project catalyst: Uhakikisho wa ubora wa mapendekezo

Katika hazina maalum ya Project Catalyst ya 6, Lido Nation ilifadhiliwa kufanya kazi na kikundi cha wazungumzaji asilia wa Kiswahili nchini Kenya. Tuliwasaidia kujifunza kuhusu Cardano, kutafsiri makala za Lido Nation katika Kiswahili, na hatimaye kuandika maudhui yao halisi kuhusu Cardano kwa hadhira inayozungumza Kiswahili. Makala haya ni sehemu ya mfululizo wa maudhui ya Kiswahili, yaliyotafsiriwa kwa Kiingereza!

Katika kila awamu ya ufadhili jamii ya Cardano huja na changamoto ambazo watu wanapaswa kuja na suluhu/mapendekezo. Mapendekezo ambayo hutumwa kwa kawaida huwasilishwa na kudhibitiwa katika https://cardano.ideascale.com/. Baada ya mapendekezo kuwasilishwa, yanakaguliwa na Proposal Assessors (PAs - zamani walijulikana kama Community Advisors/CAs). PAs hukadiria mapendekezo kama zinafaa kwenye changamoto, na ubora wao kwa ujumla. Pia wanaweza kutoa maoni juu ya mapendekezo ya kuongeza mapendekezo ya kuboresha. Watu wanaofanya hivyo wanaitwa “Proposal Assessors” na ’Veteran Proposal Assessors.“

Proposal Assessors

Proposal Assessors hutathmini mapendekezo yanayotumwa kwenye ideascale . Wanatathmini mapendekezo kulingana na Athari, Uwezekano, na Ukaguzi. Kwa kukagua mapendekezo hayo hutoa taarifa bora kwa wapiga kura na wapendekezaji.

Mtu yeyote anaweza kuwa Proposal Assessors na kupata pesa kwa kuingia tu kwenye Ideascale na kujiandikisha ili kushiriki.

Swali moja ambalo nilikuwa nalo hapo awali lilikuwa: ikiwa mtu anaweza kuruhusiwa kuwa Proposal Assessor na bado mpendekezaji? Jibu la hili ni, ndiyo!, Mtu anaruhusiwa kushiriki kama Proposal Assessors wakati yeye pia ni mpendekezaji. Jambo pekee ni kwamba hawezi kukadiria mapendekezo ambayo ni ya aina sawa na yao, kwani hii inaweza kuleta mgongano wa kimaslahi.

The Veteran Proposal Assessor (VPAs)

Kando na Proposal Assessors , pia tuna The Veteran Proposal Assessor (VPAs). ndio hundi ya wakaguzi: wanahakikisha ubora wa mapitio yaliyofanywa na PAs ni ya viwango vya juu na wanachuja mapendekezo yaliyopitiwa vibaya.

The Veteran Proposal Assessor (VPAs) wako juu kidogo ya Proposal Assessors Mtu anaweza kuwa The Veteran Proposal Assessor (VPAs) na kupata ADA ikiwa umekuwa Proposal Assessor katika awamu mbili za ufadhili zilizopita au umekuwa VPA katika awamu tatu zilizopita tangu kuanzishwa.

Kumbuka pia:

  • Mtu anapokuwa Veteran Proposal Assessor na pia mpendekeza haruhusiwi kutathmini mapendekezo ambayo ni ya makundi sawa na yao.
  • Endapo kutakuwa na suala lolote litakalotokana na mapendekezo, PAs na VPAs wanaruhusiwa kuleta suala hilo mbele ya jamii kwa majadiliano zaidi.
  • VPAs na PAs wanatathmini mapendekezo kulingana na vigezo hivi vitatu, athari, uwezekano na “uwazi” wa ukaguzi.
  • Unapokuwa VPA kazi yako itajulikana, itabidi utoe maelezo yako ambayo yataunganishwa na kazi yako na kuchapishwa.

Mifumo ya ugatuaji hufanya kazi wakati sote tunashiriki na kuwajibishana. Huenda umefikiri kwamba wasanidi programu pekee wanaweza kushiriki katika mifumo yao, lakini sivyo! Proposal Assessors na Veteran Proposal Assessors ni kazi ambazo mtu yeyote anaweza kufanya, kushiriki, kupata pesa, na kusaidia kuchangia kujenga ulimwengu bora.

Get more articles like this in your inbox

Was the article useful?

Or leave comment
Share

No comments yet…

avatar
You can use Markdown
close

Playlist

  • EP2: epoch_length

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 3 se. 24
    Darlington Kofa
  • EP1: 'd' parameter

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 4 se. 3
    Darlington Kofa
  • EP3: key_deposit

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 3 se. 48
    Darlington Kofa
  • EP4: epoch_no

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 2 se. 16
    Darlington Kofa
  • EP5: max_block_size

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 3 se. 14
    Darlington Kofa
  • EP6: pool_deposit

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 3 se. 19
    Darlington Kofa
  • EP7: max_tx_size

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 4 se. 59
    Darlington Kofa
0:00
/
~0:00