Fanya pendekezo lako kuwa pendekezo la kushinda

Katika hazina maalum ya 6 ya Project Catalyst, Lido Nation ilifadhiliwa kufanya kazi na kikundi cha wazungumzaji asilia wa Kiswahili nchini Kenya. Tuliwasaidia kujifunza kuhusu Cardano, kutafsiri makala za Lido Nation katika Kiswahili, na hatimaye kuandika maudhui yao halisi kuhusu Cardano kwa hadhira inayozungumza Kiswahili. Makala haya ni sehemu ya mfululizo wa maudhui ya Kiswahili!

Project Catalyst ni jaribio la uvumbuzi wa jamii ambapo mawazo hupendekezwa na kugeuzwa kuwa miradi yenye matokeo ambayo inakusudiwa kuendeleza mfumo ikolojia wa Cardano. Mapendekezo kama tujuavyo kwa kawaida huwasilishwa kwa Project Catalyst kupitia Ideascale. Awamu ya ufadhili kwa Project Catalyst hufanyika takriban kila wiki 12. Katika kila awamu, mapendekezo mapya huwasilishwa. Ikiwa una pendekezo lolote, basi unaliwasilisha katika changamoto zozote zinazopatikana kwa awamu hiyo ya ufadhili. Baada ya kuwasilisha, inapitia hatua tatu tofauti; uvumbuzi, utawala na utekelezaji. Kila pendekezo lina uwezo wa kupata ufadhili lakini unahitaji kuwa umefanya baadhi ya mambo ya ziada ili kufanya pendekezo lako lionekane na kupata kura za kutosha kutoka kwa jamii ili uweze kushinda. Kupitia kila hatua, kuna mikakati tofauti ambayo wewe kama mpendekezaji wa mradi unaweza kunufaika nayo na kuweka pendekezo lako kwenye njia sahihi.

Hapa kuna njia za kuhakikisha kuwa unafanya pendekezo lako liwe la kushinda

Ukaguzi wa kina wa kampeni

Kwenye ukurasa wa nyumbani wa Ideascale, kwa kawaida kuna orodha ya kampeni zinazoendelea kwa awamu iliyopo ya ufadhili. Kampeni hizi, ambazo wakati mwingine hujulikana kama changamoto, zinaangazia maeneo tofauti ambapo mfumo ikolojia wa Cardano unahitaji kukua na kuendelea. Kampeni pia hufafanua aina tofauti ambapo unaweza kuwasilisha pendekezo lako. Kategoria hizi huamuliwa na jamii iliyopiga kura katika awamu iliyopita. Unahitaji uchanganuzi makini na ukosoaji unapozipitia ili kuhakikisha kuwa pendekezo lako linalingana na aina hiyo mahususi. Usipitie tu kichwa cha habari na mukhtasari mfupi, hakikisha kuwa umeelewa tatizo, malengo na vipimo vinavyoshughulikiwa katika changamoto hiyo. Hii itakusaidia kuweka pendekezo lako katika changamoto inayofaa, ambayo huongeza nafasi zake za kushinda ufadhili.

Wasilisha pendekezo lako mapema

Baada ya kuandaa pendekezo lako, liwasilishe mara moja kwa changamoto inayofaa. Hii ni kwa sababu pindi inapowasilishwa mapema, una nafasi ya kupata maoni ya jamii kuhusu pendekezo lako katika sehemu ya maoni. Ikiwa kuna mabadiliko yoyote au uboreshaji unaohitajika, utapata wakati wa kufanya hivyo. Usisubiri siku za mwisho kuwasilisha pendekezo lako kwani huenda lisipate maoni au mchango wowote kutoka kwa jamii.

Kuwa na vipimo na hatua muhimu zinazoweza kupimika

Wakati washauri wa jamii wanatathmini pendekezo lako, moja ya mambo muhimu ambayo wanataka kuhakikisha kuwa pendekezo lako linayo ni uwezo wa kukaguliwa: ni malengo gani yanayoweza kupimika utaweza kufikia? Pia wanahitaji kuona jinsi unakusudia kupanga fedha zako, kwa hivyo jumuisha bajeti iliyo wazi na ya kina. Ni muhimu pia kuwa na mpango mzuri: Je, ni ratiba na hatua gani unanuia kufikia. Ili kufanya hivyo, hakikisha kwamba pendekezo lako lina uwazi wa kifedha na kwamba una mpango unaoendana na mradi unaotaka kutekeleza.

Eneza habari kuhusu pendekezo lako

Kutangaza wazo lako ni muhimu vile vile. Unataka kuhakikisha kwamba wamiliki wa ADA ambao watapiga kura wanafahamu wazo lako ili waweze kulipigia kura. Kuna chaneli tofauti unaweza kutumia kama vile Twitter na YouTube. Kwenye Twitter, kuna onyesho la “Cardano Over Coffee” ambapo wageni huwasilisha miradi yao kila siku ya wiki. Hapa unaweza kufanya mradi wako ujulikane kwa jamii. Kwenye YouTube, unaweza kutumia chaneli yako ya YouTube ikiwa unayo. Ikiwa huna, anza kufuata watu wengine kwenyeYouTube wanaochapisha maudhui mazuri yanayohusiana na Cardano. Shiriki katika maoni, na labda uone ikiwa wanavutiwa na mradi wako.

Hitimisho

Kila pendekezo ni la kipekee katika mbinu yao ya kukuza mfumo ikolojia wa Cardano, lakini kuweka juhudi zinazohitajika kutafanya iwe bora zaidi kwako kupata kura za kutosha. Ikiwa utaweka bidii hiyo ya ziada, unaweza kuwa na uhakika wa kupata ufadhili!

Get more articles like this in your inbox

Was the article useful?

Or leave comment
Share

No comments yet…

avatar
You can use Markdown
close

Playlist

  • EP2: epoch_length

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 3 se. 24
    Darlington Kofa
  • EP1: 'd' parameter

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 4 se. 3
    Darlington Kofa
  • EP3: key_deposit

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 3 se. 48
    Darlington Kofa
  • EP4: epoch_no

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 2 se. 16
    Darlington Kofa
  • EP5: max_block_size

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 3 se. 14
    Darlington Kofa
  • EP6: pool_deposit

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 3 se. 19
    Darlington Kofa
  • EP7: max_tx_size

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 4 se. 59
    Darlington Kofa
0:00
/
~0:00