Makala ya Project Catalyst #02 - Project Catayst/ Wanasayansi Wenye ujuzi kwenye uzunduzi

Ikiwa unajua kuhusu project catalyst, huenda unajua zaidi kuhusu sehemu ya mbele inayoutazama umma: Kampeni, mapendekezo, kura. Katika awamu 8 za project catalyst hadi sasa, unaweza kuwa umeshiriki kwa kuhudhuria mkutano wa kila wiki wa “Town Hall”, labda kwa kuwa “Mshauri wa Jamii” anayelipwa ili kutathmini mapendekezo, au (tunatumaini!) kwa kupigia kura mapendekezo bora katika programu ya upigaji kura ya catalyst

** Kinachotokea baada ya kupiga kura bado hakifahamiki kwa wengi.

Kwa mapendekezo ambayo hayajashinda ufadhili, hakuna mengi ya kusema; washiriki hawa wanaaachwa kuzingatia maoni waliyopokea na kuamua jinsi gani au kama watajaribu tena. Lakini kwa mapendekezo yaliyofadhiliwa, safari ndiyo inaanza! Makala haya yatatoa mwanga kuhusu njia za safari hii.

Sisi katika Lido Nation tumepewa fursa ya kupata kazi kama wapendekezaji waliofadhiliwa katika awamu tatu zilizopita za project catalyst. Kabla ya kushinda mara ya kwanza, hatukujua la kutarajia - ni vipi kupata pesa hufanya kazi? tunaripoti kwa nani? Ni nini kinachotarajiwa kutoka kwetu - zaidi ya kile kinachotolewa katika pendekezo letu?

Iwapo umefikiria kutafuta ufadhili kupitia project catalyst, hii inaweza kukusaidia kujiandaa kwa ajili ya kile kilicho mbele yako na kuweka matarajio ya kweli au halisi. Unaweza kusoma maelezo haya na kutambua jinsi ujuzi na maarifa yako yanaweza kuwa ya muhimu kwa jaribio. Hata kama huna nia ya kuwa mpendekezaji wewe mwenyewe, wewe ni sehemu ya jamii hii, na sisi ni bora pamoja.

Kutoka kwa kiwango cha juu, uzoefu wa wapendekezaji unaofadhiliwa una sehemu tatu: Kuanza, Ufadhili na Kuripoti, na Kukamilisha Mradi.

Funded Project Lifecycle

Leo tutajadili mchakato wa kuanza

Fomu ya Kuanza

Ndani ya siku chache baada ya matokeo ya upigaji kura, wapendekezaji wanaofadhiliwa wanaombwa kujaza fomu ya kuanza. Fomu hii ilitumikia kwa kazi tatu za kimsingi:

Kukusanya maelezo ya mawasiliano ya kiongozi wa mradi, ikiwa ni pamoja na barua pepe, telegramu na discord.

Thibitisha anwani ya pochi la Cardano kwa ajili ya malipo. Anwani za pochi huwasilishwa pamoja na mapendekezo mwanzoni mwa mchakato. Bado, watu mara nyingi hudhibiti pochi nyingi kwa sababu tofauti na wanaweza kuwa na upendeleo wa pochi flani wanaposhinda ufadhili.

Onyesha tarehe ya kumalizika kwa mradi. Mapendekezo katika Ideascale kwa kawaida hujumuisha dhana fulani ya ratiba ya matukio, lakini (ajabu, labda) hakuna tarehe maalum ya kukamilisha inayohitajika kwenye mapendekezo. Hata hivyo, wakati wa kuanza, tarehe ya mwisho inahitajika.

Fomu ya kuanza imekua na mabadiliko kidogo ndani ya hazina maalum tatu ambazo tumeshiriki, lakini matumizi ya jumla yamekuwa thabiti.

Uthibitisho wa Maisha

Kidhahania, itawezekana kwa mtu kuwasilisha pendekezo kwenye Ideascale kwa matakwa na kisha kulisahau. Mtu huyohuyo anaweza kushinda ufadhili, na kugundua tu kwamba wamejiingiza na hawana wakati, utaalam, au mwelekeo wa kufanya kazi aliyojiandikisha. Sababu zozote zile, kuna haja ya wapendekezaji waliofadhiliwa kujitokeza kwenye mkutano ili kuthibitisha kwamba wao ni wa kweli, wanahusika, na wana kile wanachohitaji ili kuwasilisha mawazo yao makuu. Fedha za Hazina hazitolewi bila ushiriki wa kibinadamu. Kusudi hili limetekelezwa na mkutano mkubwa wa zoom, inayotolewa kwa muda tofauti, kwa wapendekezaji wote wanaofadhiliwa kukusanyika na kuthibitisha ushiriki wao. Unaitwa mkutano wa “Uthibitisho wa Maisha”.

Katika kipindi cha ufadhili tatu, muundo wa mkutano huu umebadilika ili kushughulikia makundi yanayokua ya timu zinazofadhiliwa. Mara ya kwanza tulipohudhuria, ilikuwa ni sarakasi kidogo, na karibu watu 100 waliohudhuria, kila mmoja akihitajika kuchukua zamu yake binafsi kushiriki utambulisho wao na jina la pendekezo. Wakati uliofuata, mambo yalikuwa tofauti - badala yake tulikutana katika makundi kwa vipindi vifupi kupitia Kampeni ili kujitambulisha. Hivi majuzi, kulikuwa na mkutano mmoja mkubwa wa mwelekeo wa kikundi. Mikutano ya kibinafsi ya uthibitisho wa maisha iliratibiwa kando, ikipangwa na timu zinazoongoza kila Kampeni - zinazoitwa challenge teams.

Jaribio la Miamala

Wapendekeza wanaofadhiliwa hulipwa katika ADA. Kwa kuwa miamala ya blockchain haiwezi kutenduliwa, ni muhimu kuhakikisha kuwa maelezo ya malipo ni sahihi. Baada ya uthibitisho wa maisha kuthibitishwa, miamala ya majaribio katika kiasi cha ADA 1 hutumwa kwa anwani ya pochi zilizowekwa katika fomu za kuanza. Mara tu wapendekezaji wanapothibitisha kupokea muamala wa jaribio, wako tayari kuanza. Mchakato wa uthibitishaji sio mchakato kwa sana kwani wahusika - wapendekezaji huthibitisha kupokea kupitia barua pepe, gumzo za kikundi cha telegraph, au ujumbe wa simu kwenye jukwaa la kijamii walilochagua! Nisingependa kuwa mtu anayechunga kundi hilo la paka wenye furaha, lakini kwa namna fulani kazi inakamilika. Nadhani mtu atavumbua njia bora ya kuifanya hivi karibuni.

Timu za Changamoto

Timu za Changamoto ni nyongeza ya hivi majuzi kwa mfumo wa ikolojia wa project catalyst. Timu za Changamoto ni kikundi kidogo cha viongozi walioteuliwa kwa kila Kampeni. Inaweza kujumuisha mtu/watu waliopendekeza changamoto ya Kampeni katika hazina iliyotangulia, au inaweza kuwa mtu mwingine atakayejitokeza. Viongozi hawa wa timu wamekusudiwa kutumika kama rasilimali na washirika wa uwajibikaji kwa wapendekezaji wanaofadhiliwa. Zaidi ya mikutano inayoongoza ya uthibitisho wa maisha, sidhani kama majukumu yao yameratibiwa kikamilifu. Kwa pendekezo moja lililofadhiliwa, kiongozi wangu wa “Timu ya Changamoto” amekuwa akiwasiliana kupitia barua pepe kila mwezi, akihitaji nionyeshe mambo yanayowasilishwa kulingana na ramani ya njia ya pendekezo langu, na kutoa usaidizi kama itatakikana. Viongozi wengine wa Timu ya Changamoto wamekuwa watulivu kiasi - kwa kweli, hata sijui wao ni akina nani. Inaonekana kama Timu za Changamoto ni wazo zuri ambalo bado liko changa, na ninatarajia tutaona muundo na uwazi zaidi ukianzishwa kwa jukumu hili.

Rasilimali

Mara tu mwanzo unapokamilika na malipo ya kwanza ya pesa kutokea, ni wakati wa timu za mapendekezo kuanza kazi! Kazi inavyoendelea, bado kuna kipengele cha ushirikiano wa timu, ushirikiano, na uwajibikaji wa pande zote, unaohudumiwa na mikutano na rasilimali nyingi za jamii. Hizi ni pamoja na:

+Mikutano ya zoom ya Kila Wiki mara Mbili: Mikutano hii ya hiari ya wapendekezaji wanaofadhiliwa ni mahali pa kuripoti kwa kikundi pamoja na maendeleo yako, kutafuta maoni, na kuwasiliana na wajenzi wenzako.

+njia za Kijamii: Hizi ni pamoja na chaneli ya Telegramu ya matangazo ya wapendekezaji wanaofadhiliwa, nyingine ya gumzo la jumla la kikundi, na wakati mwingine vikundi maalum vya vikundi vya Kampeni. Pia inajumuisha angalau kituo kimoja cha Discord kwa wapendekezaji wanaofadhiliwa - na pengine zaidi kwa vikundi mbalimbali vya ushirika.

+Saa za Ofisi za Timu za Changamoto: huu ni utangulizi mpya na sehemu ya uchapishaji wa Timu za Changamoto kama suluhu iliyogatuliwa zaidi na inayoweza kupanuka kwa miunganisho ya vikundi.

Kwa wakati huu, rasilimali nyingi hutoka na huongozwa na uongozi wa kati: timu ya project catalyst katika IOG. Rasilimali nyingine zilizogatuliwa ambazo zinaundwa kwa kutafuta mapengo ya kujaza, na kuongeza thamani. Makala hii ni mfano wa juhudi kama hizo: tuliona pengo katika maarifa ya umma kuhusu uzoefu wa wapendekezaji unaofadhiliwa na tunajaribu kuziba. Jambo kuu kuhusu Project Catalyst ni kwamba juhudi hizo hazihusishwi tu bali zinahimizwa!

Hitimisho

Mustakabali wa project catalyst, na Cardano, ni uliogatuliwa. Hiyo ina maana kwamba kila sauti na kila wazo linaweza kupata kuskizwa - sio tu kwa waanzilishi na Wakurugenzi Wakuu kutuambia jinsi inavyopaswa kufanya kazi! Jaribio hubadilika kwa kila marudio, na tunafurahi kuwa sehemu yake. Jamii ilipiga kura ya NDIYO kuhusu pendekezo letu la kuandika makala zaidi kuhusu project catalyst. Asante kwa kura zako, na asante kwa kujitokeza kujifunza! Katika awamu inayofuata, tutaendelea kufuatilia safari ya Mpendekeza Anayefadhiliwa na kujifunza kuhusu Kuripoti, Ufadhili, na Kukamilisha Mradi.

Related Links

Get more articles like this in your inbox

Was the article useful?

Or leave comment
Share

No comments yet…

avatar
You can use Markdown
close

Playlist

  • EP2: epoch_length

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 3 se. 24
    Darlington Kofa
  • EP1: 'd' parameter

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 4 se. 3
    Darlington Kofa
  • EP3: key_deposit

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 3 se. 48
    Darlington Kofa
  • EP4: epoch_no

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 2 se. 16
    Darlington Kofa
  • EP5: max_block_size

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 3 se. 14
    Darlington Kofa
  • EP6: pool_deposit

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 3 se. 19
    Darlington Kofa
  • EP7: max_tx_size

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 4 se. 59
    Darlington Kofa
0:00
/
~0:00