Nothing came up for

"Video ya Whiteboard" Sehemu ya 1: Mageuzi ya cryptocurrency

whiteboard-video-part-1-the-evolution-of-cryptocurrency-hero-image

Mfululizo huu wa makala ni mukhtasari wa maandishi ya video maarufu ya "Whiteboard" ya Charles Hoskinson, ambayo ilitolewa mwaka wa 2017. Katika video hiyo, aliweka msingi na maono ya Cardano. Kwa watu wengi, video hiyo ni mahali pa egemeo katika ufahamu wao na msisimko kuhusu Cardano, na kufahamu umuhimu wake. Inajulikana kuwa video ilianza mwaka wa 2017 - ilhali mawazo haya bado yanatumika na jamii ya jukwaa la Cardano. Makala haya ni maneno na mawazo ya charles, yaliyopangwa kwa uwazi na usomaji katika fomu iliyoandikwa.

Ili kuelewa cardano, kwanza unapaswa kuelewa chimbuko lake. Basi, hebu tuzungumzie juu ya kizazi cha kwanza cha cryptocurrency.

Kizazi 1

Hivyo, kizazi cha kwanza ni bitcoin.

Tatizo ambalo Bitcoin lilikuwa linajaribu kutatua ni, "Je, tunaweza kuunda fedha iliyogatuliwa?"

Je! Tunaweza kuunda tokeni inayoishi kwenye blockchain kwa mfumo uliogatuliwa na ambayo inadumishwa na watu duniani kote? Je! tokeni hiyo inaweza kuwa adimu na inayoweza kuuzwa? Inaweza kuwa kama vile wakati "Zawadi" na "Juma" wanataka kutuma thamani kwa kila mmoja, kunaweza kuwa na utaratibu wa kufanya hivyo ambao hauhitaji kuwepo kwa mhusika wa tatu aliyeaminika [kama benki Au huduma nyingine ya kifedha ya kati]?

Sasa hii ilikuwa wazo la kweli na la kuvutia. Ilikuwa na mizizi ya zamani sana kuanzia miaka ya 1980 na zaidi, lakini Bitcoin ilikuwa ya kwanza kuleta hii yote pamoja. Ilikuwa jaribio la mafanikio sana! Baada ya miaka michache tu, Bitcoin haikukusanya maelfu ya watumiaji tu bali pia ilianza kuwa na thamani ya pesa halisi. Tokeni zilikwenda chini ya senti hadi $ 1.00, hatimaye $ 100. Katika kipindi hicho, tuliona mvuto mkubwa wa watu wakisema "Hii ni ya kuvutia sana." Hata hivyo, tatizo ni kuwa shughuli kati ya Zawadi na Juma ina zaidi ya tendo la kuhamisha fedha zinazohusiana nayo. Kuna hadithi nyuma ya shughuli hiyo; Kuna sheria na masharti. Kwa mfano, je Zawadi akisema "Juma nitakupa pesa ikiwa utakata nyasi yangu." Huu ni mkataba - hadithi. Kizazi cha kwanza cha teknolojia ya blockchain haikufaa sana kwa hili. Kila wakati mtu alitaka kufanya mabadiliko ya jinsi inavyofanya kazi, wangepaswa kujenga cryptocurrency tofauti, au kusakinisha itifaki ngumu ya kuwekelea kama vile mastercoin au color coin.

Kizazi cha 2.

Hapo awali mwaka wa 2014, Vitalik Buterin, Charles Hoskinson, na wengine wengi walikusanyika na kuzindua blockchain ya kwanza ya kizazi cha pili: ethereum. Ethereum ni kama vile wakati JavaScript ilikuja kwenye kivinjari cha wavuti: tulitoka kwa kurasa rahisi na zilizo tuli na ambazo hazikuwa za kutisha kimatumizi, hadi kwa kurasa ambazo zimeweza kupangwa kikamilifu. Mabadiliko hayo yaliwezesha watu kuunda Facebook, Google, Gmail … uzoefu ambao tumekuja kujua na kupenda.

Vivyo hivyo, ethereum ilileta lugha ya programu kwa blockchain. Lugha hii ya programu iliruhusu mikataba bora (smart contracts) kuandikwa - yaani, mikataba iliyoboreshwa. Kwa hivyo, wakati Zawadi anatuma thamani kwa Juma, hizo sheria na masharti zinaweza pachikwa ndani ya shughuli hiyo. Inaweza kuboreshwa kwa mahitaji yake maalum. Dhana hii, kama Bitcoin, pia ilishika kasi. Sasa ethereum ni miongoni mwa cryptocurrencies kubwa na ina jumuiya kubwa ya wasanidi. Hata hivyo, sasa kama hapo awali, tunaanza kuingia katika eneo jipya.

Kizazi cha 3

Tunaingia katika kizazi cha tatu. Masuala kadhaa muhimu yanaendesha mageuzi haya:

  • Ethereum haiwezi kupungua kwa mamilioni au mabilioni ya watumiaji.
  • Ethereum haina uzoefu wa wasanidi wazuri waliobobea.
  • Ethereum na cryptocurrencies zote zina uzoefu mbaya wa utawala. Kila wakati kuna kutofautiana kuu, badala ya kutafuta njia ya kutatua, tunaishia na kugawanyika katika mazingira, kama ethereum na ethereum classic, au bitcoin na bitcoin fedha.
  • Kuna matatizo makubwa ya uendelevu. Kwa hiyo, baada ya fedha za ICO [Initial Coin Offering], na za mradi mtaji kuisha- kwa kweli nani atalipa kujenga mazingira? Haya ni maswali makubwa ya wazi!

Kwa hivyo, kizazi cha tatu kinahusisha mada tatu: uwezo wa kuboreshwa, muingiliano, na uendelevu. Mradi wa Cardano ni falsafa na maono ya jinsi ya kutatua kila moja ya makundi haya. Wazo hili ni la kurithi sifa bora na masomo kutoka kwa kizazi cha 1 na 2, lakini pia kuongeza dhana na teknolojia mpya. Zaidi ya hayo, mradi huu umejengwa na kanuni bora zaidi. Yaani, sayansi inayoongoza suluhisho la matatizo haya hupitia hakiki ya rika. Tunakwenda kwenye mikutano, tunandika makala ya kisayansi, tunashirikisha vyuo vikuu. Kwa uhandisi wote, tuna lengo la hatimaye kuitekeleza kama "msimbo wa uhakika wa juu". Hii inamaanisha aina hiyo ya mbinu ambayo itaendana na ile ya injini ya ndege - ambapo kushindwa kwa mfumo husababisha kifo cha binadamu - tunaweza kutumia mbinu hizo kwa itifaki zetu, uhandisi na maendeleo, ndiposa tuwe na imani kubwa sana katika ubora wa kanuni; Hii inamaanisha kuepuka matukio kama yale ya udukuzi wa Dao parity, na aina nyingine za maovu ya kiteknolojia.

Katika awamu zijazo, tutasoma maelezo ya kina ya Charles kuhusu masuluhisho ya uwezo wa kuboreshwa, ushirikiano na uendelevu

Get more articles like this in your inbox

Maoni ya haraka: Je, kumekuwepo na wakati ambao umejifunza jambo jipya kuhusu vizazi vya cryptocurrency?

Leave a comment
Share

Related Insights

Wallets on Cardano and Ethereum

Blockchain ni nini? - Safari ya mgeni mmoja

Project Catalyst Funds - 5-9

The Nervous Man’s Guide to Becoming a P.A.

No comments yet…

avatar
You can use Markdown

Join our pool!

Unmatched Support
We provide phone and email support for all of our delegates. We understand that many of our community members are not tech or crypto nerds. You expect the same level of service and support you get from Reggie down at the bank or Saiid, your nephew or friend at the office that won't stop talking about Bitcoin. We host weekly meetups (currently online due to Covid). Visit our connect page for all the ways you can reach us.
Best in class servers
Our servers are run and managed by professionals whose only job is to manage and run servers 24/7 365/6 days a year. We run our Cardano nodes on the same servers powering other services you've come to rely on everyday, like Google and Pokemon Go. What this means for you is that our servers are always online and available to process transactions, earning you and the causes we support the optimal amount of $$$$. Visit our pool page for more technical details.
4% for community development and investment
Of all the rewards that come in, we keep 4% annually. All 4% goes towards charities you pick, paying LIDO nation community members like yourself to write code and content for the site, and grants for local community educational projects. See our financials page for full records of our spending, more details, and breakdowns.
An Amazing Community
When you delegate and join LIDO Nation, you get to participate in creating a space for people to interact, meet, learn, and teach each other. You get to be part of the engine that works to make every voice heard with equal importance. LIDO Nation is an idea. Delegate, take it and lets make something great!