DirectEd+ Cardano: kujenga mustakabali mzuri na mikataba bora

Katika hazina maalum ya 6 ya Project Catalyst, Lido Nation ilifadhiliwa kufanya kazi na kikundi cha wazungumzaji asilia wa Kiswahili nchini Kenya. Tuliwasaidia kujifunza kuhusu Cardano, kutafsiri makala za Lido Nation katika Kiswahili, na hatimaye kuandika maudhui yao halisi kuhusu Cardano kwa hadhira inayozungumza Kiswahili. Makala haya ni sehemu ya mfululizo wa maudhui ya Kiswahili!

Elimu ni jambo muhimu katika maendeleo ya uchumi wa nchi, lakini licha ya umuhimu wake, kwa ujumla haifadhiliwi wala kupewa kipaumbele. DirectEd ni kikundi kinachotaka kutumia teknolojia ya blockchain kusaidia wasomi katika nchi zinazoendelea. DirectEd huwezesha michango kwa ajili ya Elimu inayoendeshwa na Blockchain ya Cardano, kwa kuchanganya shughuli za blockchain, mikataba bora, vitambulishi vilivyogatuliwa (Decentralized Identifiers, DIDs) na stakabadhi zinazoweza kuthibitishwa. Njia hizi huwezesha njia ya uwazi, salama na ya gharama nafuu ya kutuma michango ya masharti kwa wanafunzi kote ulimwenguni. Kwa kuchakata michango moja kwa moja kupitia mtandao wa Cardano, na kuzisambaza kwa watu binafsi waliothibitishwa na DID, vikwazo kama vile kutoaminiana, ulaghai na gharama za usimamizi hupunguzwa kwa kiasi kikubwa. Matumaini ni kwamba wafadhili watapendelea zaidi kushiriki katika kuunga mkono wasomi wachanga wanapokuwa na muonekano wazi, wa mwisho hadi mwisho wa jinsi pesa zao zinavyotumika, na faida inayoleta.

Ili kuanzisha mradi wao, DirectEd iligeukia Project Catalyst ya Cardano kwa ufadhili. DirectEd imekuwa na mapendekezo matatu yaliyofadhiliwa hadi sasa.

Direct Donation for Education

$9,280 Received
$9,280 Requested

<p>Current donation services lack efficiency, transparency and security. ADA microlending may be difficult due to legal barriers and trust.</p>

Fund: Fund 6 Challenge: F6: DeFi and Microlending for Africa
completed Awarded 10.311% of the fund.
4.96 (24)

DirectEd - Donations dApp

$59,040 Received
$59,040 Requested

Solution: Scholarship/donation platform based on Atala PRISM enabling secure, low-cost, conditional peer-to-peer donations to students.

Fund: Fund 8 Challenge: F8: DApps and Integrations
completed Awarded 2.362% of the fund.
4.77 (30)

DirectEd-Student Scholarship Portal

$30,300 Received
$30,300 Requested

Solution: Scholarship/donation platform based on Atala PRISM enabling secure, low-cost, conditional peer-to-peer donations to students.

Fund: Fund 8 Challenge: Self-Sovereign Identity
completed Awarded 7.575% of the fund.
4.88 (24)

Mtazamo wao ni katika mikoa ambayo wanafunzi hawawezi kusoma kwa sababu ya ukosefu wa nyenzo zinazohitajika. Maono yao ni, “kujenga ulimwengu ambao mtu yeyote bila kujali mchoro wao katika bahati nasibu ya maisha, anaweza kutambua uwezo wake kamili.” DirectEd hubainisha shule za upili katika maeneo yenye mapato ya chini na wafadhili ambao wanaweza kutoa mchango. Nchini Ethiopia, shule hizi zimewekwa kwenye mfumo wa Cardano wa Atala PRISM “kitambulisho kilichogatuliwa” yaani (DID) ambao unachanganya suluhu za utambulisho, thamani na utawala katika jukwaa moja. Nchini Kenya, wao husaidia shule kuwa watoaji wa stakabadhi zinazoweza kuthibitishwa na kuwasaidia wanafunzi kuwa na Vitambulisho Vilivyogatuliwa (DIDs). Wanaunganisha vitambulisho hivyo vilivyogatuliwa na pochi za Cardano, wakiwatayarisha wanafunzi kupokea ufadhili wa masomo. DirectEd hubainisha mkataba bora kwa kila shule ya upili. Mikataba hizo hufanya mambo manne:

  • Kubainisha kiwango cha ustahiki wa ufadhili wa masomo
  • Kuchagua washindi wa ufadhili kiunasibu ikiwa idadi ya wanafunzi wanaostahiki inazidi pesa zinazopatikana
  • Kubainisha saizi ya jumla ya kila udhamini
  • Kubainisha mahitaji ya maendeleo yanayohitajika ili kutolewa kwa sehemu inayofuata ya udhamini.

Wafadhili huahidi kutoa kiasi fulani cha ufadhili kwa mojawapo ya mikataba bora, kila moja yao ikiwakilisha shule ya upili. Wafadhili hupokea NFT ambayo imetungwa na DirectEd, ambayo inaweza kutumika kuthibitisha kuwa wametoa mchango na kufungua ufikiaji wa ukurasa wa kufuatilia maendeleo kwa kundi mahususi walilolichangia. Shule za upili hutoa vitambulisho, vilivyo na alama, kwa Vitambulisho Vilivyogatuliwa vya wanafunzi. Kisha mwanafunzi anaweza kutuma ombi la mchango kwa kushiriki kitambulisho hiki kinachoweza kuthibitishwa na mkataba bora. Mara tu wakati wa kuwasilisha maombi ya ufadhili wa masomo ikiisha, kubahatisha miongoni mwa wanafunzi wanaostahiki hutumika kuamua washindi wa ufadhili wa masomo ikiwa idadi ya wanafunzi wanaostahiki itazidi pesa zinazopatikana. Wanafunzi hujiandikisha katika vyuo vikuu na msajili hutoa kitambulisho kwa DID ya mwanafunzi. Wanafunzi hushiriki uthibitisho wao wa kusajiliwa kwa mkataba bora, ambayo huanzisha uchochezi wa malipo ya kwanza ya ufadhili wa masomo. Malipo zaidi vile vile inategemea ushahidi wa mafanikio yaliyopatikana kama inavyothibitishwa na stakabadhi zinazoweza kuthibitishwa zinazotolewa na chuo kikuu au mtoa huduma mwingine wa elimu. Wanafunzi wa ufadhili wa masomo wakishindwa kukidhi baadhi ya masharti ndani ya muda uliobainishwa awali ulioandikwa katika mkataba bora, pesa zozote zinazosalia zitarejeshwa kwa anwani za wafadhili.

DirectEd imeshirikiana na taasisi za elimu kupitia mijadala isiyo rasmi nchini Kenya na Ethiopia. Nchini Kenya, wameshirikiana na Shule ya Upili ya Kagumo na Chuo Kikuu cha Kenyatta ambazo zote ziko Nairobi. Nchini Ethiopia, wameshirikiana na Chuo Kikuu cha Elimu cha Kotebe, Addis Ababa na Chuo Kikuu cha Elimu cha Kotebe Menelik. Pia wameshirikiana na wasambazaji wa teknolojia kama vile Kotani pay ambayo hutoa njia panda ya crypto kwenye simu ya mkononi barani Afrika, Gero wallet ambayo ni pochi ya crypto na Proofspace ambayo hutoa suluhu za utoaji wa stakabadhi zinazoweza kuthibitishwa.

DirectEd inafaidi maisha ya wanafunzi na tunatumai kuona miradi zaidi kama hizi zikipendekezwa. Ili kujifunza mengi kuhusu DirectEd na jinsi unavyoweza kusaidia mradi wao, tembelea tovuti yao kwenye https://directed.dev/.

Get more articles like this in your inbox

Was the article useful?

Or leave comment
Share
Commenter avatar

Great and informative piece. Good projects on the cardano network!

avatar
You can use Markdown
avatar
You can use Markdown
close

Playlist

  • EP2: epoch_length

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 3 se. 24
    Darlington Kofa
  • EP1: 'd' parameter

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 4 se. 3
    Darlington Kofa
  • EP3: key_deposit

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 3 se. 48
    Darlington Kofa
  • EP4: epoch_no

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 2 se. 16
    Darlington Kofa
  • EP5: max_block_size

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 3 se. 14
    Darlington Kofa
  • EP6: pool_deposit

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 3 se. 19
    Darlington Kofa
  • EP7: max_tx_size

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 4 se. 59
    Darlington Kofa
0:00
/
~0:00