Utawala wa Ugatuaji wa siku zijazo

Je, ni karibu kiasi gani - na ni umbali kiasi gani?

“Utawala Uliogatuliwa” na “uwezo wa shirika kukagua tabia zake yenyewe” ni njia mbili za kuweka ahadi moja inayotajwa mara nyingi ya siku zijazo za blockchain. Katika ulimwengu wa leo, nguvu ya kati na nguvu ikiwa mikononi mwa watu wachache ni hali halisi ya ulimwengu ambayo husababisha shida, kubwa na ndogo. Wengine wanaofikiria uwezekano tofauti wanaona blockchain kama zana ambayo inaweza kuwezesha siku zijazo. Leo tutazingatia tukio la hivi majuzi katika Jamii ya Cardano, uchaguzi wa Mzunguko wa catalyst katika raundi ya nne. Uchaguzi huu uliashiria hatua ndogo na pia ilionyesha kuwa tuna safari ndefu sana.

Catalyst Circle (Mzunguko wa catalyst) inafafanuliwa kama “safu ya kihisia ya kibinadamu” kwa ajili ya jaribio la project catalyst. Mzunguko huo una jukumu la kukutana mara kwa mara ili kujadili kinachoendelea katika project catalyst. Hasa, malengo yao ya msingi ni:

  • Kurahisisha mawasiliano kati ya vikundi tofauti vya utendaji
  • Kutoa tahadhari wakati kikundi moja ou nyingine kimevuka mpaka
  • Kupendekeza mipango ya uboreshaji na michakato inayounda project catalyst (pamoja na mzunguko yenyewe!)

Upigaji kura kwa raundi ya nne ya Mzunguko wa catalyst (CCv4) ulifanyika mnamo Desemba 2022. Kikundi hiki kidogo kilianzishwa kwa mara ya kwanza mnamo Julai 2021; washiriki wa Mzunguko huu hupigiwa kura na jamii na huhudumu kwa muda wa miezi kadhaa (urefu wa muhula umetofautiana). CCv4 iliweka mahala pa egemeo kwa Mzunguko, katika muundo wake na jinsi upigaji kura ulivyofanyika. Mzunguko ya Awali iliundwa na wawakilishi kutoka kwa vikundi vya washikadau katika mfumoya ikolojia ya catalyst - Wapendekezaji, Watathmini wa Mapendekezo, Watengenezaji zana, Waendeshaji wa nodi, Wamiliki wa Ada, Wakfu wa Cardano, na IOG. Uchaguaji ya wawakilishi wa Cardano Foundation na IOG yalifanyika ndani ya mashirika hayo. Kwa majukumu ya umma, “kura ya umma” ilifanyika kwa njia isiyo ya kawaida: Waliohudhuria kwenye Zoom walipiga kura kwa wawakilishi wao wanaopendelea kwa kuinua mikono yao, katika mkutano ya Zoom, ili kupiga kura. Ikiwa umewahi kujiuliza ingekuwaje kuwa katika chumba na waanzilishi wa taifa jipya, wakizozana na kupiga kelele na kupiga kelele “ndio!” na “hapana!” na kumsukuma kiongozi wao awaliomchagua hadi kwenye jukwaa, huenda ulifikiri siku hizo zilikuwa zimepita. Sivyo!

Tukizingatia hatua ya tatu hapo juu, inaonekana kwamba raundi ya awali ya Mzunguko yamefanya kazi yao hadi kupendekeza uboreshaji wa uundaji wao wenyewe unaoendelea. Kwa CCv4, mabadiliko mawili yanaonekana:

  1. Badala ya kujumuisha “wawakilishi” saba wa vikundi vya washikadau, Mzunguko una washiriki watano tu wanaogombea wadhifa kwenye jukwaa na wanaelezea nia yao ya uongozi.
  2. Upigaji kura hufanyika kwa njia ya mtandao, kwa kutumia nguvu ya kupiga kura ya ada katika pochi zilizounganishwa.

Pembe nyingi za jamii zilijitokeza ili kuwezesha mabadiliko haya:

  • Wagombea wa Mzunguko walichaguliwa kupitia mikutano ya town hall na mawasiliano ya kimsingi kati ya watu.
  • Taarifa za Mfumo kutoka kwa wagombea zilikusanywa na kuchapishwa kwenye Jukwaa la Cardano.
  • DripDropz ilitengeneza jukwaa la upigaji kura kwa njia ya mtandao, ilichapisha blogu na video ya jinsi ya kuwasaidia wapiga kura, na waloijitokeza kwenye mkutano wa Town Hall kuelezea mchakato huo.
  • Lido Nation ilitengeneza dashibodi ya kuripoti ili kuonyesha uchanganuzi mbalimbali wa kura wakati upigaji kura ulipokuwa unaendelea - na matokeo ya mwisho. + @HoskyToken na @QuasarSure walichangia tokeni Bilioni 100 za $HOSKY na $DISCO mtawalia kama motisha kwa wapigakura, ili zigawiwe kwa wapigakura wanaojiandikisha kwa usambazaji wa tuzo kwenye Lido Nation.
  • Jamii kwa ujumla ilishiriki mawazo yao kwenye mitandao ya kijamii, na timu ya DripDropz ilikuwa msikivu sana na kutoa maoni ya moja kwa moja!

Kama mtazamaji wa kando, ilikuwa ya kufurahisha kuona ushirikiano huu uliogawanyika ukija pamoja moja kwa moja katika hafla ya Rare Bloom mnamo Oktoba 2022. Tarehe ya mwisho ya uteuzi ilikuwa karibu; kati ya mikutano na matukio, @stoicpool walikuwa wakikimbia na kamera ya video yenye maikrofoni, akirekodi taarifa za jukwaa la wagombea. Kulikua na msisimko, na wagombea kadhaa wazuri walivutwa kwenye kinyang’anyiro hicho katika dakika ya mwisho.

Upigaji kura wa mtandaoni ulifanyika katika dripdropz.io mapema Desemba. Niliangalia matokeo ya moja kwa moja mara kadhaa wakati wa kupiga kura, na uilikuwa ushindani mkali! Wagombea maarufu walionekana mapema katika kinyang’anyiro hicho, lakini matokeo ya mwisho hayakuwa wazi hadi mwisho. Mwishowe, wagombea watano wenye sifa nzuri walichaguliwa, na tunatazamia kuona kitakachofuata kutoka kwa uongozi wao! Kwa ajili ya makala haya, tutaweka mawazo yetu kwenye mchakato wa utawala wenyewe.

Kwanza, hebu tuzingatie ushiriki wa jumla. Ingawa uwezo wa kupiga kura katika uchaguzi huu uliegemezwa kwenye ada, na si wapiga kura binafsi, tunaweza kuwa karibu iwezekanavyo kukadiria kiasi cha ushiriki kwa kuangalia anwani za kipekee za wadau wanaoshiriki. Jumla ya anwani 1140 za kipekee za hisa zilishiriki katika uchaguzi huo. Hii inalinganishwa vyema na uchaguzi uliopita wa “Zoom”, ambapo kila nafasi kilichoweza kuchaguliwa kilishirikisha wapiga kura wachache tu!

https://storage.googleapis.com/www.lidonation.com/9007/1StakeKey1Vote.png

*Chati hii inawakilisha Wapiga Kura 1140 kwa ukubwa wa pochi. Theluthi mbili ya wapiga kura - wigo mzima wa zambarau - wanashikilia ada isiyozidi 10K kwenye pochi zao.

Kisha, hebu tuzingatie matokeo za umiliki wa ada kwenye kura. Kumbuka, muundo wa uchaguzi huu haukuwa “ufunguo 1 wa hisa” = “Kura moja” - hii haitakuwa na maana hata hivyo kwa kuwa ufunguo wa hisa si sawa na utambulisho wa kipekee. Inapotazamwa, tofauti ni ya kushangaza. Hapa tunaona kwamba wapiga kura walio na ada chini ya 10K kwenye pochi zao, ingawa walikuwa na 70% ya pochi za kupigia kura, walikuwa na chini ya 2% ya nguvu ya kupiga kura.

https://storage.googleapis.com/www.lidonation.com/9008/AdaPowerRanges.png

*KUMBUKA kuwa mpangilio wa rangi kati ya chati hizi mbili NI SAWA - wigo wa zambarau unaotawala chati ya kwanza karibu hauonekani kwenye chati hii kwa sababu uwezo wao wa kifedha wa kupiga kura ni mdogo sana.

Matokeo kuu ni kwamba 40% ya “nguvu” ya kupiga kura iko kwenye mikono ya pochi 10 zenye ada zaidi ya 1M. Tukipunguza hadi ada 500K, tunaweza kuhesabu 60% ya nguvu ya kupiga kura na kuongezea pochi 13 zaidi za kupigia kura pekee. Pamoja na kuenea kwa wapiga kura 7 wakuu wanaofikia ada M 10 pekee, inawezekana kabisa kwamba pochi moja ya ada 10M ya kupiga kura ingeweza kuamua uchaguzi mzima. Kwa hivyo swali ni: je, hatimaye tulifanya vyema zaidi kuliko chaguzi ya zoom, ambapo ni dazeni chache tu waliweza kushiriki?

Ingawa matokeo haya yanashangaza, lengo letu la kuripoti si kuleta mshtuko. Badala yake, tuko hapa kuangalia kwa uwazi ukweli tunaoweza kupata ili tuweze kujenga mbele pamoja. Juu ya orodha yangu ya mazingatio yanayofuata ni kufikiria jinsi hii, inatumika kwa project catalyst. Ikilinganishwa na jumla ya ada 66.8M ambazo zilishiriki katika uchaguzi wa CCv4, zaidi ya ada 3.6B walijiandikisha kupiga kura katika awamu ya hivi majuzi ya project catalyst (hazina maalum ya 9; takwimu za usajili wa wapigakura kulingana na maelezo yaliyoshirikiwa kwa maneno kutoka IOG). Je, nyangumi mmoja au wawili bado wana nguvu nyingi sana wakati wa kuogelea kwenye bwawa kubwa zaidi? Jibu ni - ndio, labda. Mapendekezo mengi, ikiwa ni pamoja na yale yaliyoshinda, yanahesabu kura 200 tu zisizo za kawaida zilizopigwa kwa kila pendekezo - sio tofauti kabisa na idadi ya washiriki katika kura ya Mzunguko na, kwa hivyo, kwa ushawishi ambao idadi ndogo ya pochi ya kupiga kura lazima itokee. Vilinganishi kamili (nguvu kamili ya upigaji kura ya pochi mahususi za upigaji kura, n.k. - mambo tuliyoweza kuona katika uchaguzi wa CCv4) hazipatikani hadharani kwa umma. Kura za project catalyst hurekodiwa kwenye blockchain ya kibinafsi kwenye IOG. Hiyo inafanya uchunguzi huu wa data ya moja kwa moja ya kura ya blockchain kuwa muhimu zaidi!

Suala la ni wapi pa kuenda baadae haijapuuzwa. Mabadiliko ya kwanza ambayo tunaweza kuona yatakuwa uzinduzi wa “dReps,” ambayo bado imepangwa kwa Hazina maalum ya 10 mapema 2023. Wazo la dReps ni kwamba badala ya kila mpiga kura kujaribu kuleta maana ya mapendekezo 1000+ na kuchukua muda mrefu badala yake, wapiga kura wangeweza kukasimu mamlaka yao ya kupiga kura kwa “dReps” moja au zaidi. dReps watakuwa na jukumu la kupiga kura wakiwa na uwezo wote wa kupiga kura waliokabidhiwa. Hili litaruhusu kujumlishwa kwa nguvu za pochi nyingi ndogo, ambazo zingetumika kutumia “nguvu” ya jumla ya upigaji kura kuliko ikiwa watu hao wote wangepiga kura nyingi walivyotaka. Ingawa siwezi kujizuia kuteta kidogo ninapofikiria kuhusu siasa za mfumo huu bila shaka zitazuka, bado nina shauku ya kushuhudia tofauti nyingine katika jaribio na kuona tutajifunza nini kutoka kwayo.

Kuelekea Mkutano wa Cardano 2022, timu ya Zana za Metadata katika Wakfu wa Cardano ilipewa jukumu la kuunda programu ya kusaidia upigaji kura kwa ajili ya “uchaguzi wa Spika” ambao ulichochea siku ya pili ya mawasilisho ya spika kwenye Mkutano huo. Zana waliyounda ilikuwa muhimu kwa ajili ya kufurahisha, uchaguzi wa viwango vya chini. Ilifaulu kupunguza uwezo wa kupiga kura kuwa 1-wallet=kura-1; kiwango cha ada haikua kipengele haikuwa sababu. Hata hivyo, mtu yeyote ambaye alijali angeweza kupiga kura kwa pochi zake nyingi, wakati wale walio na pochi ya Ledger pekee hawakuweza kushiriki kabisa. Hata hivyo, matatizo mbalimbali yalifikiriwa na kutatuliwa katika mradi huu. Matokeo ni ya chanzo-wazi, na kutoa hatua kwa wajenzi wanaofuata kutumia na kuboresha.

Lengo, wengi wanapendekeza, ni suluhisho la Utambulisho Uliogatuliwa (DID) ambalo huruhusu kwa kweli mtu 1=kura 1. Atala Prism, RootsID, na IAMX yote ni miradi ambayo inashughulikia Utambulisho Uliogatuliwa. Iwapo umesikia kuhusu DID lakini huna uhakika zitatumika kwa ajili gani, jibu ni “mambo mengi,” lakini acha ufafanuzi wa leo uwe mfano wako wa kwanza mzuri.

Unaweza kupata maelezo zaidi kuhusu matokeo ya uchaguzi wa CCv4

katika zana ya Catalyst Explorer ya Lido Nation, ambayo inajumuisha chati zilizotajwa hapa pamoja na uchanganuzi mwingine wa kuvutia. Acha maoni yako!

Related Links

  • Project Catalyst Town Hall Re: Circle Nominations Oct 5 2022 YouTube
  • The Cardano Ballot: developing a decentralized voting app Cardano Foundation Blog
  • DripDropz blog about the voting tool Blog
  • Cardano Forum: Candidate platform statements Forum
  • Project Catalyst Town Hall - More about Catalyst Circle Oct 12 2022 YouTube
  • Project Catalyst Town Hall Oct 12 Slides Slide Deck
  • Fund 9 Voting Results Google Sheets
  • Relevant Link 3 link
  • Atala Prism Website
  • Relevant Link 1 link

Get more articles like this in your inbox

Was the article useful?

Or leave comment
Share

No comments yet…

avatar
You can use Markdown
close

Playlist

  • EP2: epoch_length

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 3 se. 24
    Darlington Kofa
  • EP1: 'd' parameter

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 4 se. 3
    Darlington Kofa
  • EP3: key_deposit

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 3 se. 48
    Darlington Kofa
  • EP4: epoch_no

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 2 se. 16
    Darlington Kofa
  • EP5: max_block_size

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 3 se. 14
    Darlington Kofa
  • EP6: pool_deposit

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 3 se. 19
    Darlington Kofa
  • EP7: max_tx_size

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 4 se. 59
    Darlington Kofa
0:00
/
~0:00