Mradi wa Project Catalyst: Majaribio Ndani ya Decentralized Autonomous Organization

Project Catalyst ni jaribio ndani ya ushirikiano na uvumbuzi kwa Cardano. Jaribio hili limewazeshwa na blockchain ya Cardano. Muundo wa project Catalyst ni mfululizo wa raundi za ufadhili, ambapo changamoto huwasilishwa, na mtu yeyote ulimwenguni anaweza kupendekeza masuluhisho. Jamii ya Cardano hupigia kura suluhu wanazopenda. Mapendekezo yanayoshinda hupokea ufadhili wa kuwasilisha suluhisho zao.

Katika Makala ya awali tulisoma kuhusu Decentralized Autonomous Organization (DAO) ambayo ni njia ya kupanga na kugawa kazi kwa kutumia blockchain. Na wiki iliyopita tulitaja ufadhili wa kibinafsi wa Hazina ya Cardano, ambayo inakuza maendeleo na uhifadhi wa mtandao. Project Catalyst ndipo dhana hizi mbili zinakutana. Ni mpango wa kwanza wa aina yake ambao unatafuta kuhamasisha “kiwango cha juu zaidi cha ushirikiano wa kibinadamu.”

Jaribio hilo

Jaribio la Project Catalyst lilianza na hazina maalum ya 1 mnamo Septemba mwaka wa 2020. Na tunapoandika nakala hii mnamo mwezi Agosti mwaka wa 2021, tupo katikati ya hazina maalum ya 6. Kila raundi imekuwa ikipata pesa zaidi katika Stake, matatizo zaidi ya kutatua, na watu wenye akili za ubunifu kujaribu kuzitatua. Kutoka ngazi ya juu, mchakato huo ni rahisi:

1) Changamoto:

Changamoto hizo zinazoitwa kampeni pia, zinatoa wito wa maeneo ya mtandao yanayohitaji maendeleo. Hapa kuna mfano kutoka kwa hazina maalum ya 6; Changamoto hii inaonyesha haja ya rasilimali ya lugha nyingi ili kukuza mtandao. Multilingual Resources Campaign

2) Mapendekezo:

Mtu yeyote anaweza kuwasilisha pendekezo, wakielezea jinsi wangetatua changamoto hiyo. Kama unavyoweza kufikiria, kuna njia mbalimbali za kukabiliana na haja ya rasilimali ya lugha nyingi! Katika mfano wa hapo awali, nambari ya “43” iliyo mwishoni mwa kurasa inawakilisha idadi ya mapendekezo yaliyowasilishwa kwa changamoto hii. Mapendekezo mazuri yanajumuisha mpango kamili, mradi wa ramani ya njia, na bajeti ya kina.

3) Kupiga kura:

Kwa sasa, yeyote aliye na angalau ADA 500 kwenye pochi inayoauni upigaji kura anaweza kupiga kura. Nilipiga kura kwa mara ya kwanza katika hazina maalum ya 5. Niligundua kuwa kupigia kura mawazo mengi ambayo yako nje ya anuwai ya uzoefu na ujuzi wangu ilikuwa ya kutisha na ya kusisimua . Kwa upande mmoja, ilikuwa fursa ya kujifunza mambo mapya na kupanua ujuzi wangu na ufahamu wa Cardano. Kwa upande mwingine, haikuwa lazima kwangu kuzingatia mapendekezo ya kiufundi ambazo zilikuwa nje ya maeneo yangu ya ujuzi na mvuto. Ikiwa ningependezwa zaidi na ufahamu kuhusu Rasilimali za Lugha nyingi, ningeweza tu kuzingatia umakini wangu na kura zangu katika eneo hilo. Kwa njia hii, ufadhili na mwelekeo wa mtandao unaundwa na maslahi yangu! Hatimaye, niligundua kwamba hata bila ufahamu wa kina wa kategoria za kiufundi sana, bado niliweza kusoma mapendekezo na kutambua yale ambayo yalionekana kuwa na maono wazi, mpango ulioelezwa vizuri, na vipimo vinavyoweza kupimika vya mafanikio. Kwa kura zangu, nilihimiza mapendekezo ya siku zijazo kuongeza kiwango cha kuunda na kuelezea mipango yao.

4) Ufadhili, Utawala, na zaidi …

Baada ya shughuli ya upigaji kura kufungwa, mapendekezo yaliyopita hupokea ufadhili. Hatua zifuatazo ni kwa washindi hawa kujenga na kutekeleza mapendekezo yao, na kwa wakaguzi kufuatilia na kuhakikisha kuwa uwekezaji wa jamii unatumika vizuri. Wakati awamu hizi za ujenzi na utawala zinaendelea tu, awamu inayofuata ya ufadhili inaanza - kila mzunguko ni fupi.

Project catalyst inaongozwa na IOG, kampuni iliyounda Cardano, na inafadhiliwa na Hazina ya Cardano, ambayo ni ya ufadhili wa kibinafsi wa mtandao. Sehemu ndogo ya kila ada ya mtandao wa Cardano inaelekezwa kwa hazina, mradi mtandao unaendelea na unatumika, kutaendelea kuwa na pesa za kutatua matatizo na uvumbuzi wa aina hii.

Project Catalyst $ Awarded by Round Number of Winning Proposals by Round

Zana ya project catalyst ya Lido Nation

Ikiwa ungependa kupata maelezo zaidi kuhusu mapendekezo ya project catalyst, Lido Nation imeunda maktaba, kwenye ukurasa wetu wa Hazina ya Cardano. Tuliunda zana hii kwa sababu tuligundua kuwa hakuna hifadhi inayoonekana kwa umma ya mapendekezo yote ya awali, yenye seti kamili ya zana za utafutaji na vichujio vya kuelewa historia kamili ya mradi. Kiolesura cha msingi cha kutazama na kupiga kura kwenye mapendekezo yaliyotolewa na IOG kinahitaji usajili kuingia. Zaidi ya hayo, ni vigumu kuona mapendekezo ya awali isipokuwa zilifadhiliwa. Tunafikiri ni muhimu kwamba kama jamii, tunapaswa kuwa na uwezo wa kuona vipande vyote vya fumbo, ili tuwe wananchi walio na taarifa na wachangiaji. Chukua muda wa kuangalia mapendekezo ya awali, na uone ikiwa kuna kitu ambacho kinakuvutia!

Siku zijazo za project catalyst

Project catalyst ni kama mradi wa Utafutaji Umati - kinachoenda kwa kasi! Lengo la kila raundi ni kwamba vipande vingi vya fumbo hupendekezwa, kuamuliwa, na kuendeshwa na jamii yenyewe. Kwa mfano, katika raundi za awali, “Changamoto” ziliekwa na timu katika IOHK.Katika raundi zote zinazofuata, jamii imeombwa kupendekeza na kupigia kura maswali ya Changamoto kwa raundi inayofuata.Katika mzunguko wa sasa, hazina maalum ya 6, nusu yachangamota za kampeni zilitoka kwa jamii. Hatimaye, changamoto zote zitaamuliwa kikamilifu na kuwekwa na jamii, pamoja na vipengele vingine vya kufanya maamuzi na utawala. Wakati fulani, tunatarajia kwamba project catalyst kama tunavyojua kitafikia kikomo. Kisha, mambo ambayo tumejifunza yatafungua njia ya kuanzishwa kwa DAO itakayofanya kazi kikamilifu. Kwa wakati ujao, jukumu la IOG litabadilika; umiliki na usimamizi wa mtandao utakuwa mikononi mwa wamiliki wa tokeni za ADA, kama wewe! Kutoka kwa Ramani ya njia ya Cardano: “Wakati tunajenga Cardano, sisi ni walezi tu. Mtandao utakapogatuliwa kikamilifu utakuwa wa jamii, na itakuwa jamii itakayoamua mustakabali wake kupitia vipengele vya juu vya utawala.”

Jinsi unavyoweza kushiriki

Ikiwa una angalau ADA 500, unaweza na unapaswa kupiga kura. Kuamua juu ya mustakabali wa Cardano sio tu kwa wanateknologia na wa wakilishi. Cardano ni zana yetu sote, na inahitaji sisi sote ili kufikia uwezo wake kamili. Usajili wa Hazina maalum ya 6 umefunguliwa sasa, hadi mnamo Septemba mwaka wa 2021, na upigaji kura kwa hazina maalum ya 6 utaanza tarehe 7 Oktoba. Ikiwa utasoma hii katika siku zijazo, ingia tu! Maagizo ya usajili yanaweza kupatikana hapa.

Mara tu unaposhiriki katika upigaji kura, utakuwa na wazo bora ya aina nyingi za maoni tofauti na mapendekezo. Labda hata utakuwa na mawazo ya ubunifu ya kile unachoweza kuchangia, na utahamasishwa kutoa pendekezo katika raundi inayofuata…

Lido Nation imejumuishwa!

Timu ya Lido Nation iliamua kushiriki katika hazina maalum ya 6, na iliwasilisha mapendekezo 3. Huku kukiwa na mapendekezo mengine zaidi ya 800 katika kinyang’anyiro cha kupata nafasi 100 za ushindi, ushindani utakuwa mkali! Lakini tumefurahia mchakato wa kuunda mawazo yetu katika mapendekezo na kuyaweka katika kinyang’anyiro

Baada ya kusajiliwa kupiga kura, angalia mapendekezo yetu juu ya Ideascale, utupe maoni na “pongezi”, na uwe tayari kutupigia kura mnamo Oktoba!

Treasury and Catalyst Directory: Hii ndio zana ya Lido Nation ilichotajwa hapo awali katika makala haya. Pendekezo letu litaturuhusu kuijenga kuwa rasilimali bora zaidi kwa jamii nzima ya Cardano. Spanish News, Insight, and Onboarding: Kihispania ni mojawapo ya lugha kuu za asili duniani. Ufadhili huu utaturuhusu kufanya maktaba yetu ya rasilimali zinazoeleweka kwa urahisi kupatikana kwa Kihispania. Swahili News, Insight and Onboarding: jamii ya Cardano ina nia ya kutatua matatizo barani Afrika. Kwa hivyo tumeungana na kikundi cha vijana wa teknolojia nchini Kenya kutafsiri maudhui yetu kwa Kiswahili.

Mwezi huu, tutapokea maoni kutoka kwa wanajamii na washauri wa pendekezo. Baada ya hapo, tunatarajia matokeo ya upigaji kura mnamo Oktoba. Ikiwa mapendekezo yetu yoyote yatafadhiliwa, itakuwa yenye kuhimiza sana, na itashawishi kile tunachozingatia katika siku za usoni. Bila kujali matokeo, tunabakia tukikuzingatia kutoa habari na rasilimali kwa wanachana wapya wa Cardano.

Related Links

  • Fund your Project with Catalyst developers.cardano.org
  • Relevant Link 1 link
  • Register to learn about Proposals and submit a business idea ideascale
  • Go deeper with Catalyst Discord discord
  • IOG Launch Announcement blog
  • Project Catalyst Challenge and Proposal Guide How to write Challenge and Proposal Guide
  • Places to connect people and ideas Catalyst Swarm Events Calendar
  • Fund8 Launch Guide pdf
  • Project Catalyst – the first winning proposals iog blog
  • Cardano Treasury with Kevin Hammond gitbook
  • Announcements only telegram
  • Weekly Townhall zoom

Get more articles like this in your inbox

Umejifunza nini hapa, na Je unaswali lolote?

Or leave comment
Share
pablo balondani avatar

ce vraiment tres bien

avatar
You can use Markdown
avatar
You can use Markdown
close

Playlist

  • EP2: epoch_length

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 3 se. 24
    Darlington Kofa
  • EP1: 'd' parameter

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 4 se. 3
    Darlington Kofa
  • EP3: key_deposit

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 3 se. 48
    Darlington Kofa
  • EP4: epoch_no

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 2 se. 16
    Darlington Kofa
  • EP5: max_block_size

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 3 se. 14
    Darlington Kofa
  • EP6: pool_deposit

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 3 se. 19
    Darlington Kofa
  • EP7: max_tx_size

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 4 se. 59
    Darlington Kofa
0:00
/
~0:00