Mikataba bora- Kasi & Urahisi

Katika hazina maalum ya 6 ya Project Catalyst, Lido Nation ilifadhiliwa kufanya kazi na kikundi cha wazungumzaji asilia wa Kiswahili nchini Kenya. Tuliwasaidia kujifunza kuhusu Cardano, kutafsiri makala za Lido Nation katika Kiswahili, na hatimaye kuandika maudhui yao halisi kuhusu Cardano kwa hadhira inayozungumza Kiswahili. Makala haya ni sehemu ya mfululizo wa maudhui ya Kiswahili!

Cardano imejulikana kufikia shughuli 250 kwa sekunde yaani Transaction Per Second (TPS) na mipango ya kukuza nambari hii iwe juu zaidi. Shughuli kwa sekunde 250 ina maana ya idadi ya shughuli inayopata kuchakatwa kwenye blockchain kila sekunde. Nambari hii inalinganisha vyema sana na mitandao mingine maarufu: Ethereum, kwa mfano, kwa sasa inachakata shughuli 30 kwa sekunde tu, ambayo inasababisha msongamano wa mtandao na gharama kubwa kwa watumiaji.

Kuzaliwa kwa Mikataba bora ilitokea mwaka wa 2014, wakati Charles Hoskinson na wengine walizindua blockchain ya kwanza ya kizazi cha 2, Ethereum, ambayo ilileta lugha ya programu kwa blockchain. Uwezo wa kuendesha mantiki yoyote ya upangaji wa kompyuta kwenye blockchain ilifanya mikataba bora kuwezekana. Mkataba bora hufanya kazi kwa kupachika sheria na masharti ya wahusika na kisha kutekeleza shughuli wakati sheria na masharti hayo mahususi yametimizwa. Mikataba bora hurahisisha watumiaji wa blockchain kupata mwingiliano salama na usioaminika.

Mikataba bora hufanya kazi vipi hasa?

Kama tu aina nyingine yoyote ya shughuli, kuna viunganishi vya maneno ambavyo hutumika kukuza sheria na masharti. “Ikiwa” na “Lini” huandikwa katika msimbo kwenye blockchain na kupachikwa ndani ya shughuli ili Mikataba bora iweze kuzifuata. Washiriki wanaohusika wanahitaji kufafanua sheria zote ambazo zitasimamia shughuli zao na kuhakikisha kuwa wanaangalia vizuizi vyote. Mfano wa shughuli ndani ya Mkataba bora itakuwa “Nitakulipa utakaponifulia nguo zangu” Hii ina maana kwamba utapata malipo mara tu unapomaliza kazi ya kufua.

Kwa ujumla, Mikataba bora huleta urahisi sana wakati wa kufanya shughuli. Imeghairi hitaji la wapatanishi ambao wangetekeleza shughuli hiyo, na ambao wanaweza hata kuibadilisha kwa manufaa yao ya kibinafsi, bila kutaja kwamba wanahitaji malipo fulani ili kutekeleza shughuli hiyo. Kasi inahakikishwa kwani Mikataba bora hujiendesha kiotomatiki. Hii ina maana kwamba mradi masharti yaliyowekwa awali yametimizwa, mkataba unatekelezwa mara moja. Hakuna kupoteza muda wakati wa kutekeleza shughuli. Kwenye Cardano, mikataba bora inaweza kufanya kile ambacho mwanadamu anaweza kufanya kama vile kupiga kura au hata kuweka hisa kwenye ADA yao.

Tuko mwanzoni tu mwa kile ambacho Mikataba bora inaweza kufanya. Chombo hiki kinapokuwa maarufu zaidi na kujulikana, kuwa na mtandao wa kuaminika na ulio na TPS ya juu itakuwa muhimu zaidi! Tunafikiri kuwa Cardano imejipanga vyema kuendelea kuwa kiongozi katika nafasi hii.

Get more articles like this in your inbox

Was the article useful?

Or leave comment
Share
Commenter avatar

Simple and well put information, easy to understand. Thanks for this information

💯 1
avatar
You can use Markdown
avatar
You can use Markdown
close

Playlist

  • EP2: epoch_length

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 3 se. 24
    Darlington Kofa
  • EP1: 'd' parameter

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 4 se. 3
    Darlington Kofa
  • EP3: key_deposit

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 3 se. 48
    Darlington Kofa
  • EP4: epoch_no

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 2 se. 16
    Darlington Kofa
  • EP5: max_block_size

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 3 se. 14
    Darlington Kofa
  • EP6: pool_deposit

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 3 se. 19
    Darlington Kofa
  • EP7: max_tx_size

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 4 se. 59
    Darlington Kofa
0:00
/
~0:00