Pendekezo la Lido Nation

Teknolojia ya Blockchain ni njia yenye nguvu ya kutumia na kupanua mtandao kama tunavyoijua, na itabadilisha ulimwengu wetu. Kama vile mtandao, mabadiliko hayo yataleta fursa nyingi mpya, lakini kwa wakati huu yanaonekana kuwa mapya na ya ajabu kwa watu wengi. Kupata habari nzuri kuhusu blockchain inaweza kuwa changamoto. Taarifa nyingi mtandaoni huwekwa kwenye vikao vya wasanidi programu au mijadala mikuu kati ya wataalam wa kifedha. Mbaya zaidi, ingawa inatabirika,Habari nyingi kuhusu blockchain kwenye mtandao ziko kwenye majadiliano kati ya watayarishaji programu za kompyuta, mabenki, na wawekezaji wakubwa. Mbaya zaidi, kuna utapeli mwingi na habari za kupotosha, zinazoahidi utajiri wa haraka kwa wageni “ Hata habari kuu kwa kawaida huacha kitu cha kutamanika, kwani habari zinazochipuka kwa kawaida hukosa muktadha na uhusiano na picha kuu.

Lido Nation ni tovuti ya watu wa kila siku na wageni kujifunza kuhusu sehemu moja ya ulimwengu wa blockchain - hasa mradi unaoitwa Cardano, na sarafu inayohusishwa nayo, ADA. Tunagawanya dhana kubwa katika vipande vinavyoweza kueleweka, na kutoa muktadha ili kuelewa ni kwa nini unapaswa kujali. Wanaotembelea tovuti wanaweza kuingiliana katika seheu za maoni, au kuwasilisha mapendekezo ya makala kuhusu mambo ambayo wangependa kujifunza. Kila Ijumaa saa sita mchana (Saa za Kati) tuko mtandaoni kwa majadiliano ya jukwaa wazi, Maswali na Majibu, au mawasilisho mafupi.

Kwa nini tunafanya hivyo? - au tunapataje pesa? Lido Nation pia ni “Staking Pool” - au nodi katika mtandao wa Cardano. Cardano huzalisha, huthibitisha, na hulinda shughuli mpya kwa kutumia mtandao uliosambazwa wa waendeshaji nodi. Wakati nodi ya Lido Nation inapofanyia Cardano kazi, tunapata tuzo za kifedha. Ni msukosuko ambao unaweza kuwa kazi ya wakati wote, na ni mradi ambao tunaamini sana.

Swali linalofwata ni, kwa nini tulichagua Cardano? Ilhali kuna maelfu ya miradi ya blockchain na sarafu ya kuchagua. Umeskia juu ya Bitcoin ethereum, na huenda unajua nyingi zaidi ya hayo. Hakika, kunayo “alt-coin” mpya karibu kila siku. jambo ambalo huenda hujui ni kwamba mengi ya haya sio mawazo mapya kabisa au asili. Alt coin nyingi ni nakala za itifaki za bitcoin au ethereum zilizo na lebo mpya kwenye ufungaji. Baadhi yao hufanya marekebisho hapa na pale, lakini sarafu nyingi ni muigo, huku kukiwa na matumaini ya kupata pesa za haraka. Sarafu zingine zina mawazo asili, lakini zimeundwa kwa kusudi finyu, kama vile aina maalum ya chombo cha kifedha, au jukwaa la NFT. Sarafu nyingi zinaingia kwenye soko na ICO, “Initial Coin Offering” inayoongeza fedha kwa ajili ya mradi huo. Kutoka hapo, mradi huo unaeza shika kasi au ufeli. Sarafu zingine zinaweza kuwa muhimu na za thamani kwa muda mrefu, lakini zingine hazitakuwa na sifa hizi, ikiwa zitakosa pesa za kukuza na kudumisha mtandao wao kabla ya kudhaminiwa sana. Zaidi ya hayo, zile zinazotegemea itifaki sawa na Bitcoin na Ethereum, zinategemea nguvu nzito za kompyuta na matumizi ya nishati kutekeleza kazi za mtandao, na kuzua maswali kuhusu uwezo wa kuboreshwa na uendelevu.

Cardano ni aina tofauti kabisa ya jitihada. Mpangilio wake ni wa asili, kulingana na utafiti wa kitaaluma uliopitiwa na marika. Iliundwa kwa matumizi ya muda mrefu, kuongeza viwango vya kimataifa, na maadili ya kibinadamu. Hebu tuzingatie kila moja ya haya:

Matumizi ya muda mrefu.

Tofauti na miradi ambayo hufika tamati wakati fedha kutoka kwa ICO zao zinaisha, Cardano iliundwa na hazina ya kujitegemea. Sehemu ndogo ya ada za mtandao inaelekezwa kwa hazina ambayo inafadhili maendeleo na matengenezo ya mtandao. Hii inalinda cardano kutoka kwa kupanda na kushuka kwa soko la dunia, na kuhakikisha uwezekano wa muda mrefu na nguvu.

Upanuzi wa kimataifa.

Cardano ina vipengele kadhaa vya kubuni ambayo ni muhimu kwa uwezo wake wa kuboreshwa. Kwanza, hutumia dhana ya blockchain ya kizazi cha 3 inayoitwa “proof-of-Stake” ili kufanya kazi za mtandao. Pia ina usanifu wa safu 2, na leja iliyotengwa na safu ya hesabu. Hatimaye, hutumia mbinu ya kutunza rekodi ambayo inaruhusu masasisho ya leja kwa kutumia sehemu ndogo tu za utendaji kazi wa taarifa iwezekanavyo. Chaguo hizi za muundo huiruhusu kuwa ya haraka sana, iliyokuzwa kimataifa, na iliyo na matumizi bora ya nishati.

Maadili ya kibinadamu.

Cardano ina sifa ya kuwa ya kibinadamu katika maadili yake, muundo na uzingatiaji wake. Maamuzi kuhusu jinsi mtandao unavyotengenezwa na kutumika hupendekezwa na kupigiwa kura na jamii. Hivyo basi, miradi ya Cardano huwa tofauti tofauti na yenye kuhamasisha, kama tu watu. Miradi ya Cardano ni pamoja na, kutumika kwa blockchain ili kutoa rekodi salama na imara za elimu kwa wanafunzi nchini Ethiopia, na kujenga zana mpya za kifedha kwa wakazi wasiostahili, kuanzisha na kufadhili maabara ya utafiti ya Blockchain katika vyuo vikuu, na kupea kipaumbele kwa utafsiri wa mafunzo na habari katika lugha zingine.Juhudi hizi zinatoa fursa ya kujumuisha miradi hii ya Cadano na kutoa nafasi ya watu kujiunga nayo kote ulimwenguni. Wazo la “kuendeshwa kwa kusudi” linaonekana wazi katika pembe zote za mfumo ikolojia wa Cardano, kuanzia na kanuni yake ya msingi ya “Kufikia kiwango cha juu zaidi cha ushirikiano wa kibinadamu”, na kushuka hadi kwenye Stake pool kama yetu, ambapo ni kawaida kupata. kwamba sehemu ya faida inaweza kutolewa kwa mashirika ya misaada na ya kibinadamu.

Watu ambao wanavutiwa na Cardano wanaweza kununua ADA. Unapomiliki ADA, unaweza kuunga mkono usalama wa mtandao, kupigia miradi kura, na kupata ADA zaidi kwa kukasimu kwa Stake pool kama LIDO Nation. Tofauti na mitandao ya proof Of Stake ambayo haifungii sarafu zako, na unahifadhi umiliki kamili wa sarafu zako wakati wote, kumaanisha unaweza kutumia au kuuza ADA zako wakati wowote.

Wamiliki wa Cardano wana uhuru wa kuchagua kati ya maelfu ya staking pools na mtandao unategemea ushindani wa haki kati staking pools nyingi nzuri. LIDO Nation inapania kuweka viwango ambavyo vinapaswa kufikiwa na kila staking pool. Msingi wa pool yoyote ni kwamba lazima iwe tayari na iwe na uwezo wa kufanya kazi kama nodi ya kompyuta kwa mtandao wa Cardano. Waendeshaji wabunifu wa pool wanatambua kwamba kuna mengi zaidi ambayo tunaweza na tunapaswa kufanya ili kuvutia wajumbe. Lido Nation inachukua maadili yanayoshikiliwa na jamii na kuyatumia kama msingi wa uwendeshaji wake. Ingawa tovuti nyingi za pool huhisi kama klabu ya techies na watu wenye ufahamu wa crypto, tunazingatia maudhui na rasilimali kwa watu wasio na ufahamu wa ndani kuhusu crypto. hatuna nia ya kupata sifa au pesa za haraka, lakini tunavutiwa sana na teknolojia ya msingi na athari zake kwa wanadamu. Tunachapisha maudhui mapya kila wiki, yenye vichwa vya habari, maarifa, na ufafanuzi wa mawazo changamano. Tunachangia sehemu ya faida zote kwa mashirika ya hisani yaliyochaguliwa na wawakilishi wetu. Zaidi ya hayo, tunachangia maendeleo ya mfumo wa ikolojia wa Cardano kwa kushiriki katika Kichocheo cha Mradi, ambayo ni mojawapo ya ubunifu wa cardano unaokuzwa. Ufadhili, maoni na fursa za ushirikiano kutoka kwa juhudi hizi hurejea kwenye hisa letu, na kuleta thamani zaidi kwa wawakilishi wetu, na kwa jamii kwa ujumla. Tunaamini kwamba Cardano ni teknolojia ya siku zijazo, na kwamba siku zijazo zinahusisha kila mtu

Get more articles like this in your inbox

What do you find most compelling about the Cardano Project?

Or leave comment
Share

No comments yet…

avatar
You can use Markdown
close

Playlist

  • EP2: epoch_length

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 3 se. 24
    Darlington Kofa
  • EP1: 'd' parameter

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 4 se. 3
    Darlington Kofa
  • EP3: key_deposit

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 3 se. 48
    Darlington Kofa
  • EP4: epoch_no

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 2 se. 16
    Darlington Kofa
  • EP5: max_block_size

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 3 se. 14
    Darlington Kofa
  • EP6: pool_deposit

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 3 se. 19
    Darlington Kofa
  • EP7: max_tx_size

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 4 se. 59
    Darlington Kofa
0:00
/
~0:00