Pochi la crypto: Kituo chako cha uraia wa cardano

Pochi lako la crypto ndio sehemu kuu zaidi ya muingiliano wako wa kibinafsi na mtandao wa blockchain. Licha ya hali yao ya msingi, chaguzi na maelezo ya kimsingi kuhusu pochi za crypto si rahisi kuelewa.

Kimsingi, pochi la crypto huhifadhi nakala ya funguo za kidijitali zinazodhibiti mali yako yote kwenye blockchain. Katika tamaduni za Magharibi, pochi ndicho kitu ambacho watu wengi hutumia kuweka pesa, aina ya kitambulisho, kadi za uwanachama, na picha za watoto wao au wanyama. Tofauti na pesa taslimu au picha za paka wako, mali ya crypto huhifadhiwa kwenye mtandao wa blockchain ambao husambazwa kote ulimwenguni. Unaweza kufikiria pochi lako la crypto zaidi kama uwazi au programu ya kuingiliana na mali yako ya crypto kwenye mtandao wa kimataifa wa blockchain. Kadiri matumizi ya teknolojia ya blockchain yanavyobadilika na kukua, hasa katika Cardano, pochi za Crypto zitakuwa matumizi yenye nguvu zaidi, na uwezekano wa kuwa “kituo cha uraia wa kidijitali.”

Leo hii, pochi nyingi hukuwezesha kuingiza funguo zako za kidijitali ili uweze kutuma pesa na kuona ni pesa ngapi unazo kwenye mtandao wa blockchain. Kwa kawaida, unatakiwa kuweka nenosiri yako mara moja, kwa sababu pochi huhifadhi nakala yake ili muingiliano wa siku zijazo uwe wa kasi. Kabla ya kujifunza kidogo zaidi kuhusu mipango ya kusisimua ya pochi za cardano, hebu tuangalie kwa haraka aina tofauti za pochi ambazo unaweza kusikia kuhusu: hosted wallets, non-custodial wallets, na hardware wallets..

Hosted wallets

Hizi ni pochi ambazo funguo zake za kidijitali zimeundwa na kumilikiwa na mtoa huduma wa tatu. Unapoweka crypto yako kwenye hosted wallet, unamwamini mtoa huduma huyo kuiweka crypto yako, kama vile benki inavyofanya kwa sarafu za fiat. Hosted wallets maarufu zaidi ni crypto za kubadilishana; Bitpoint, Coinbase, binance, ni mifano michache. Mifumo hii hukupea jina la mtumiaji na nenosiri ambalo hukuwezesha kudhibiti crypto yako.

Hosted wallets sio za kutisha kimatumizi kwa wageni, lakini pia zina vizuizi. Mabadilishano yanalenga tu kununua na kuuza crypto. Watumiaji hawawezi kutekeleza utendakazi nyingine ya blockchain, kama vile kuchagua staking pool, kupiga kura, kufanya biashara za NFT, au kuingia kwenye tovuti.

Non-Custodial wallets

“Non-custodial wallets”au “self custody” ni programu tumizi zinazokuwezesha kuunda funguo zako za kidijitali za blockchain na kuingiliana na blockchain moja kwa moja kwenye kompyuta au simu yako ya kibinafsi . Pochi hizi zipo katika aina mbili. Aina ya kwanza huweka nakala ya blockchain nzima kwenye kompyuta yako. Unapotumia pochi hili, si lazima upitie kwenye seva za mbali; nakala ya blockchain nzima ipo kwenye kifaa chako. Aina ya pili inajulikana kama “light wallet.” light wallet nzuri ,bado huunda funguo zako kwenye kifaa chako mara ya kwanza unapoitumia. Kazi zinazohitaji matumizi ya funguo hutekelezwa ndani ya kifaa chako kabla ya kutumwa kwa seva za mbali ili kusawazisha na blockchain. Self-custody wallet kwa kawaida huwa na kipengele kamili, huku ikikuruhusu kutekeleze vitendo vyote vinavyowezekana ukiwa na mali yako moja kwa moja kwenye pochi.

Hardware wallets

Hardware wallet ni kifaa halisi, mara nyingi huwa na umbo la USB. Nakala ya funguo zako huundwa na kuhifadhiwa kwenye kifaa hiki halisi. Kuweka nakala ya funguo zako kwenye maunzi, tofauti na kompyuta au simu yako, hufanya iwe vigumu kwa crypto yako kuibiwa ikiwa kompyuta yako imedukuliwa. Ili kufanya vitendo vingi, unapaswa kuunganisha hardware wallet yako kwenye kompyuta au simu yako na uthibitishe vitendo vyako kwa kubofya kitufe kwenye kifaa.

Uwazi wako wa programu ndani ya blockchain

Kwa kila aina hizi za pochi, tumejadili “funguo” ambazo zinadhibiti mali yako ya kidijitali. Unapojihusisha na blockchain kwa mara ya kwanza, isipokuwa ukitumia suluhisho lingine au suluhisho lingine la hosted wallet, hatua ya kwanza ni kuunda ufunguo wako wa kidijitali. Ufunguo huu kwa kawaida ni nenosiri la dokezo la maneno 15 au 24,ambalo linalotolewa na programu la pochi. Ufunguo huu wa nenosiri huthibitisha uwepo wako kwenye mtandao. Unapopokea mali, sehemu ya umma ya ufunguo huu hutumika kutia sahihi au kuweka muhuri wa mali hizi. Unapotuma mali ya kidijitali kwa mtu mwingine au kuibadilisha, unatoa idhini yako kwa kutumia sehemu ya faragha ya ufunguo wako.

Ingawa programu za pochi zinakusaidia kuunda ufunguo wako wa umma na wa kibinafsi kwa namna ya maneno, ni muhimu kujua kwamba kampuni ya pochi haimiliki ufunguo wako, au kuijua. Funguo zinazalishwa moja kwa moja kwenye kompyuta yako ili pasiwe na mtu mwingine au kampuni iliyo na nakala yake. Blockchain si seva kuu. Ipo kwa maelfu ya vifaa kila mmoja na nakala ya mtandao. Unaweza kutumia funguo sawa ili kufikia mali yako ya kidijitali kwenye pochi yoyote kwa kutumia simu au kompyuta, ikiwa pochi huo hutoa msaada kwa aina yako ya ufunguo. Unaweza hata kuweka ufunguo wako katika pochi mbili tofauti na wakati huo huo, kutumia vipengele tofauti. pochi hilo ni uwazi tu wa kutazama mtandao wa blockchain. Hii ndiyo sababu ni muhimu kutumia pochi ambazo zinatengenezwa au kupendekezwa na timu inayojenga mtandao wa blockchain unaoutumia. Ni muhimu kupakua programu yako ya pochi moja kwa moja kutoka kwenye tovuti ya kampuni inayotengeneza pochi hiyo. Pochi hufanya kazi kwa kutumia maneno yako ya siri; Ikiwa unaweka maneno yako ya siri ndani ya pochi bandia, watendaji wabaya wanaweza kuiba mali yako. Hii ni kama kuweka nenosiri lako la benki kwenye tovuti bandia. Katika kesi ya crypto hata hivyo, shughuli haiwezi kubadilishwa. Ikiwa mtu anapata nenosiri yako na kuiba crypto yako, hakuna malipo.

Pochi zilizoko kwenye cardano

Cardano inatengenezwa kwa zaidi ya pesa tu. Kwenye Cardano, unaweza kupiga kura, unaweza kuweka hisa, kutuma na kupokea NFTs, na bila shaka unaweza kutuma na kupokea ADA. IOG, msanidi mkuu wa mtandao, ameonyesha nia ya kutengeneza pochi ya Cardano ya Daedalus kuwa “kituo cha raia wa kidijitali.” Wazo hili bado ni la dhahania, lakini inafurahisha kuzingatia jinsi pochi za Cardano zinavyoonekana na kile wanakuruhusu kufanya wakati mtandao unaendelea kukua na kukuza. Hebu fikiria kufungua pochi yako ya kidijitali na kuona hati zako zote za malipo, taarifa za kodi na rekodi za matibabu, zote kutoka kwa programu moja. Na kwa kuwa mtoa programu hatamiliki data yako - kwa sababu wao ni uwazi wa programu tu kwenye blockchain - wasanidi watakuwa na ushindani mzuri kila wakati kutengeneza pochi bora zaidi.

Get more articles like this in your inbox

Je, kunayo jambo jipya umejifunza kwa kusoma makala haya?

Or leave comment
Share

No comments yet…

avatar
You can use Markdown
close

Playlist

  • EP2: epoch_length

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 3 se. 24
    Darlington Kofa
  • EP1: 'd' parameter

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 4 se. 3
    Darlington Kofa
  • EP3: key_deposit

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 3 se. 48
    Darlington Kofa
  • EP4: epoch_no

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 2 se. 16
    Darlington Kofa
  • EP5: max_block_size

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 3 se. 14
    Darlington Kofa
  • EP6: pool_deposit

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 3 se. 19
    Darlington Kofa
  • EP7: max_tx_size

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 4 se. 59
    Darlington Kofa
0:00
/
~0:00