Tuangazie Wada

Katika hazina maalum ya Project Catalyst ya 6, Lido Nation ilifadhiliwa kufanya kazi na kikundi cha wazungumzaji asilia wa Kiswahili nchini Kenya. Tuliwasaidia kujifunza kuhusu Cardano, kutafsiri makala za Lido Nation katika Kiswahili, na hatimaye kuandika maudhui yao halisi kuhusu Cardano kwa hadhira inayozungumza Kiswahili. Makala haya ni sehemu ya mfululizo wa maudhui ya Kiswahili, yaliyotafsiriwa kwa Kiingereza!

Katika makala yangu iliyopita nilizungumzia kuhusu Cardano barani Afrika. Cardano inashirikiana na nchi za Afrika kujenga miundombinu na kutatua matatizo ya ulimwengu halisi kwa kutoa rasilimali muhimu - huku Cardano akifaidika kwa kujulikana na kukubalika na watu wengi. Tulizungumza kuhusu Cardano nchini Kenya, Tanzania na Ethiopia. Kusoma zaidi kuhusu makala hii hapa kuna kiungo https://www.lidonation.com/en/posts/cardano-in-Africa.

Wada

mustakabali mzuri wa Afrika na cardano huenda pamoja. Katika Afrika kuna muungano ambao ni mtandao wa rasilimali kwa ajili ya kufungua uwezo wa Afrika na nje ya africa kwa kusambazwa kwa ya leja teknolojia, maarifa. Shirika linalofanya hivi lilianzia Afrika Magharibi, na kujiita “West Africa Decentralized Alliance (WADA)”. Tangu wakati huo, na kama utakavyoona hapa chini, kazi yao imekua haraka, na haiko tena Afrika Magharibi tu. Kwa hivyo, hawatumii tena jina lililojanibishwa - sasa ni “Wada.” Wada ni muungano wa kimataifa wenye nyayo za ndani, ambao huwapa wasanidi programu wa ndani na wajasiriamali kujenga programu na biashara zilizogatuliwa kwa ajili ya maisha yao ya baadaye.

Wada ina nguzo tatu ambazo ni:

Miundombinu na kujenga uwezo/ maendeleo

Elimu

Uundaji wa Dapps

Wada huwapa wasanidi programu nyenzo kama vile ushauri na usaidizi wa usanifu na mkakati wa utekelezaji wa Dapps. Wada pia hutoa elimu na mafunzo kuhusu projet catalyst - kuwafanya wajasiriamali na wanafunzi wa Kiafrika kufahamu kuhusu project catalyst na fursa inazotoa.

Wada katika project catalyst

Wada ilikuwa na miradi kadhaa iliyowasilishwa katika hazina maalum ya 4, 5, 6, 7 na 8 wa Kichocheo cha Mradi.

Katika hazina maalum ya 4 walikuwa na mradi unaoitwa “West Africa Proposer Outreach” ambao ulifadhiliwa. Lengo lilikuwa kutoa mafunzo, elimu na jukwaa mtandaoni ili kuwafahamisha wajasiriamali wa Afrika Magharibi kuhusu ufadhili wa Project Catalyst. Mradi huu umekamilika! Katika awamu hiyo hiyo ya ufadhili pia walikuwa na miradi mingine iliyofadhiliwa pia: “West Africa devs tools and events “, “Local centers in west Africa “, na “West Africa catalyst onboarding .” Unaweza kuangalia miradi hii na maendeleo yake hapa kwenye Lido Nation kwa kutumia zana zetu za Kichunguzi cha project catalyst.

proposals ids=3254,3277,3093,3263]

Katika hazina maalum ya 5 , “Media funnel for proposers” ilikuwa mojawapo ya miradi yao iliyofadhiliwa ambapo walipaswa kuunda maudhui ya kuona ya kuvutia ili kuandika safari za mapendekezo kutoka chini kwenda juu na pia kuhimiza watumiaji wapya kujiunga na project catalyst. “Wada university students catalyst registry” ulikuwa mradi mwingine uliofadhiliwa katika hazina maalum ya 5. Lengo la mradi huu lilikuwa kushirikisha wanafunzi wa vyuo vikuu katika programu za Project Catalyst kupitia elimu na ushirikishwaji wa jamii. Miradi hii yote miwili imekamilika!

WADA Media Funnel for Proposers

$12,000 Received
$12,000 Requested

Solution: Create engaging visual content to document proposal journey from the bottom up, and to motivate new users to come to into Project Catalyst.

Fund: Fund 5 Challenge: F5: Proposer Outreach
funded Awarded 12% of the fund.
4.36 (11)

WADA Uni Students Catalyst Registry

$11,000 Received
$11,000 Requested

Solution: Diversify project catalyst inclusion through onboarding, navigation events, and resource provision for university students in West Africa

Fund: Fund 5 Challenge: F5: Catalyst Value Onboarding
completed Awarded 11% of the fund.

Katika hazina maalum ya 6 WADA ilikuwa na miradi kadhaa. Kwanza, “Strengthening stake pools in Africa ’ kulidhamiria kubuni mfumo wa kipekee mahususi kwa ajili ya changamoto za kipekee za kuendesha kundi la wadau na kuunda bwawa la kujifunza. Mradi wa pili ulikuwa “Scale up WADA`s outreach”; mradi huu ulikuwa wa kutoa mafunzo kwa washauri ili kusaidia wajasiriamali wanaotaka kuwasilisha mapendekezo bora. Mradi wa tatu ulikuwa “Green Lion (GL) leading in Ghana’’ ambapo WADA inafanya kazi kwa ushirikiano na Green Lion ili kuendeleza mabwawa ya kujiendesha ya ukwasi kwa ajili ya kutoa biashara kwa mikopo ya gharama nafuu kwa sekta isiyo rasmi ya Ghanian. Muda mfupi baada ya Fund 6, Green Lion ilinunuliwa na mshindani wake, TradeDeopt.co - na tunashangaa jinsi mabadiliko hii inaweza kuathiri mradi! Hii ni miradi michache tu iliyofadhiliwa katika hazina maalum ya 6; miradi hii bado inaendelea.

Green Lion (GL) lending in Ghana

$15,000 Received
$15,000 Requested

Solution: Wada + Green Lion seek to develop self-sustaining liquidity pools for providing low cost business loans to the Ghanaian informal sector

Fund: Fund 6 Challenge: F6: DeFi and Microlending for Africa
funded Awarded 16.667% of the fund.
3.44 (18)

Scale up WADA's Outreach Program

$7,000 Received
$7,000 Requested

<p> African devs and entrepreneurs lack support to submit high quality proposals into project catalyst</p>

Fund: Fund 6 Challenge: F6: DLT Entrepreneurship Toolbox
completed Awarded 4.667% of the fund.
4.47 (15)

Strengthening Stake Pools in Africa

$22,000 Received
$22,000 Requested

<p>Stakepools in Africa are subject to outages and infrastructure issues on top of the general risks faced by SPOs</p>

Fund: Fund 6 Challenge: F6: Disaster: When all is at stake
completed Awarded 14.667% of the fund.
4.67 (12)

Katika hazina maalum ya 7 Wada ilikuwa na miradi kadhaa. Moja ilikuwa, “Djangui: Local Savings Account Mgmt”. Madhumuni ya mradi huu ni kuunda jukwaa la ugatuzi la kusimamia shughuli zinazozingatia uwazi na haki za umiliki wa ukusanyaji wa fedha, kwani hapo awali wakusanyaji hawakuwa wawazi na waliweka watu kwenye udanganyifu. Mradi mwingine unaofadhiliwa ni, “Small Change Wallet”; hii ilikuja kama matokeo ya changamoto nchini Kamerun ambapo kupata mabadiliko sahihi ili kuendana na ununuzi wa bidhaa ilikuwa ngumu. wada inalenga kuunda tokeni asilia na pochi ili kusaidia kukusanya mabadiliko madogo. Hii ni baadhi tu ya miradi iliyopendekezwa katika hazina maalum ya 7 na wada; miradi bado inaendelea.

Djangui: Local Savings Account Mgmt

$24,000 Received
$24,000 Requested

Solution: Create a decentralized platform to manage collection activities focusing on: transparency and ownership rights of collected funds.

Fund: Fund 7 Challenge: F7: Boosting Cardano's DeFi
completed Awarded 4.8% of the fund.
4.78 (9)

Small Change Wallet

$4,500 Received
$9,000 Requested

Solution: Create a native token and a wallet to help collect small change making sure to incorporate an exchange platform with microfinance businesses

Fund: Fund 7 Challenge: F7: Mini/Low-Budget Dapps & Integrations
funded Awarded 4.5% of the fund.
4.44 (9)

hitimisho

** Kati ya mapendekezo 41+, Wada imeshinda ufadhili wa jumla ya miradi 19+ .**

Maelezo ya kikundi katika mfumo huu changa na uliogatuliwa si kamilifu na yanabadilika. Project Catalyst ni jaribio, na wachangiaji wake wote ni wanasayansi wadogo. Katika kipindi cha hazina maalum hizi za kwanza, muungano na ushirikiano umeundwa. Ni kama kuanzisha kampuni, na ni kama kuwa washirika wa maabara na rafiki yako bora. Vyovyote vile, kwa sasa si rasmi na ni vigumu kufuatilia - bado ni muhimu na ya kuvutia tunapotafuta kuelewa mazingira ya mfumo huu wa ikolojia unaoibukia! Unaweza kutazama zote - au nyingi! - ya miradi ya Wada kwenye ukurasa wa kikundi cha Wada wa zana yetu ya ugunduzi wa project catalyst : https://www.lidonation.com/en/project-catalyst/group/wada

Ufahamu wa Cardano umeongezeka kwa kiasi kikubwa katika Afrika. Cardano inalenga kutoa rasilimali zinazohitajika ili kufanya miradi barani Afrika ifanye kazi kwa kutoa huduma kama vile intaneti ya nguvu, mitandao, elimu na mafunzo kwa Waafrika Magharibi. Wada inalenga kuwezesha upatikanaji wa elimu ya blockchain na upanuzi wa biashara na huduma za ushauri kwa kuunganisha wafanyabiashara, wamiliki wa biashara na wasanidi programu kwenye mfumo wa ikolojia wa Cardano ili watimize ndoto zao.

Get more articles like this in your inbox

Was the article useful?

Or leave comment
Share

No comments yet…

avatar
You can use Markdown
close

Playlist

  • EP2: epoch_length

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 3 se. 24
    Darlington Kofa
  • EP1: 'd' parameter

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 4 se. 3
    Darlington Kofa
  • EP3: key_deposit

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 3 se. 48
    Darlington Kofa
  • EP4: epoch_no

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 2 se. 16
    Darlington Kofa
  • EP5: max_block_size

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 3 se. 14
    Darlington Kofa
  • EP6: pool_deposit

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 3 se. 19
    Darlington Kofa
  • EP7: max_tx_size

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 4 se. 59
    Darlington Kofa
0:00
/
~0:00