamefanya kufikia sasa, na tunatazamia kuendelea kufanya kazi nao - kwa sababu wakati ujao ni wa kila mtu!

"Pata habari zaidi kuhusu maabara kwa kuifuata kwenye Twitter: @NgongRoadLab

Pia tutakuwa tukituma sasisho za mradi hapa LidoNation.com - Viungo hapa chini"

Get more articles like this in your inbox

Ungetaka kujua nini kuhusa maabara haya?

Or leave comment
Share

No comments yet…

avatar
You can use Markdown
close

Playlist

  • EP2: epoch_length

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 3 se. 24
    Darlington Kofa
  • EP1: 'd' parameter

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 4 se. 3
    Darlington Kofa
  • EP3: key_deposit

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 3 se. 48
    Darlington Kofa
  • EP4: epoch_no

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 2 se. 16
    Darlington Kofa
  • EP5: max_block_size

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 3 se. 14
    Darlington Kofa
  • EP6: pool_deposit

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 3 se. 19
    Darlington Kofa
  • EP7: max_tx_size

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 4 se. 59
    Darlington Kofa
0:00
/
~0:00