Makala ya project catalyst #03 - Wanasayansi wenye ujuzi

Katika makala iliyotangulia, tulijifunza kuhusu mchakato wa kuanza kwa Wapendekezaji Waliofadhiliwa na project catalyst. Wakati huu, tutajifunza jinsi wapendekezaji waliofadhiliwa hupokea ufadhili wao, kuripoti maendeleo yao, na kukamilisha miradi yao. Iwapo itasaidia kuupitia kuhusu makala ya "project catalyst ni nini," angalia makala ifuatayo: https://www.lidonation.com/en/posts/cardanos-project-catalyst-experiments-in-decentralized-autonomous-organization-dao

Hali ya kazi ya mpendekezaji aliyefadhiliwa inatofautiana sana, kulingana na asili ya kazi. Miradi mingine inawezakua kazi ya siku chache kwa mtu mmoja; zingine ni za muda mrefu na zinalengo, kwa mfano, tafsiri, uundaji wa rasilimali, au kunda misimbo ya programu. Zingine zinahusisha kuajiri na kupanga timu kwa majukumu tofauti ili kutekeleza mradi huo. Bila kujali ukubwa na upeo wa kazi, wapendekezaji wote wanaofadhiliwa hufuata muundo sawa wa kuripoti, ufadhili, na kukamilisha mradi.

Kuripoti

Wapendekezaji Waliofadhiliwa wanatarajiwa kuwasilisha ripoti ya kila mwezi kuhusu maendeleo yao. Kwa sababu ya aina mbalimbali za miradi yaliyofadhiliwa, fomu za kuripoti ziko wazi. Viongozi wa mradi huombwa kuthibitisha tarehe yao ya mwisho wa mradi, kuripoti vikwazo au masuala yoyote waliyokumbana nazo, na kutoa viungo au upakiaji wa bidhaa zinazohusika.

Kwa miradi ya kwanza tuliyofadhiliwa, hitaji la kuripoti lilikuwa mara 2 kwa mwezi. tulianza kuhisi kama tunafanya kazi mingi ya kuunda ripoti kuliko kazi halisi ya mradi! na sasa yamepunguzwa hadi mara moja kwa mwezi. Hili ni jambo la busara zaidi, lakini kwa kuwa sasa timu yetu ina miradi mingi inayofadhiliwa, bado ni kazi kubwa. Ni muhimu kutambua kwamba kuboresha mahitaji haya kunahitaji kushiriki kikamilifu katika Jamii ya catalyst––zaidi kuhusu hili katika hitimisho hapa chini.

Ripoti za mradi ni za umma! Unaweza kutazama hati hii ya umma na kupata mradi unayoipenda kwenye viungo vilivyo hapa chini.

Ufadhili

Utoaji wa fedha hauji kwa kutolwa mara moja. Badala yake, imegawanywa katika mgao sawa wa kila mwezi kulingana na kiasi cha Dola cha bajeti yako; niruhusu nieleze. Miradi kwa sasa inapangiwa bajeti na kushinda kwa kiasi cha Dola ya Marekani, lakini hulipwa kwa ADA. Kwa hivyo, kiasi cha ADA unachopokea katika malipo yako ya kila mwezi kitategemea na bei ya ADA siku hiyo. Tuseme malipo yako ya kila mwezi yamewekwa kuwa $1,000. Ikiwa ADA ina thamani ya $0.50 katika mwezi wa kwanza wa mradi wako, utapokea ADA 2000 (yaani ADA yenye thamani ya $1,000) kama malipo yako. Ikiwa mwezi unaofuata, bei ya ADA imepanda hadi $2, basi utapokea ADA 500 (yaani bado ADA yenye thamani ya $1,000).

Kipengele hiki cha mchakato kinaweza kuanzisha kipengele cha matatizo kwa timu kubwa ambapo kunaweza kuwa na wachangiaji wengi wakulipwa, labda ikiwa ni pamoja na wakandarasi ambao wangependelea kulipwa kwa fedha za kawaida. Wasimamizi wa fedha wa miradi wanahitaji kupima hatari na mazingatio haya na kufanya mpango wa busara. Ikiwa kulipa wakandarasi katika fedha za kawaida ni muhimu, inaweza kuwa bora “kutoa” malipo yako ya ADA mara moja ili kuepuka hasara inayotokana na kushuka kwa bei - au mbaya zaidi, kushindwa kulipa timu yako.

Tumeona marekebisho kadhaa kwenye mpango wa malipo katika vipindi vyote vya ufadhili. Katika ufadhili za awali, kiasi cha malipo kiligawanywa katika malipo kadhaa ya kila mwezi - lakini hazikuhusishwa na urefu wa jumla wa mradi au kukamilika kwa mradi. Hii ilimaanisha kuwa mradi mfupi ungemaliza kazi yao na bado watalazimika kusubiri pesa zao, na kinyume chake, mradi wa muda mrefu ungepata pesa zao zote katika miezi michache ya kwanza, muda mrefu kabla ya kumaliza kazi hiyo. Hii haikufanya kazi vizuri kwa sababu kadhaa, ikiwa ni pamoja na kwamba hapakuwa na ishara kwa timu kuonyesha kukamilika kwa mradi! Hata kama walikuwa wakikamilisha kazi yao kwa uwajibikaji, ilikuwa ya kushawishi na rahisi kutangatanga au kuruka katika mradi unaofuata bila kufanya kazi muhimu ili kuonyesha kukamilika kwa mradi. Vyovyote vile sababu,awamu za mapema au za kwanza za project catalyst zimekuwa na viwango vya chini vya ripoti za kukamilika kwa mradi zilizowasilishwa hadi sasa.

Sasisho mbili za mpango wa malipo zimeanzishwa:

  • Kwanza, timu zinahitajika kutaja tarehe ya mwisho. Kisha malipo hugawanywa katika kipindi hicho cha muda. Mradi wa miezi mitatu utapata malipo ya kila mwezi mara tatu; mradi wa miezi kumi na mbili utapata kumi na mbili. (Bila kujali urefu, miradi yote pia yanapokea malipo ya “Uzinduzi” na malipo ya kukamilisha - kwa hivyo idadi halisi ya malipo ni “urefu wa mradi katika miezi” pamoja na mbili zingine)
  • Pili, malipo ya mwisho yanategemea kuwasilishwa kwa ripoti ya kukamilika kwa mradi.

Pamoja na kuboreshwa kwa uwazi na uwajibikaji wa umma pamoja na zana za utafiti za Lido Nation project catalyst, masasisho haya tayari yanaongoza kwa ripoti za Kukamilika kwa Mradi.

kukamilika kwa mradi

Kwa wakati huu, mchakato wa kumalizwa kwa mradi unahitaji ripoti iliyoandikwa na video kuwasilishwa.

  • Ripoti Iliyoandikwa: Timu za mradi zinatarajiwa kuweka pamoja hati zilizoandikwa zinazoonyesha kukamilika kwa mradi. Hii ni pamoja na kukagua matokeo yanayoweza kupimika yaliyoahidiwa katika pendekezo na kutoa uthibitisho unaofaa. Muhtasari wa ripoti pia ulazimu wapendekezaji kutafakari juu ya changamoto za mradi, mafunzo, na hatua zinazofuata. +** Video**: Miradi mingi yanahitaji “onyesho” ili kuelezea na kuelewa kilichojengwa. Hapo ndipo video ya kakamilika inaingililia! Timu za mradi zinaombwa kutoa video fupi (dakika 2-5) na “kuonyesha na kuwaambia” kile wameunda. Mbali na kutoa rekodi muhimu ya kazi, video teule zinaweza kushirikiwa kwa upana zaidi na uongozi wa Project Catalyst kwenye vituo vya kijamii au mikutano ya zoom.

Ripoti za Kufunga Mradi pia ni za umma na zinaweza kupatikana katika hati sawa na ripoti za Hali ya Mradi. Unaweza kuipata kwenye viungo vilivyo hapa chini.

Hitimisho

Project Catalyst ina wakosoaji wake. Hakika, mtu yeyote ambaye ameshiriki katika kiwango chochote amepata jambo la kulalamika kuhusu: “Programu ya kupiga kura haifai watumiaji!” “Mchakato wa CA ni fiche sana!” “Wapendekezaji wanaofadhiliwa wana makaratasi mengi sana!” Badala ya kuzingatia matatizo, na katika jitihada za kisayansi, napendekeza tuzingatie maendeleo - uthibitisho kwamba uboreshaji hutokea kutokana na ushiriki wa vitendo. Katika awamu tatu tu ambazo tumeshiriki kama wapendekezaji wanaofadhiliwa, tumeona mabadiliko na maboresho yakifanyika katika kila awamu, kutoka kwa kuanza hadi kuripoti hadi kukamilika kwa mradi. Kama unavyoweza kujua, ufafanuzi hasa wa project catalyst ni kwamba ni jaribio linaloendelea. Kufanya mabadiliko na kujaribu mawazo mapya sio ishara kwamba yamevunjika; kinyume kabisa, ni uthibitisho kwamba inafanya kazi. Kuna kazi zaidi ya kufanya, na tunatumai utakuwa sehemu yake - kwa sababu siku zijazo ni za kila mtu!

Related Links

  • Project Catalyst Monthly Reports Google Spreadsheet
  • Project Close Reports - Funded Project Dashboard Google Spreadsheet

Get more articles like this in your inbox

Was the article useful?

Or leave comment
Share

No comments yet…

avatar
You can use Markdown
close

Playlist

  • EP2: epoch_length

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 3 se. 24
    Darlington Kofa
  • EP1: 'd' parameter

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 4 se. 3
    Darlington Kofa
  • EP3: key_deposit

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 3 se. 48
    Darlington Kofa
  • EP4: epoch_no

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 2 se. 16
    Darlington Kofa
  • EP5: max_block_size

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 3 se. 14
    Darlington Kofa
  • EP6: pool_deposit

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 3 se. 19
    Darlington Kofa
  • EP7: max_tx_size

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 4 se. 59
    Darlington Kofa
0:00
/
~0:00