Lido Nation - Getting in the middle of it

Teknolojia ya Blockchain ni njia yenye nguvu ya kutumia na kupanua mtandao kama tunavyoijua, na itabadilisha ulimwengu wetu.** Lido Nation imejitolea kwa elimu ya blockchain, rasilimali, na fursa kwa watu wa kila siku na wageni.**

Kwa hivyo blockchain ni nini? Kwanza kabisa, blockchain inahusu ugatuaji. Badala ya wavuti kote ulimwenguni ambayo inadhibitiwa zaidi na watoa huduma wachache wakubwa na watoa huduma wa kuhifadhi data, mtandao bora wa blockchain unaendeshwa na wewe, na mimi, na maelfu ya watu wengine kote ulimwenguni. Kupitia ushiriki wa kimataifa uliogatuliwa, blockchains zinaweza kutoa usalama usiolinganishwa, yenyekudumu, na inayoaminika. Zaidi ya hayo, kwa kuwa haijadhibitiwa na shirika lolote kuu, huduma na fursa zinazotolewa na blockchain zinaweza kupatikana zaidi na za bei nafuu kuliko zile za ulimwengu wa “urithi”.

>> Metaverse - anuwai - mtandao wa 3 - mapinduzi ya 4 ya kiviwanda: maneno haya ya mtindo yote yanahusiana na wazo la ugatuaji wa wakati ujao.

Kama mtandao, teknolojia hii italeta fursa nyingi mpya, lakini kwa wakati huu ni ya kushangaza kwa watu wengi. Kupata habari nzuri juu ya blockchain inaweza kuwa changamoto. Habari nyingi mkondoni hutolewa kwa vikao vya watengenezaji wa teknolojia na nakala zilizoandikwa kwa nyanja kifedha. Mbaya zaidi, ingawa inaweza kutabirika, ni watu wasio na tabia nzuru: watu wanaoeneza ukuzaji na mpango unaofuata wa utajiri wa haraka. Habari za kawaida haziachi hamu, kwani vichwa vya habari vya kila siku havina muktadha na unganisho kwa picha kubwa.

Ahadi za kusisimua za ugatuaji zinaweza kufikiwa tu wakati sisi sote tunaweza kushiriki. Sio tu kwa watu wa teknolojia, au vijana, au wawekezaji wajasiri. Wakati ujao ni kwa kila mtu - na ndipo ambapo Lido Nation inakuja! Kuna zaidi ya mradi mmoja wa blockchain ulimwenguni; Bitcoin ndiyo iliyoanza, na Ethereum kujengwa kwa msingi huo. Katika miaka iliyofuata, wengine wengi wametokea. Tunavutiwa zaidi na mradi unaoitwa Cardano, na sarafu yake inayoitwa ADA.

Kwa nini tulichagua Cardano?

Sasa kuna maelfu ya miradi ya blockchain huko nje; Kwa kweli, kuna mtandao mpya na “sarafu ya alt” karibu kila siku. Kile usichoweza kujua ni kwamba nyingi ya hizi sio fikra mpya, ya asili. Nyingi ni nakala za itifaki za Bitcoin au Ethereum, na lebo mpya kwenye ufungaji. Baadhi yao huongeza ladha yao wenyewe na kuibadilisha hapa au pale, lakini nyingi ni nakala za unakili, wakitarajia kutengeneza milioni au bilioni ya pesa. Miradi mingine ina maoni ya asili, lakini zimeundwa kwa kusudi nyembamba, kama zana maalum ya kifedha, mchezo, au jukwaa la NFT. Miradi mingi ya blockchain ya umma huingia sokoni na ICO, “Initial Coin Offering” inayoongeza pesa kwa mradi huo. Kutoka hapo, itafanikiwa au ikose kufanikiwa. Zingine zinaweza kuwa muhimu na yenye dhamani kwa muda mrefu, lakini nyingi hazitafanikiwa, ikiwa watakosa pesa za kukuza na kudumisha mtandao wao kabla ya kuthaminiwa sana. Zaidi ya hayo, zile ambazo hutegemea itifaki sawa na Bitcoin na Ethereum hutegemea nguvu ya kompyuta nzito na utumiaji wa nishati kufanya kazi za mtandao, ambayo huzua maswali juu ya uwezo wa kuboreshwa na uendelevu. Wengine huzingatia kasi na kiwango, lakini wanasahu usalama.

>> Cardano ni tofauti kabisa. Ubunifu wake ni wa asili, kwa msingi wa utafiti wa kitaalam uliopitiwa na watu wa rika sawa. Ilijengwa kwa matumizi ya muda mrefu, kuongeza kiwango cha ulimwengu, usalama wa hali ya juu, na maadili ya kibinadamu.

Wacha tuzingatie kila moja ya haya:

Huduma ya muda mrefu

Tofauti na miradi ambayo ilinakatika wakati pesa kutoka ICO zao zinamalizika, Cardano ilibuniwa na hazina ya kujipatia pesa. Sehemu ya ada ya mtandao imeelekezwa kwa hazina ambayo inafadhili maendeleo ya mtandao na matengenezo. Hii inalinda Cardano kutokana na kushuka na kupanda kwa soko la ulimwengu, na inahakikisha uwezekano wa muda mrefu na nguvu.

Kuongeza kiwango ulimwenguni

Cardano ina vitu kadhaa vya kubuni ambavyo ni muhimu kwa uwezo wake wa kuongeza. Kwanza, hutumia wazo la kizazi cha 3 cha blockchain linaloitwa “proof-of-stake” kufanya kazi za mtandao. Pia ina usanifu wa safu-2, na leja iliyowekwa tofauti na safu ya hesabu. Mwishowe, hutumia njia ya kutunza rekodi ambayo inaruhusu visasisho vya leja kwa kutumia tu vifaa vidogo vya habari iwezekanavyo. Chaguzi hizi za kubuni huruhusu iwe haraka sana, ina kiwango cha juu ulimwenguni, na ina nguvu sana ya nishati.

Usalama

Cardano hutumia utaratibu sawa wa usalama kama Bitcoin, ambayo imejidhihirisha kuwa salama sana. Walakini, Bitcoin inatumia carboni kwa ukubwa, inategemea mashine maalum ambazo zinahitaji umeme mkubwa. Kwa Cardano, badala ya kununua mashine ya bei ghali na yenye kutumia nishati kwa wingi, badala yake lazima uwe na sarafu, ADA. Itifaki ya usalama na Leja ya Cardano imethibitishwa kuwa salama dhidi ya aina tofauti za shambulio, ikidhaniwa kuwa zaidi ya 50% ya node na ADA kwenye mfumo huo inadhibitiwa na watendaji waaminifu ambao hawako kwenye vifijo. Usalama wa Cardano pia umejaribiwa katika ulimwengu wa kweli - mtandao umekuwa ukifanya kazi tangu mwaka wa 2017 bila matukio yoyote ya usalama.

Maadili ya kibinadamu

Cardano haswa ni ya kibinadamu katika maadili, muundo na umakini wake. Uamuzi juu ya jinsi mtandao unavyotengenezwa na kutumiwa unapendekezwa na kupigiwa kura na jamii. Hivyo basi, miradi ya Cardano ni tofauti na ya kusisimua, kama watu walivyo. Miradi ya Cardano ni pamoja na kutumia blockchain kutoa rekodi salama na imara za elimu kwa wanafunzi nchini Ethiopia, na kuunda zana mpya za kifedha kwa idadi ya watu waliohifadhiwa, kuanzisha na kufadhili maabara ya utafiti wa blockchain katika vyuo vikuu, na kuweka kipaumbele tafsiri ya mafunzo na rasilimali za habari katika lugha zingine. Jaribio hizi zinatengeneza njia na fursa ulimwenguni kote. Wazo la kuwa “ linaloendeshwa kikusudi“ linaonekana katika pembe zote za mfumo wa Cardano, kuanzia na maelezo maarufu, “kufikia kiwango cha juu cha ushirikiano wa kibinadamu”, na kuja chini kwa stake pools binafsi kama yetu, ambapo ni kawaida kupata kwamba sehemu ya faida inaweza kutolewa kwa mashirika ya kibinadamu na ya hisani.

Lido Nation

Tuko hapa kufungua njia kwa wageni ili wajifunze kuhusu Cardano, na kujiunga na safari ya siku zijazo za ugatuaji. Hapa kuna kile tunachofanya, na jinsi unaweza kushiriki:

Staking Pool

Lido Nation ni “Staking Pool” - au nodi kwenye mtandao wa Cardano. Cardano huchakata, huhalalisha, na kulinda shughuli mpya kwa kutumia mtandao uliosambazwa wa waendeshaji wa nodi, kama sisi. Wakati nodi ya Lido Nation inafanya kazi yake kwa Cardano, tunachangia katika operesheni salama ya mtandao, na tunapata zawadi za kifedha. Unaweza kushiriki kwa kununua ADA, na kuwekeza na Lido Nation. Hii inaitwa “kukabidhi” ADA yako. Wakati nodi yetu inapata zawadi za mtandao - nawe utapata pia! Tofauti na mitandao kadhaa za udhibitisho, kustake haifungi sarafu zako, na unashikilia umiliki kamili wa sarafu zako wakati wote, kumaaniksha kuwa unaweza kutumia au kuuza ADA yako wakati wowote.

Phuffycoin

Unapowekeza na Lido Nation, unapata tuzo za ADA, lakini pia unapata tokeni yetu, Phuffycoin. Phuffycoins inawakilisha nusu ya thawabu za ndani za staking pool yetu - ambayo tunatumika kutoa misaada. Lakini badala ya kutoa pesa tu ambapo tunataka na kukuambia juu yake, kwanza tunapeana pesa hiyo kwa wajumbe wetu, kwa njia ya Phuffycoins. Phuffycoins zina kusudi moja, ambalo ni kuelekeza utoaji wa hisani yetu. Unapopata Phuffycoins kama mjumbe, unapata kutuambia tutakapotoa pesa zetu!

Project Catalyst

Project catalyst ni mojawapo ya mambo ya kufurahisha zaidi katika mfumo wa ikolojia wa Cardano. Kumbuka Hazina ya Kujifadhili ambayo inalipa maendeleo ya mtandao? Njia moja ambayo hii hufanyika ni kupitia project catalyst. Kupitia jaribio hili (linalozidi kugatuliwa), watu wanapendekeza miradi na suluhisho ambazo zinaweza kusaidia mtandao kustawi na kukua. Wamiliki wa ADA wanapiga kura juu ya mapendekezo haya, na mapendekezo ya kushinda hupokea ufadhili wa kutekeleza maoni yao! Lido Nation ni mshiriki hai katika project catalyst katika majukumu anuwai, pamoja na kama mpendekezaji anayefadhiliwa. Unaweza kushiriki kwa kununua ADA, na kupiga kura kwa miradi ambayo unapenda kwa kutumia ADA yako. Ni kama kura katika mkutano wa wadau, isipokuwa wadau wanaweza pia kupendekeza hoja, au kufanya kazi hiyo!

Vyombo vya wapiga kura wa project catalyst

Lido Nation inapenda project catalyst. Tunataka kuisaidia kukua kutoka kwa asili yake, kama wazo kubwa, katika maisha yake ya baadaye - kama mafanikio makubwa! Kwa maana hiyo, tunadumisha hifadhidata ya umma ya aina yake ya project catalyst. Kupitia zana za utaftaji, vichungi, na chati, tunakuwezesha kutafiti kwa urahisi miradi ya zamani na ya sasa, wapendekezaji, na matokeo. Mteule aliye na habari ni yule ambaye amewekwa kufanya maamuzi mazuri na yenye nguvu. Unaweza kutumia zana zetu kujenga orodha yako wakati wa kupiga kura, na kujibu maswali ambayo unaweza kuwa nayo juu ya miradi na watengenezaji wa zana katika jamii.

Kuchapisha

Waandishi katika Lido Nation wanzifanya dhana kubwa kuwa za kueleweka kwa urahisi, na kutoa muktadha wa kuelewa ni kwanini unapaswa kujali. Wageni wa wavuti wanaweza kuingiliana katika maoni, au kuwasilisha maoni ya makala juu ya vitu ambavyo wanagependa kujifunza. Kwa zaidi ya mwaka mmoja, tulitoa nakala za kila wiki kuhusu blockchain na Cardano - bila kulipwa. Jamii iliamini kile tulichokuwa tunafanya, na walipiga kura katika project catalyst ili kutufadhili kuendelea na kazi hii. Tuliweza kuajiri mwandishi wa tatu na kuwalipa waandishi wetu waliopo ili kuendelea na kazi nzuri.

Maabara ya Lido blockchain

Kupitia pendekezo la project catalyst lililoshinda, tuliweza kupata maabara ya Ngong Road blockchain nchini Kenya. Hapa ni eneo la kwanza la mpango wetu wa Lido blockchain Labs, ambayo hutoa mafunzo ya ndani, elimu, kazi ya mkataba wa kulipwa, na fursa za mafunzo zilizozingatia Cardano blockchain. Sehemu za mitaa zimetambuliwa kama njia muhimu na nzuri ya kuongeza ufikiaji na athari za Cardano katika maeneo ya ulimwengu kama Afrika ambayo yanafaidika sana na blockchain. Unaweza kuona kazi ya wasanidi programu wetu wa blockchain katika tovuti ya Lido Nation, angalia tafsiri za Kiswahili na rekodi za sauti zilizoundwa na watafsiri wa maabara, na usome nakala za asili kuhusu Cardano kutoka kwa wafundishaji wetu wa maabara.

Lugha tofauti na vituo vingi

Tunajua kuwa kufanya maudhui kupatikana kwa watu zaidi kunamaanisha zaidi ya nakala tu zilizoandikwa kwa Kiingereza. Kupitia ufadhili wa project catalyst na programu ya Maabara ya Lido blockchain, tunatafsiri nakala kwa Uhispania na Kiswahili. Tunatazamia kuongeza lugha zaidi katika siku zijazo. Wavuti yetu inakubali matoleo ya sauti ya kila nakala iliyochapishwa, kwa kila lugha inayoungwa mkono! Mradi wa sauti ni ya umati wa watu: Ikiwa utaona nakala bila toleo la sauti, unaweza kubonyeza kitufe cha kurekodi na kusoma kwa sauti ili kuchangia nakala ya sauti! Unaweza pia kutupata kwenye Twitter @lidonation, ambapo tunachapisha maudhui mara kwa mara, na tunayo maonyesho ya “Twitter Space” ya moja kwa moja. Mpango wetu wa habari unaofuata unatoka baadaye mnamo mwaka wa 2022 - lidominute itatoa maudhui katika elimu katika viunzi vifupi. Video za Lidominute ziko kwenye chaneli yetu ya YouTube, na podikasti ya Lidominute itaenda moja kwa moja baadaye mwaka huu. Jitayarishe kwa fursa za kufurahisha za NFT na udhamini zinazoandaliwa kwa podikasti ya Lidominute!

Lido Nation inachukua maadili yaliyoshikiliwa na jamii ya Cardano na kujenga juu yake. Wakati tovuti nyingi za blockchain zinahisi kama klabu cha watu waliobobea kiteknolojia na wa ndani wa crypto, tunazingatia maudhui, rasilimali, na fursa kwa watu wa kila siku. Hatuvutiwi na kutengeneza pesa za haraka, lakini tunavutiwa sana na teknolojia na athari zake kwa wanadamu. Tunaamini kuwa Cardano ni teknolojia ya siku zijazo, na kwamba siku zijazo zitajumuisha kila mtu.

Get more articles like this in your inbox

Was the article useful?

Or leave comment
Share

No comments yet…

avatar
You can use Markdown
close

Playlist

  • EP2: epoch_length

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 3 se. 24
    Darlington Kofa
  • EP1: 'd' parameter

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 4 se. 3
    Darlington Kofa
  • EP3: key_deposit

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 3 se. 48
    Darlington Kofa
  • EP4: epoch_no

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 2 se. 16
    Darlington Kofa
  • EP5: max_block_size

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 3 se. 14
    Darlington Kofa
  • EP6: pool_deposit

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 3 se. 19
    Darlington Kofa
  • EP7: max_tx_size

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 4 se. 59
    Darlington Kofa
0:00
/
~0:00