DAOs kwa urahisi: Shirika linalojali watu

Decentralized Autonomous Organization (DAO) ni njia inayoibuka ya kupanga kazi inayobadilisha muundo wa kawaida wa nguvu ya mamlaka ya uongozi. Kwa njia hii mpya ya kupanga, mpangilio wa washiriki ni mdogo kama piramidi, na zaidi kama meza ya pande zote. Njia hii ya kupanga hueka kazi iwe ya kibinafsi. DAOs husogeza maamuzi muhimu karibu na wachangiaji binafsi, ikimpa kila mtu mamlaka zaidi, wakala, na hisa katika matokeo ya kazi.

Historia ya kazi

Uhitaji wa kupanga daima imekuwa sehemu ya maisha na mageuzi ya binadamu. Katika siku za mwanzo za mageuzi ya mwanadamu, wanadamu walipanga kukusanya chakula, kutengeneza nguo na kujenga makaazi. Tuliunda zana, tukapata njia za kushiriki maarifa, na tukawa wastadi sana katika kazi inayohitajika ili kuishi. Hii ilimaanisha kuwa tulitumia muda mchache kufanya kazi kwa ajili ya kujikimu tu, na tukapata masaa machache wakati wa mchana kutafakari aina mpya za kazi.

Utamaduni wa kisasa wa kazi

Katika Misri ya kale tulijifunza kwamba mpangilio ulikuwa zana yenye nguvu ya kukuza kazi; Cha kushangaza, ilikuwa wakati wa kujenga piramidi ambapo wanadamu walijaribu kwa mara ya kwanza miundo ya shirika ya zaidi ya viwango viwili. Wamisri pia walianzisha wazo la utawala ambalo halina msingi wa ukoo wa familia. Katika miaka 4,000 tangu Misri ya kale, mpangilio wa kazi nyingi umeundwa kama piramidi: mtu mmoja au kikundi kidogo kinachukua ncha, na hawa wachache huamua kile kinachotokea katika tabaka zote chini yao. Kadiri piramidi inavyokuwa kubwa, mtazamo zaidi unawekwa kwenye kazi, na kupunguzwa kwa watu. Kuna kuongezeka kwa makubaliano kwamba hii ni mbaya kwetu. Vichwa vya habari vinaanzia na: “Profesa Stanford anaonya watu kuhusiana na mahali petu pa kazi ya kisasa penye madhara (healthline.com),” hadi “mahali pa kazi panaua watu na hakuna anayejali (Stanford Business).”

Jaribio la Uswizi.

Taifa la Uswizi ni maarufu kwa chokoleti zake, benki zake, saa zake za bei ghali na milima ya alps. Lakini je, unajua kwamba pia ni nyumbani kwa jaribio kubwa na refu zaidi la shirika mbadala la kazi ya kiraia? Huko Uswizi hakuna mfalme au rais - hakuna mtu mmoja ambaye anaweza kuathiri maisha ya nchi nzima. Tawi lao la utendaji linaongozwa na watu saba wenye dhamani sawa. Shirika hili (Baraza la Shirikisho) lina uwezo wa kusimamia forodha, sera za kigeni, mfumo wa fedha, jeshi, programu za kijamii, na sheria. Zaidi ya mambo haya, usawa wa kazi ya kiraia upo mikononi mwa kitengo chao kidogo zaidi cha uongozi kiitwacho jumuiya (communes). Jumiya (Communes) ni kama mji au jiji, lakini yenye uhuru zaidi kuliko ya kawaida. Mambo ya kuvutia kuhusu muundo wa kiraia wa Uswizi ni kama vile:

  • Raia yeyote anaweza kuanzisha sheria mpya, ikiwa anaweza kukusanya saini 100,000.
  • Uraia hautolewi na serikali kuu, bali na jumuiya (communes) zilizogatuliwa.
  • Ikiwa serikali ya shirikisho au ya eneo itapitisha sheria, raia yeyote anaweza kupendekeza suala kwa saini 50,000 pekee.
  • Mabadiliko yoyote ya katiba ya Uswizi yanahitaji idhini ya raia wake. Uswizi imepanga kazi ya kutawala kwa njia ambayo watu binafsi wana uzingatia zaidi kuliko katika miundo mingine ya kisasa ya serikali.

Makampuni yenye wakurugenzi watendaji wengi

Katika ulimwengu wa ushirika, kumekuwa na majaribio mengi ya hivi karibuni na wazo la kuwa na wasimamizi wengi. Majina makubwa kama vile Netflix, Samsung, Deutsche Bank, na Chipotle wamegundua wazo la kuwa na Wakurugenzi watendaji wengi. Wazo la jumla ni kwamba kushirikiana kwa kazi ya kupanga na kufanya maamuzi ni bora, na husababisha uchovu kidogo.

Dao kwa kina

Decentralized Autonomous Organization ni mtindo mpya unaoleta kufanya maamuzi na utawala karibu zaidi na mtu binafsi. Huweka kundi nzima la watu binafsi katikati ya kupanga na kusimamia kazi. Wazo la DAO ni kwamba hakuna kiongozi mmoja anayepaswa kuendesha ajenda ya kampuni nzima, au nchi. Badala yake, mtu yeyote anaweza kuweka kipengele cha ajenda na kushirikiana kusimamia kazi inayotokea. Kwa njia hii “upangaji” na usimamizi ni “Umegatuliwa.” Mara tu kazi inapobainishwa na kuidhinishwa, DAO huwezesha utekelezaji wa “Otomatiki” wa kazi ambazo zingefanywa hapo awali na meneja, mkurugenzi au kamati ya uangalizi.

Tayari umeingiliana na matukio madogo ya Mashirika ya Kiotomatiki ikiwa unaishi mahali popote penye ufikiaji wa mtandao na ununuzi wa mtandaoni. Kwa mfano, unapoweka agizo kwenye Amazon, hakuna mwanadamu anayehitaji kuthibitisha agizo lako. Kompyuta hukagua kiotomatiki kuwa malipo yako yamefaulu, na kubaini ni ghala gani la Amazon lililo karibu nawe ambalo agizo lako linapatikana. Kisha kompyuta hutuma agizo kwenye ghala na habari zote zinazohitajika ili kuifikisha kwenye mlango wako. Mamlaka moja kuu (Amazon) bado huweka sheria kuhusu jinsi kila hatua ya otomatiki inavyofanya kazi, lakini mfano huu unaonyesha kuwa maamuzi changamano, yanayotokana na matukio yanaweza kuwa otomatiki.

Zingatia jinsi DAO inavyoweza kutumiwa ili kusimamia bajeti ya elimu ya nchi kulingana na mahitaji ya kila shule, ikiendelezwa na taarifa zinazoweza kuthibitishwa na kuwekwa kwenye kompyuta kwa urahisi. Taarifa zinazoweza kuthibitishwa zinaweza kujumuisha utabiri wa hali ya hewa na gharama ya umeme, idadi ya wanafunzi katika eneo fulani, na umbali ambao mabasi ya shule hulazimika kusafiri kuwachukua wanafunzi. Kwa kuwa utekelezaji unaosimamiwa na DAO ni wa kiotomatiki na wa haraka, bajeti kama hiyo inaweza kulipwa kila mwezi au kila wiki bila ucheleweshaji wa kibinadamu kama vile likizo, wakati wa ugonjwa au kubadilishwa kwa wafanyikazi.Shule inaweza kupokea pesa zaidi wiki moja kwa ajili ya kiyoyozi kutokana na rekodi ya halijoto ya juu, na wiki ijayo kupokea kiasi chao cha kawaida. Katika mfano wa jamii hii, mwananchi yeyote anaweza kupendekeza mabadiliko ya jinsi kiwango cha pesa kinavyohesabiwa, na wanachama wote walioidhinishwa wa jiji hilo wanaweza kupiga kura juu ya mabadiliko hayo bila kuhitaji meya au baraza la jiji. Huu ndio uwezo wa Decentralized Autonomous Organization. Mabadiliko yanaweza kutoka popote! Kadhalika, upinzani dhidi ya mabadiliko yanaweza pia kutokea popote. Blockchain ni salama na ya kudumu, kila kitu ni wazi na kinaweza kukaguliwa. Kwa hiyo, mara maamuzi yanapofanywa, hakuna anayeweza Kuyabadilisha.

DAO’s katika Cardano.

Decentralized Autonomous Organization ni wazo changa ambalo linawezeshwa na teknolojia ya blockchain. Bitcoin ilikuwa jaribio la mafanikio ambalo lilithibitisha kwamba pesa, ambayo hapo awali ilikuwa inaonekana, inaweza kufanywa ya kidijitali kabisa. DAOs zitatuwezesha kufanya vitu vingine vingi kuwa vya kidijitali pia. Teknolojia kadhaa za blockchain zinafanya majaribio na DAOs; Cardano inaongoza kikundi hiki kwa kufanya usanidi na usimamizi wa DAO kuwa rahisi sana. Cardano kwa sasa ndiyo jukwaa pekee la umma la blockchain lenye DIDs (Decentralized Identifiers) ambalo linaweza kutumika kuunda mifumo ya vitambulisho vya kitaifa na zana za upigaji kura zilizojumuishwa moja kwa moja kwenye itifaki yake.

LIDO Nation inaidhinisha DAOs.

Hebu fikiria kuwa na chaguo kati yenye shirika la kitamaduni na ya DAO. Je, unaweza kuamini Shirika kuwa na tabia ya haki na yenye manufaa yako, bila kujali ni nani aliye kwenye bodi ya wakurugenzi? Badala yake, fikiria kuwa na ufikiaji wa moja kwa moja wa habari kuhusu shughuli za biashara na fedha, na kuwa na kura katika maamuzi kuhusu jinsi mafanikio ya Kampuni yanavyogawanywa. Bado tuna safari ndefu kabla ya kuanza kuona mashirika na serikali yakibadilisha baadhi ya shughuli au urasimu kwa kutumia DAOs. Sisi katika Lido Nation tunafurahia kushiriki katika majaribio haya ya awali, na tunachochewa na matarajio ya ulimwengu ambapo kila mtu atapata sauti na kura sawa, kwa kuzaliwa tu.

Related Links

  • Open source tools to support DAO infrastructures ADAO Website
  • Deep Dive into a Cardano DAO medium article

Get more articles like this in your inbox

Je, kuna jambo jipya umejifunza kuhusu DAOs?

Or leave comment
Share

No comments yet…

avatar
You can use Markdown
close

Playlist

  • EP2: epoch_length

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 3 se. 24
    Darlington Kofa
  • EP1: 'd' parameter

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 4 se. 3
    Darlington Kofa
  • EP3: key_deposit

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 3 se. 48
    Darlington Kofa
  • EP4: epoch_no

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 2 se. 16
    Darlington Kofa
  • EP5: max_block_size

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 3 se. 14
    Darlington Kofa
  • EP6: pool_deposit

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 3 se. 19
    Darlington Kofa
  • EP7: max_tx_size

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 4 se. 59
    Darlington Kofa
0:00
/
~0:00