Cardano Cash! AHHHHHHH !!!

Takriban wiki moja iliyopita Mkurugenzi wa Uendeshaji wa shughuli za Afrika za Cardano alituma ujumbe kwenye mtandao wa Twitter kama vile habari ambayo kwa kiasi kikubwa haukutambuliwa na vyombo vya habari vya crypto. Sisi hapa LIDO Nation tunadhani hii ilikuwa yakuvutia kama mwanadamu kutua mwezini kwa mara ya kwanza. Changamoto yenyewe sio ile iliyochukuliwa na miradi mingine yoyote ya crypto, na tunajua kuhusu miradi mingine mingi ya crypto. Bila shaka, hatuwezi kujua kila mradi wa crypto. Baada ya kusoma makala haya, ikiwa unajua mradi mwingine unaojaribu kutatua tatizo sawa, tafadhali tujulishe katika maoni; kutatua tatizo la “fedha” katika crypto ni hitaji la kuchukua nafasi ya fedha zetu za sasa.

Nimeona onyesho la shughuli ya nje ya mtandao la #Cardano including #Ada na mali nyingine asili ambayo ilinisisimua. Usaidizi kwa simu yoyote ya android kwa miaka 5 iliyopita. Mambo machache ya kusuluhisha lakini kesi za utumiaji vimepita kiasi. @InputOutputHK

Blockchain na cryptocurrency ni za kidigitali. Msingi wa blockchain ni wazo la kuweka vitu vinavyoonekana viwe vya kidigitali ili kulinda haki ya umiliki kutoka kwa kampuni moja au serikali. Jina la mtaani linalovuma zaidi ya crypto ni “pesa ya mtandao.”

Cardano Cash ni nini? Kama kipengele cha jinsi Cardano imeundwa, shughuli za Cardano karibu kila mara zinahitaji taarifa kidogo tu. Iwapo ungemtumia jirani wako Juma dola 800 katika ADA kwa ajili ya gari lake, hivi ndivyo shughuli hiyo ingefanyika hivi. Kompyuta yako (au simu) itaambia mtandao wa Cardano: “Hivi ndivyo vitu vitatu ambavyo namiliki kwa sasa. Hii hapa ni uthibitisho wangu kwamba namiliki vitu hivi. Pamoja vitu hivi ni vya thamani ya dola 900. Nataka uweke vitu hivi vitatu pamoja, kisha uunde vitu viwili vipya. Moja yenye thamana ya dola 800, na nyingine la dola100 (aina ya jinsi rejesta ya pesa inaweza kufanya kazi kwenye duka). Badilisha mmiliki wa dola 800 kuwa Juma, na unifanye mmiliki wa dola100 zilizosalia.

Kwa kawaida unapofanya hivi kwenye simu au kompyuta yako, kifaa chako kitakuwa kikiwasiliana na kompyuta zote duniani zinazounda mtandao wa cardano kwenye mtandao.. Cardano cash ni wazo la, badala ya kulazimishwa kuwasiliana na mtandao mzima wa Cardano kutumia Juma dola 800, vipi ikiwa simu yako inahitaji kuwasiliana na simu ya Juma.

Hii inaleta changamoto kwa sababu chache. Changamoto moja ni, simu ya Juma inajuaje kwamba kweli unamiliki vitu vitatu unayoweka kwenye shughuli? Kwa ujumla, kuthibitisha kuwa unamiliki vitu vinavyotengeneza dola 900 ndiyo kompyuta kwenye mtandao wa Cardano hufanya. Ili kutatua hili, tutahitaji njia ya kuhamisha yote au baadhi ya vitu unavyomiliki kutoka kwa mtandao hadi kwa simu yako au kifaa kingine. Kwa hivyo mkusanyiko wako wa vitu utafutwa kutoka kwa mtandao wa Cardano (au kusmamishwa), na kuhamishwa kwenye simu yako. Kama sehemu ya uhamisho huu, mtandao utahitaji kukupa aina fulani ya cheti ambayo simu ya Juma inajua jinsi ya kuthibitisha. Kwa cheti hicho, simu ya Juma inaweza kusema, ndiyo, mambo haya ni ya kweli; Ndiyo, unamiliki zote tatu. Simu ya Juma itahitaji kuthibitisha kwamba mara tu unapomtumia kitu cha thamani ya dola 800, unaharibu nakala yako hivyo Juma ni mmiliki pekee. Wakati wewe au Juma mko tayari, kwa tarehe ya baadaye, unaweza kuhamisha vitu unavyomiliki kutoka kwenye simu zako hadi kwenye mtandao wa Cardano.

Je! Hiyo inaonekana kama jinsi pesa inavyofanya kazi kwa sasa? Unaweza kuenda kwenye benki yako, kuchukua fedha. Kulipa mtu. Wanaweza kuiangalia na “kuthibitisha” kwamba ni ya kweli, kwamba haukuipata kwa njia isiyo sawa. Wanaweza kukupa chenji ikiwa unawapa tatu 20 kwa kitu kinachogharimu 50. Na nyote wawili mnaweza kurudi kwenye benki yako na kuweka pesa wakati unavyopenda.

Hii ni kurahisisha kupita kiasi lakini hii kimsingi ndio changamoto ya Crypto Cash. Cardano inasema kuwa imeendesha mtihani wa mafanikio. Hii ni kubwa! Hii ina maana kuwa watu wanaweza kupata faragha sawa na wanayopata kutoka kwa pesa sasa, huku wakipata vipengele vingi vipya. Crypto, kwa kuwa ni “ya kidijitali” ni rahisi sana kusafiri nayo. Mikoa kote ulimwenguni ambayo haiishi kwenye mtandao wakati wote yanaweza kuwa na crypto! Hii inamaanisha kuwa biashara ndogo ndogo zinaweza kukubali malipo salama kwa shughuli za dola sufuri. Hebu niseme hiyo tena. Hii ina maana kuwa biashara ndogo ndogo zinaweza kukubali malipo salama kwa dola sufuri.

Changamoto nyingine ya Crypto Cash, na pengine ile ngumu zaidi, ni tatizo la udukuzi. Ni vipi tunaweza kuzuia programu kwenye simu yako na ya Juma dhidi ya udukuzi? Kwa upande mwingine, unaweza kuwa na mtu anayepiga simu kuwa kimsingi kuweka nakala ya “fedha” wanatumia na kamwe wasiishiwe na pesa! Tunawezaje kusasisha programu kwa njia iliyosalama? Tweet ilitaja simu kutoka miaka 5 iliyopita kwa sababu vifaa hivi vipya vina kitu kinachoitwa mazingira ya vifaa vya kuaminika. Unapotumia kificho kwa vifaa hivi, vinahakikisha kuwa kanuni haiwezi kubadilishwa mara tu inapowekwa.

Ni nini kinachotokea unapopoteza simu yako? Kitu kimoja kinachotokea unapopoteza pochi lako! Tunafurahi kuona maendeleo ya cardano Cash na tutakua makini kwa maendeleo na hatua zozote.

Get more articles like this in your inbox

Was the article useful?

Or leave comment
Share

No comments yet…

avatar
You can use Markdown
close

Playlist

  • EP2: epoch_length

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 3 se. 24
    Darlington Kofa
  • EP1: 'd' parameter

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 4 se. 3
    Darlington Kofa
  • EP3: key_deposit

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 3 se. 48
    Darlington Kofa
  • EP4: epoch_no

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 2 se. 16
    Darlington Kofa
  • EP5: max_block_size

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 3 se. 14
    Darlington Kofa
  • EP6: pool_deposit

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 3 se. 19
    Darlington Kofa
  • EP7: max_tx_size

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 4 se. 59
    Darlington Kofa
0:00
/
~0:00