Video ya Whiteboard Sehemu ya 2: Uwezo wa kuboreshwa (scalability)

Mfululizo huu wa makala ni mukhtasari wa maandishi ya video maarufu ya "Whiteboard" ya Charles Hoskinson, iliyotolewa mwaka wa 2017. Katika video hiyo, aliweka msingi na maono ya Cardano. Kwa watu wengi, video hiyo ni mahala pa egemeo katika ufahamu wao na msisimko kuhusu Cardano,na nini inaifanya iwe tofauti katika nafasi ya blockchain. Inajulikana kuwa video hiyo ilianza mwaka wa 2017 , ilihali mawazo haya bado yanatumika kuimarisha jamii ya Cardano hii leo. Makala haya ni maneno na mawazo ya Charles, yaliyopangwa kwa uwazi na usomaji katika fomu iliyoandikwa.

Katika Sehemu ya 1, tulijifunza kwamba kizazi cha 3 cha cryptocurrency kinahusu jinsi ya kutatua matatizo ya uwezo wa kuboreshwa (scalability), uingiliano (interoperability), na uendelevu. Katika sehemu hii ya pili iliyotolewa kwenye video ya Whiteboard, Charles anaelezea suluhisho la Cardano kwa uwezo wa kuboreshwa (scalability):

Uwezo wa kuboreshwa (scalability) ina maana nyingi, lakini kutokana na mtazamo wa cryptocurrency, unaweza kuifikiria kwa njia tatu:

1) Shughuli kwa sekunde ( Transactions Per Second, TPS)

Mara nyingi utasikia watu wakisema, “Bitcoin pia ina shughuli 7 kwa sekunde” au “etherenum ina shughuli 10 au 20 kwa sekunde”. Hii ni wazo tu la shughuli ngapi ambazo zinaweza chakatwa kwenye blockchain ndani ya kipindi cha muda. [Maelezo ya Mhariri: Cardano imefanikiwa kufanya ~ 250 TPS, na mipango ya kua na idadi kubwa zaidi!]

Kutambulisha Ouroboros.

Ili kukabiliana na TPS, tulianzisha whitepaper iliyopitiwa na rika kwa itifaki yetu ya uthibitisho wa salama inayoitwa Ouroboros. Ouroboros ni moja wapo ya itifaki ya makubaliano ya ufanisi zaidi katika nafasi ya cryptocurrency, na ni ya kwanza kuthibitishwa salama kwa njia kali ya kriptografia. Jambo la kushangaza kuhusu Ouroboros ni kuwa imetengenezwa kwa njia ya kawaida na udhibitisho wa siku zijazo katika DNA yake

Hivi ndivyo Ouroboros inavyofanya kazi:

Kwanza, inagawanya ulimwengu katika epochs [Kwa sasa, epoch ya cardano ni siku 5] Katika epoch, usambazaji wa tokeni inaangaziwa, na kutokea kwa chanzo cha namba nasibu, hufanya uchaguzi ili kuchagua “viongozi wa slot”. Viongozi wa Slot hufanya kazi sawa na mchimbaji wa bitcoin wakati “wanaposhinda bloki.” Tofauti ni kwamba haihitaji rasilimali nyingi za hesabu ambazo Bitcoin inahitaji. Kwa hiyo, mfumo huu ni wa bei nafuu sana kuendeleza, ingawa tuna dhamana sawa ya usalama. haya ni maendeleo makubwa

Hizi ni baadhi ya faida za Itifaki ya Ouroboros:

  • Viongozi wa Slot sio lazima wadumishe bloki moja na mtandao moja. Wanaweza kudumisha bloki zingine na mitandao mingine kwa sababu gharama ya kujenga bloki ni ya chini sana. Kwa kweli sasa ni rahisi kuzungumza kuhusu makubaliano juu ya blockchains mbalimbali badala ya mtandao moja.
  • Zaidi ya hayo, epoch inaeza kuendeshwa kwa usambamba; Badala ya kuendeleza epoch moja baada ya nyingine, tutaweza kuendeleza mfumo kwa kutumia Ouroboros ambapo epoch zinaendelezwa kwa usambamba, na shughuli zinagawanyika ipasavyo. Hii ina maana kua unapopata watumiaji zaidi, na watumiaji wako wanapata uwezo zaidi, viongozi hawa wa slot wataweza kudumisha aina zaidi za blockchains na pia kuendeleza usindikaji wa shughuli za blockchains kwa usambamba. Haya ni maendeleo makubwa!
  • Ouroboros ina viwango vya juu vya usalama kulingana na misingi yake ya kinadharia pamoja na utekelezaji wake. Tunapoendeleza uwezo mpya wa itifaki, uwezo huu pia utakuwa salama. Hii ni kinyume na mifumo mingine, ambapo mtu anahitaji kuthibitisha mambo haya kwa msingi wa moja kwa moja, na wakati mwingine kufanya marekebisho makubwa ili mfumo uwe salama.
  • Tunatarajia Ouroboros kuwa na uwezo wa kutopimika wakati wowote ifikapo mwaka wa 2018. Wakati kiongozi wa slot anatia saini , watakuwa wakitumia mpango wa saini yenye uwezo wa kutopimika. Kwa hili, tunapata udhibitisho wa siku zijazo katika mfumo. [Maelezo ya Mhariri: Kompyuta za Quantum ni kompyuta zenye nguvu ya siku zijazo, ambazo tunafikiri zinaweza kuvunja funguo za kriptografia. Kama ilivyo leo, tishio hili ni la dhahania, lakini kuipangia kwa sasa ni jambo muhimu la siku za usoni!]

Vipengele hivi vinahusu maswali ya uwezo wa kuboreshwa (scalability)

“Ni vipi Tutatengeneza njia ya kudumisha mtandao ambao hauna gharama ya $ 300,000 / saa, ambayo ni gharama ya bitcoin kwa sasa?” Maelezo ya Mhariri: Charles Hoskinson alitoa majadiliano haya mwaka wa 2017. Gharama ya Nishati ya Bitcoin imezidi mara nne tangu wakati huo. Mahitaji ya nishati ya kuendeleza Bitcoin yanazidi ile ya nchi nzima ya Argentina.

“Tutajengaje mfumo ambao utatuwezesha kwenda sambamba na kudumisha mitandao mingine kwa wakati mmoja?”

Kujibu maswali haya ni kipaumbele cha Ouroboros.

2) Kipimo data

Shughuli kwa sekunde ni muhimu, lakini sio kitu pekee tunachohitaji kuwa na wasiwasi nao. Shughuli hubeba data, na unapopata shughuli zaidi unahitaji rasilimali zaidi za mtandao. Hili ni wazo la kipimo data. Kwa mfumo kuwa bora (scale) - ikiwa itakua kwa mamilioni na mabilioni ya watumiaji - mfumo huo unaweza kuhitaji mamia ya gigabytes kwa sekunde ya kipimo data ili kupea kiguzo data zote zinazopitia mfumo huo. Aina hii ya kiasi ni ya kawaida katika ulimwengu wa biashara, lakini sio katika ulimwengu wa rika hadi rika.

Kutambulisha Rina.

Muungano wetu unapozidi kuongezeka kutoka kwa shughuli mia chache kwa sekunde, hadi kwa mamia ya maelfu ya shughuli kwa sekunde, hatuwezi kudumisha topolojia ya mtandao sambamba. Kwa maneno mengine, hatuwezi kuwa na hali ambapo kila nodi inapaswa kuhusisha kila ujumbe. Tunapokua, kutakuwa na nodi ambazo hazina uwezo huo. Kwa hiyo, tunaangalia aina mpya ya teknolojia inayoitwa Rina. Hii kwa urefu ni Recursive Internetwork Architecture. RINA ni njia mpya ya kuunda mtandao kwa kutumia kanuni janja za uhandisi - hasa zilizozalishwa na John Day kutoka kwa Chuo Kikuu cha Boston. Lengo la RINA ni kujenga mtandao tofauti ambao hutupa faragha, uwazi, na ubora ( scalability). RINA ni hatua kuu mbele ambayo itatupa njia ya kuunganisha na kusanidi Cardano inapoendelea kukua.

3) Kiwango cha data.

Blockchains kuhifadhi vitu - kwa matumaini, milele! Kila wakati unaweka shughuli ndani, inaenda kwenye logi. Kwa hiyo, kama una shughuli nyingi, unahitaji data zaidi na zaidi. Kwa sababu hiyo, blockchains itaongezeka kutoka megabytes hadi gigabytes hadi terabytes hadi petabytes …. uwezekano hata exabytes. Hii ni sawa katika ulimwengu wa biashara kubwa [na vituo vya data vya kati], lakini tunapozungumzia juu ya mfumo ulioigwa ambao mfano wa usalama unategemea kila nodi kuwa na nakala ya blockchain?Kiasi hicho cha data haipatikani kwa vifaa vya watumiaji [yaani kompyuta za nyumbani za kawaida].

Cardano inajaribu kutatua matatizo haya kwa njia ya kifahari sana. Katika Cardano, tunapoongeza watu kwenye mtandao, kwa kawaida tunapata shughuli nyingi kwa sekunde. Sisi pia kwa kawaida hupata rasilimali zaidi ya mtandao. Hatimaye, tutapata hifadhi zaidi ya data. Yote bila kuacha mfano wetu wa usalama!

Kutambulisha kupogoa, kugawanya, na minyororo ya upande

Ili kukabiliana na tatizo la kuoza data, kile tunachopaswa kutambua ni kwamba si kila mtu anahitaji data zote. Shughuli ambazo Zawadi anatuma kwa Juma sio muhimu kwa Waridi na Baraka. Shughuli hizo ni muhimu tu kwa muktadha wa kuwa watu hawa wanaweza kujua tokeni wanazopokea ni halali na sahihi. Mbinu zingine za kushughulikia suala hili ni:

  1. Kupogoa: kuzuia kile ambacho watu wengine wanaweza kuona, kwa msingi wa kesi-kwa-kesi.
  2. Kugawanyika: mtumiaji anaweza kuwa hana nakala kamili ya blockchain, lakini badala yake ana kipande tu.
  3. Minyororo ya upande: Unda uwakilishi wa msisitizo wa blockchain [kwenye mlolongo wa pili], na utafsiri shughuli kati ya minyororo

Rigor ya kitaaluma - Kitofautishi cha Cardano

Mojawapo ya mambo muhimu zaidi wakati wa kuendeleza kiriptografia mpya ni kuhakikisha kuwa imeendelezwa na kukaguliwa na rika kwa njia ya ukali sana. Ouroboros ilikubaliwa katika “Crypto 17” [mkutano wa 37 wa kila mwaka wa kriptografia ya kitaaluma], ambapo timu yetu iliwasilisha. Matoleo yajayo ya itifaki yanaendelea kupitia hakiki ya rika kali,na kutupa uhakika wa juu kwamba muundo wa dhana wa mfumo ni sahihi. Sisi pia tunaunda vipimo rasmi vya ouroboros tukitumia “side-calculus “ - lugha rasmi ambayo inaeleweka na mashine. Hatimaye, tutaweza kuunganisha kwenye msimbo wa Haskell katika repo yetu ya GitHub na kwa kweli kuonyesha kwamba tumeweka itifaki kikamilifu. Hiki ni kiwango ambacho hakipo katika nafasi ya blockchain, na tunafurahi sana kuwa wa kwanza kufanya hivyo.

Lengo la mradi wa Cardano ni kusoma maswali yote kwa njia kali na kuja na usanifu mpya wa blockchain. Ufumbuzi lazima uwawezeshe watu kuwa na kiasi kidogo cha data, wakati bado wanapata kiwango sawa cha uhakika kwamba shughuli ni sahihi. Jambo moja la bahati ni kwamba wakati mahitaji ya TPS na bandwidth yanakuwa kwa haraka, hifadhi ya data bado ni ya bei nafuu na inapatikana. Kwa hiyo tunaamini kuwa upande wa uwezo wa kuboreshwa kwa data (data scaling) ya cardano utakuwa ni kitu ambacho hatutakuwa na haraka sana ya kutatua. Utafiti juu ya maswali haya yanafanyika katika Chuo Kikuu cha Edinburgh; Tunaamini tutakuwa na suluhisho la jumla kwa tatizo hili mwishoni mwa mwaka wa 2019.

Kwa hiyo hii ndiyo nguzo ya kwanza ya cryptocurrency ya kizazi cha tatu: uwezo wa kuboreshwa (scalability)

Get more articles like this in your inbox

What questions do you have about Scalability?

Or leave comment
Share

No comments yet…

avatar
You can use Markdown
close

Playlist

  • EP2: epoch_length

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 3 se. 24
    Darlington Kofa
  • EP1: 'd' parameter

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 4 se. 3
    Darlington Kofa
  • EP3: key_deposit

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 3 se. 48
    Darlington Kofa
  • EP4: epoch_no

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 2 se. 16
    Darlington Kofa
  • EP5: max_block_size

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 3 se. 14
    Darlington Kofa
  • EP6: pool_deposit

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 3 se. 19
    Darlington Kofa
  • EP7: max_tx_size

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 4 se. 59
    Darlington Kofa
0:00
/
~0:00