Zaidi ya Bloki

Je, unajua NFT zako ziko wapi?

Kama jamii tunayopenda teknolojia ya blockchain, tunazungumzia kuhusu kuweka mambo mengi kwenye blockchain. Blockchain inatoa faida za kudumu, usalama, na utawala usio wa kati. Watumiaji wanaweza kudhibiti wanachomiliki bila kuhitaji imani au idhini kutoka kwa mamlaka kuu au chama cha tatu.** Hivyo, ina mantiki kuwa hii inaweza kuwa na manufaa kwa mambo zaidi ya rekodi za kubadilishana fedha tu.** Katika makala nyingine, tumezungumzia kutumia blockchain kwa mambo kama mikataba, hati za umiliki, rekodi za elimu, nyaraka za utambulisho, na sanaa, kwa mfano, NFTs.

Kuna jambo muhimu kukumbuka, hata hivyo, kuhusu kutumia blockchain kufuatilia faili kubwa kama hati kubwa au NFTs: Mara nyingi zaidi, faili hizo HAZIKO moja kwa moja kwenye blockchain, zimefungwa kwenye kizuizi/bloki kwa wakati wote. Si kwa njia ileile ambayo rekodi za shughuli za kifedha zinavyofanyika, hata hivyo.

Kwanza kabisa, kwa nini siyo hivyo?

Jibu la haraka na rahisi ni ukubwa wa faili. Tabia/ Asili ya blockchain ni kwamba kila kitu lazima kiweze kusawazishwa kati ya nodi zinazoshiriki. Ikiwa kiasi cha data katika bloki kingekuwa kikubwa sana, kusawazisha bloki ingechukua muda mrefu sana, hivyo kutoa uwezekano mkubwa wa mashambulizi, hivyo kuathiri usalama. Ukubwa wa faili ya picha yenye ubora wa juu, kwa mfano, si tu kidogo zaidi ya rekodi ya shughuli rahisi - bali ni mara nyingi zaidi. Hatimaye, ukubwa mkubwa na usiozuilika wa bloki pia ungeathiri uwezo wa kusonga mbele, pamoja na kasi na usalama wake.

Kila blockchain inaainisha ukomo wake wa ukubwa wa bloki. Kwenye baadhi ya mtandao, ukubwa wa bloki ni kubwa ya kutosha hata kwamba ungeweza kuweka faili za ukubwa fulani zaidi kwenye bloki. Kikomo hicho si kuhusu ikiwa ni rekodi ya shughuli, au NFT, au kitu kingine chochote. Kwa kweli, vyote ni tarakimu 1 na 0 kwa wakati fulani! Kikomo halisi ni ukubwa wa data hiyo. Kwa mfano, Cardano ina kikomo cha ukubwa wabloki kidogo zaidi kuliko baadhi ya mitandao mengine. Moja ya sababu za uamuzi huo ilikuwa kukuza na kutekeleza wazo kwamba si kila kitu kinapaswa kuwekwa moja kwa moja KWENYE blockchain.

Basi inafanyaje kazi?

Hivyo, ikiwa kitambulisho chako chenye thamani, NFT, au hati haipo moja kwa moja kwenye bloki, iko wapi? Na ikiwa haipo kwenye bloki, inamaanisha nini kuweka vitu hivi kwenye blockchain?

Kile kinachowekwa kwenye bloki si data ya faili lako, bali ni metadata - data inayoelezea nani, nini, wapi, na lini, kuhusu faili. Mara nyingine, pamoja na metadata, kazi ya hash hutumika kuunda uwakilishi mdogo, wenye ukubwa unaohitajika, wa data kubwa zaidi ya asili, ili kuweka kwenye mtandao kama ithibati.

LAKINI IKO WAPI??

Thamani ya kuweka kitu kwenye mtandao haiko tu katika kujua kuwa imehifadhiwa. Kwa mfano, kwa JPG nzuri, unaweza kuwa unataka kuiona!

Kidhahania inawezekana kwamba JPG inaweza tu kuhifadhiwa mahali fulani, huku metadata ya blockchain ikielekeza mahali ilipo. Hata hivyo, hifadhi ya jadi ni ya kati, isiyo salama na haidumu. Kwa hivyo haipaswi kushangaza kwamba wajenzi wa blockchains wamegeukia njia mpya za kutatua tatizo hili. Mbili zinazotumiwa zaidi ni IPFS na Aweave.

The InterPlanetary File System (IPFS)

IPFS ni mfumo wa kugawana faili uliopo huria, uliogawanyika, na wa rika kwa rika. Maelfu ya washiriki kote ulimwenguni wanashiriki katika kazi ya kuhifadhi data na kutoa data hiyo wakati inapohitajika. Kila wakati faili inapohitajika, inapitia nodi kadhaa za mtandao wa rika kwa rika, ikiacha nakala zake popote inapokwenda. Faili zinazohitajika mara nyingi daima zipo tayari na nakala mpya zilizohifadhiwa kwenye nodi nyingi. Faili ambayo mara nyingi huitajika kwenye IPFS inaweza kuwa ya kudumu kweli.

Hata hivyo, uhifadhi uliopo kwenye kila nodi ya IPFS una kikomo. Wakati nodi inapofikia kikomo cha uwezo wake, faili za zamani zaidi ambazo hazijatazamwa sana huondolewa. Ikiwa faili kwenye IPFS haitahitajika kamwe, nakala zote zake hatimaye zitaondoka kwenye mtandao. Kukabiliana na hilo, kampuni zilianzishwa zinazotoa huduma inayoitwa “pinning services” au “huduma za kufunga.” Kwa ada, watakubali jukumu la kuhakikisha faili lako kwenye IPFS linaendelea kuwa salama na haliondolewi. Ikiwa unataka kununua NFT au kutumia huduma inayoshiriki faili kwenye IPFS, unaweza kutaka kujua ikiwa mradi huo unalipia huduma ya kufunga, au ikiwa ni juu yako kuhakikisha faili zako zinabaki mpya.

Arweave

Arweave ni suluhisho linaloshughulikia tatizo la kudumu. Arweave inatumia muundo ambao ni kama wa blockchain. Tofauti na IPFS, waendeshaji wa nodi wanahamasishwa moja kwa moja, kama waendeshaji wa nodi za blockchain zozote. Kwa hiyo, kutumia Arweave sio bure. Hata hivyo, gharama ni ndogo sana na gharama hiyo inatabirika. Kama huduma, Arweave inatoa njia ya kutazama faili zako kwa urahisi, ambayo ni ya manufaa. blockchain nyingi hutumia Arweave kwa uhifadhi wa faili, kwa sababu kwa gharama iliyowekwa na inayofaa, unahakikishiwa uhifadhi salama ambao unapaswa kudumu kwa muda mrefu sana.

Nini kuhusu faragha??

Ikiwa faili yako inasambaa katika mtandao wa kushiriki faili rika kwa rika, au kwenye blockchain ya umma, hiyo inamaanisha yeyote anaweza kuiona. Ikiwa ni faili ya .jpg, wanaweza kuiona kwa kutumia programu yoyote ya kuonyesha picha. Ikiwa ni faili ya .doc au .txt, wanaweza kuisoma. Inawezekana kutumia mifumo hii na faili “zisizo salama” za aina hizi; kwa kweli, zinaweza kutumiwa haswa kwa kushiriki faili kwa njia ambayo kwa makusudi ni ya umma. Hata hivyo, ikiwa faragha, ulinzi wa hakimiliki, au kipekee ni muhimu, faili zinaweza kusimbwa kwa njia fiche kabla ya kuziweka kwenye IPFS na Arweave.

Kupima chaguzi

IPFS ni bure kutumia, imekuwepo kwa muda mrefu, ina zana nyingi zaidi za mfumo wa ikolojia, na inaendana sana na mifumo iliyopo. Inaweza kuwa bure. Walakini, haidumu - au lazima utumie zaidi ili kuifanya iwe ya kudumu.

Arweave inatoa suluhu ya kweli kama blockchain, yenye uimara wa juu sana kwa gharama isiyobadilika ya chini. Hata hivyo mustakabali wa Arweave haujulikani. Ikiwa uchumi wa hazina na motisha za nodi hazifanyi kazi kwa njia ifaayo, gharama zinaweza kubadilika siku moja, au uwezekano wa biashara nzima unaweza kutiliwa shaka. Kwa sasa, hata hivyo, inaonekana kama suluhisho bora kwa uhifadhi wa faili wa muda mrefu, uliogawanywa.

Kwa mradi wa NFT wa hapa Lido Nation, tulichagua Aweave. Tulifanya uamuzi huo kulingana na upendeleo wetu, katika kesi hii, kwa uimara mkubwa kwa gharama isiyobadilika na ya bei nafuu. Inawezekana kwamba tungechagua IPFS kwa mradi tofauti. Ikiwa mradi haukuhitaji uimara wa muda mrefu, tungetumia IPFS kwa sababu ni bure. Vile vile, ikiwa kulikuwa na dhamana ya maslahi yanayoendelea katika faili, IPFS inaweza kudumu na bila malipo, na itakuwa chaguo nzuri.

Kwa siku za usoni, eneo la uhifadhi wa faili thabiti na usio na mshiko litazidi kuendelea kubadilika. Arweave na IPFS wanaweza kuongezeka au kupungua, na suluhisho mpya yanaweza kutokea. Kuwa na ufahamu wa mambo na mawazo yaliyoelezwa hapa inaweza kusaidia kuelewa vizuri miradi unayochagua kushiriki ndani yake.

Get more articles like this in your inbox

Was the article useful?

Or leave comment
Share

No comments yet…

avatar
You can use Markdown
close

Playlist

  • EP2: epoch_length

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 3 se. 24
    Darlington Kofa
  • EP1: 'd' parameter

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 4 se. 3
    Darlington Kofa
  • EP3: key_deposit

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 3 se. 48
    Darlington Kofa
  • EP4: epoch_no

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 2 se. 16
    Darlington Kofa
  • EP5: max_block_size

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 3 se. 14
    Darlington Kofa
  • EP6: pool_deposit

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 3 se. 19
    Darlington Kofa
  • EP7: max_tx_size

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 4 se. 59
    Darlington Kofa
0:00
/
~0:00