Njia 8 za kushiriki katika project catalyst na Kupata Pesa katika hazina maalum ya 7!

Mnamo Novemba 11, wakati wa mkutano wa kila wiki wa town hall wa Cardano, Charles Hoskinson alitangaza kuanza kwa Hazina maalum ya 7 ya project catalyst. Nilihesabu watu waliohudhuria kwa zoom ni zaidi 500, miezi chache iliyopita, town hall kwa kawaida ilikua na takriban watu 50 waliokuwa wakihudhuria . Ukuaji huu unajitokeza katika kila sehemu ya jaribio la catalyst. Kwa mfano, bajeti imeongezeka maradufu kwa kila awamu. Katika awamu hii, dola milioni 6.4 zitatolewa kwa timu zinazopendekeza suluhisho la changamoto katika kategoria 21. Pia, kuna Milioni 1.6 zitakazotolewa kwa watu wanaoshiriki katika majukumu mengine katika mradi huo. Aina hii ya mwisho na bajeti mara nyingi hupuuzwa. Masuluhisho bunifu ya matatizo ndiyo yanayofanya project catalyst kua ya kusisimua sana, lakini hutokea tu wakati jamii hutekeleza majukumu mengi muhimu. Nafasi hizi ni rahisi na za muda mfupi. Ni njia nzuri ya kujifunza huku kusaidia kujenga kitu kipya - na kulipwa kukifanya!

Endelea kusoma ili upate maelezo kuhusu majukumu 8 yaliyofidiwa kwa ushiriki wa jamii katika Catalyst:

(Ikiwa ungependa kuanza na mukhtasar wai project catalyst, tuliandika kuihusu hapa:

https://www.lidonation.com/fr/posts/cardanos-project-catalyst-experiments-in-decentralized-autonomous-organization-dao. )

1) Wapendekezaji

Wakati watu wengi wanafikiria kuhusu project catalyst, wanawafikiria Wapendekezaji. Kimsingi, unapoingia kwenye Ideascale na kuangalia kote, mapendekezo ndio ya muhimu. Walakini, jukumu la mpendekezaji mara nyingi haieleweki. Mpendekezaji ni kama mwanzilishi - mwenye wazo. Wakati mwingine mtu huyo ana ujuzi wa kutekeleza mawazo yao, lakini mara nyingi hawatekelezi! Wanaweza kuwa na uwezo muhimu, kama vile ukuzaji wa biashara, uuzaji, n.k, lakini wanahitaji timu iliyo na ujuzi maalum ili kutekeleza wazo lao. Ikiwa una wazo, unaweza kushiriki katika catalyst kama Mpendekezaji anayetafuta watekelezaji.

2) Watekelezaji

Labda wewe ni mhandisi wa programu, msanidi programu, msanii wa graphic, mtafsiri, Guru wa kifedha, mchukua video, nk Unaweza kuenda kwa catalyst, kuvinjari mawazo, na kuungana na wapendekezaji wanaotafuta watu ili kutekeleza mawazo yao. Angalia sehemu ya “Timu” ya mapendekezo ambayo yanakuvutia; Mara nyingi kutakuwa na fursa zilizoorodheshwa za watu wenye seti maalum za ujuzi zinazohitajika ili kukamilisha timu.

3) Warejeleaji

Ikiwa unajua timu ambayo inaweza kufaidika kwa kujenga na Cardano, unaweza kuwaelekeza kutuma maombi ya ufadhili wa catalyst. Warejeleaji hushiriki maarifa kuhusu uzuri wa catalyst. Ukimrejea mtu kwa catalyst na pendekezo lao lipate ufadhili, nyote mtapata tuzo! Hazina maalum ya 7 itafanya dola 80,000 kupatikana kwa ajili ya fidia ya rufaa.

4) Mzunguko wa catalyst

Katika kipindi cha miaka miwili iliyopita ya ukuaji wa haraka tangu kuanzishwa kwa project catalyst, baadhi ya makundi ya washiriki na washikadau yaliundwa kiasili. Kwa mfano, waendeshaji wa nodi, wapiga kura (wamiliki wa ADA), na wapendekezaji waliofadhiliwa ni makundi yaliyo na maswala sawa na ambao kwa kawaida huzungumza na kila mmoja. Ili kutoa uwakilishi wa makundi haya na sauti ya moja kwa moja katika kuunda mradi huo, mzunguko wa catalyst ulianzishwa. Mzunguko wa catalyst ni “safu ya sensor ya kibinadamu inayofanya kama chombo cha uwakilishi kwa makundi yote tofauti yanayoshiriki katika project catalyst.” Watu ambao huketi kwenye mzunguko huo huchaguliwa kila baada ya miezi mitatu. Wanachama wa mzunguko huo hulipwa katika ADA. Bajeti ya dola 9,500.00 ya mzunguko huo yenyewe ni pendekezo la catalyst, ambalo lazima liidhinishwe katika kila awamu ya ufadhili ili kuendelea.

5) Timu za Changamoto

“Changamoto”, ambayo pia huitwa “kampeni”, hufafanua matatizo ambayo jamii inapaswa kutatua kwa mzunguko fulani. Katika hazina maalum ya 7, kuna zaidi ya “changamoto” 20 za kipekee. Mawazo na masuluhisho yanayopendekezwa lazima yaingiane na changamoto iliyobainishwa. Timu za changamoto huzisimamia katika catalyst. Wanafuatilia maendeleo na kuripoti kwa jamii kuhusu kama na jinsi changamoto zilishughulikiwa. Mawasilisho hufanywa katika town halls ambazo hufanywa mtandaoni. Michakato na zana za ufuatiliaji hii ni kazi inayoendelea - unaweza kuwa sehemu ya suluhisho! Hadi dola 80,000 inapatikana kwa timu katika hazina maalum ya7.

6) Washauri wa Jamii

Mapendekezo mapya ya kila awamu zinawekwa kwenye https://cardano.ideascale.com/,, ambapo wanajamii wanaweza kutuma maoni na maswali. Timu za pendekezo basi zina nafasi ya kujibu na kuboresha mapendekezo yao. Kisha, kabla ya kupiga kura, mapendekezo yanapitiwa na washauri wa jamii (CAS). Washauri wa Jamii hutathmini kila pendekezo la kuzingatia katika changamoto, uwezekano wakutekelezwa na kukaguliwa. Hii husaidia kuongeza ubora wa mapendekezo ambayo hatimaye huwasilishwa ili yaweze kupigiwa kura. Katika hazina maalum ya 7, $ 320,000 USD inabajetiwa kwa ajili ya CAS.

7) Washauri wa Jamii wa zamani.

Katika huduma zaidi ya uhakika wa ubora, tathmini kutoka kwa washauri wa jamii wenyewe wametathminiwa na watu ambao walikuwa washauri wa jamii katika hazina maalum ya awali. Washauri wa jamii wa zamani ndio huangalia waangalizi . $ 80,000 USD itatolewa kwa sababu ya bidii yao katika hazina maalum y a7

8) Wapigaji kura.

Hatimaye, kiini cha mchakato mzima, ni fursa kwa kila mmiliki ADA kuwa na maoni. Mapendekezo yanajitokeza kwenye kura huwasilishwa katika programu ya apple na android, ambapo wamiliki wa ADA hupiga kura ya ndiyo au la kwa kila pendekezo. $1,040,000 itasambazwa kwa kila mpigaji kura wa hazina maalum ya 7.

Hazina maalum ya 7 itaendelea kwa wiki 10; mapendekezo yanayoshinda yatatangazwa katika wiki ya 11 au 12. Tunatumahi utaingia na kupata jukumu ambalo litakufurahisha. Chukua nafasi yako katika historia - kama mwanzilishi katika jaribio la kuchochea kiwango cha juu zaidi cha ushirikiano wa binadamu! Ili kuanza, nenda kwenye cardano.ideascale.com, fungua akaunti, na uje kwenye mkutano wa Town Hall unaofuata. Tazama viungo hapa chini ili kupata taarifa za hivi punde.

Related Links

  • Relevant Link 1 link
  • Register to learn about Proposals and submit a business idea ideascale
  • Project Catalyst - Zoom Weekly Town Hall Reoccurring Zoom Link
  • IOG Launch Announcement blog
  • Project Catalyst Challenge and Proposal Guide How to write Challenge and Proposal Guide
  • Places to connect people and ideas Catalyst Swarm Events Calendar
  • Fund8 Launch Guide pdf
  • Project Catalyst – the first winning proposals iog blog
  • Announcements only telegram
  • Go deeper with Catalyst Discord discord

Get more articles like this in your inbox

How will you participate in fund 7? What questions do you have?

Or leave comment
Share

No comments yet…

avatar
You can use Markdown
close

Playlist

  • EP2: epoch_length

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 3 se. 24
    Darlington Kofa
  • EP1: 'd' parameter

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 4 se. 3
    Darlington Kofa
  • EP3: key_deposit

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 3 se. 48
    Darlington Kofa
  • EP4: epoch_no

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 2 se. 16
    Darlington Kofa
  • EP5: max_block_size

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 3 se. 14
    Darlington Kofa
  • EP6: pool_deposit

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 3 se. 19
    Darlington Kofa
  • EP7: max_tx_size

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 4 se. 59
    Darlington Kofa
0:00
/
~0:00