Video ya whiteboard sehemu ya 3: Uingiliano

Mfululizo huu wa makala ni mukhtasari wa maandishi ya "Whiteboard" maarufu ya Charles Hoskinson, ambayo ilitolewa mwaka 2017. Katika hiyo, aliweka msingi na maono kwa Cardano. Kwa watu wengi, video ni "pivot uhakika" katika ufahamu wao na msisimko kuhusu Cardano, na nini inafanya kuwa tofauti katika nafasi ya blockchain. Inajulikana kuwa video imeanza mwaka 2017 - maisha katika nafasi ya blockchain - lakini mawazo haya bado yanaendesha gari na kuimarisha jamii ya Cardano leo. Nyaraka hizi ni maneno ya Charles na mawazo, yaliyopangwa kwa uwazi na usomaji katika fomu iliyoandikwa.

Katika Sehemu ya 1, tulijifunza kwamba kizazi cha 3 cha cryptocurrency kinahusu kutatua matatizo ya usawa, uingiliano, na uendelevu. Hii ni sehemu ya tatu kutoka kwenye video ya Whiteboard, ambapo Charles anaelezea falsafa ya Cardano ya uingiliano:

Hakutakuwa na sarafu moja ya blockchain itakayo tawala zote. Kutakuwa na aina nyingi ya mitandao kama vile ethereum, bitcoin na ripple. Zaidi ya hayo, kutakuwa na mifumo ya urithi kama benki za kitamaduni, zinazoendeshwa kwa itifaki za jadi, na mitandao ya makazi ya zamani kama ACH na kadhalika. Mifumo hii yote hufanya kazi kwa njia zao maalum na ina na mantiki na sheria zao za biashara. Kwa sasa, ni vigumu sana kwa ethereum na Bitcoin kuelewana. Hii ni kweli zaidi kwa mitandao ya benki za jadi ambazo zina mahitaji ya ziada ya metadata na maelezo kwa ajili ya shughuli zinazofanywa. Uingiliano ni wazo la kuruhusu mitandao kuingiliana- kwa urahisi na usalama.

Shida ni kwamba wakati hatuna njia moja ya mifumo kuwasiliana, thamani hugawanyika sana. Bila kujali jinsi mfumo wowote wa ikolojia huu unaweza kuwa umegatuliwa, mfumo kuu ndio unaodhibiti uhamishaji wa thamani kati ya mifumo. Hivi sasa tunaziona kama ubadilishanaji [kama Coinbase, nk]. Kwa bahati mbaya, ubadilishanaji huu ni dhaifu sana:

  • Zinaweza kudukuliwa.
  • Ziko chini ya kanuni kali.
  • Mara kwa mara, hufungwa kwa sababu ya sera za udhibiti.

Kundi ndogo kudhibiti kama mtu anaweza kubadilisha thamani kutoka kwa mfumo mmoja hadi mwingine sio hali nzuri. Hasa kwa mfumo wa ikolojia ulio gatuliwa na usio na ruhusa, yaani mtu yeyote anaweza ifikia. Zaidi ya hayo, wakati watu wanafanya biashara - ikiwa biashara hizi zinadhibitiwa - kwa kawaida zinapaswa kuingiliana na ulimwengu wa kifedha wa jadi. Kwa mfano, hebu tuseme kwamba wewe ni kampuni ya cryptocurrency na unatoa tokeni.Kwa kutumia tokeni hiyo, unakusanya mamilioni ya dola kwa kuwauzia watu wengi. Kisha, kama kampuni halisi iliyo na akaunti ya benki katika mamlaka ya kisheria, unaweka mamilioni ya dola kwenye akaunti yako ya benki.

Kwa vile benki ni shirika linalodhibitiwa, swali la kwanza watakalouliza ni “ulipata wapi mamilioni haya ya dola?”

Utasema “niliwauzia watu wengi tokeni na nikapata rundo la pesa.”

Nayo benki itakuuliza, “wateja wako ni akina nani?”

Na utajibu, “Watu kwenye Mtandao!”

Na kwa bahati mbaya jibu hilo si nzuri. Kwa hivyo Benki, kama taasisi ya biashara inayodhibitiwa, inabidi iandikishe ripoti ya shughuli inayotiliwa shaka. Wanapaswa kukabiliana na watu katika Idara ya Hazina au labda Umoja wa Ulaya (European Union) na kadhalika, na mashirika haya yanahisi kuwa hili ni pendekezo hatari sana. Kwa bahati mbaya, huu ndio ukweli tunaoishi nao - tuna viungo tete katika cryptocurrency na vilevile katika mfumo wa fedha wa urithi. Hakuna njia ya kuongeza shughuli kwa njia ya asili. Kufanya biashara na ulimwengu wa urithi kunahitaji metadata, maelezo, na kuzingatia shughuli zinazofanywa, [ambayo mitandao ya blockchain haitoi.] Kwa hivyo, mtu yeyote anayefanya biashara katika nafasi hii moja kwa moja inakua biashara hatari. Hii ni hali ya bahati mbaya.

Uingiliano - mtandao wa Blockchains.

Wazo moja la kizazi cha tatu cha cryptocurrency ni moja ambayo ina uwezo wa kueleweka na kusimamia cryptocurrency zingine. Cryptocurrency ambayo inaweza kuona shughuli ya ethereum na kuthibitisha kuwa ni halali. Kwa mfano, kama Zawadi anasema ana ether, na anaituma kwa Juma, cryptocurrency ya kizazi cha 3 inapaswa kuwa na uwezo wa kujua kwamba hiyo ni shughuli halali. Kwa hiyo, uhamisho wa cross-chain ni wa kuaminika, na unaweza kufanyika bila kuhitaji mhusika wa tatu wa kuaminika. Hili ndilo jambo moja muhimu zaidi: tunataka kuunda mtandao wa blockchains - mtandao wa thamani - unaozunguka kwa urahisi kama Bitcoin au Ether - lakini tunataka kuwa na uwezo wa kusongesha cross-chain.

Hatua ya kwanza ya kuunda ulimwengu huu ni kuwa na dhana fulani ya side chains. Hili sio wazo geni: atomic cross chain swaps na side chains zimekuwepo kwa muda mrefu. zilipendekezwa mwaka wa 2012, au labda mapema zaidi. Wazo la msingi ni kwamba kuna njia fulani ya kupanga habari kutoka kwa chain moja hadi nyingine ili kwamba shughuli inapotumwa, muundo huo ulioshinikizwa wa habari unakupa uwezo wa kujua ikiwa shughuli hiyo ni halali. Kwa maneno mengine, mtu anayekutumia ana thamani hiyo na kwamba haijatumiwa mara mbili. Ni dhana muhimu sana.

Jambo la pili ni kwamba unapaswa kuwa na uwezo wa kufanya hivyo kwa njia iliyoshinikizwa. Kuna zaidi ya cryptocurrency elfu moja zinazotumika, na zinazaidi kuwa kubwa. Kwa hivyo huwezi kusema, “ njia pekee ya kuelewa mfumo mwingine ni kuwa na nakala ya blockchain nzima ya mfumo mwingine.“ Suluhisho hili halina uwezo wa kuboreshwa. Badala yake, unapaswa kuwa na uwezo wa kuangalia mifumo hii kwa njia iliyoshinikizwa.

Cardano imeanza kazi kwenye side chains. hivi majuzi tulichapisha karatasi ambayo ina mkabala wa jinsi ya kutoa udhibitisho katika ulimwengu wa udhibitisho wa kazi, unaoitwa, “Non- interactive proof of proof-of-work.“Tuna matumaini kwamba mbinu hii inaweza pia kutumiwa katika uwekezaji wa hisa[kama katika cardano].

Cryptocurrencies zingine ziko hapa kukaa! Kwa hivyo tunatarajia kwamba vitu hivi viwili - side chains na mgandamizo - pamoja na uhandisi fulani, inapaswa kutuwezesha kuwa na ufahamu wa kina wa kile kinachoendelea miongoni mwa na kati ya cryptocurrency nyingine.

Uingiliano - ulimwengu wa urithi.

Hata kama tunaweza kuunda utopia ambapo blockchains zote zinaweza kuzungumza na kila mmoja, tatizo ni kwamba ulimwengu wa cryptocurrency bado haupatani na ulimwengu wa biashara na benki. Kuna mambo matatu ya msingi katika pengo hili:

1) metadata.

Metadata ni hadithi nyuma ya shughuli. Sio kwamba umetumia dola hamsini ambazo ni muhimu. Kitu muhimu ni:

  • Uliitumia wapi?
  • uliitumia kufanya nini?
  • ulimpa nani?

Aina hizi za metadata hazijatolewa vyema katika nafasi ya cryptocurrency, lakini ni jambo la kawaida katika ulimwengu wa kifedha wa urithi.

Kuna kiasi kikubwa cha thamani katika shughuli ya metadata. Kwa mfano, shughuli ya metadata inaruhusu shughuli ziingizwe katika uongozi ulio hatarika. Ikiwa kuna uhamisho wa waya kati ya benki mbili za Afrika zilizoko Nairobi zinazohusisha makampuni makubwa - hili ni jambo la kawaida sana na hutokea wakati wote. [Hii haiwezi kuibua tuhuma yoyote.] Sasa hebu fikiria kwamba kuna uhamisho wa waya kutoka kampuni ndogo ya Africa hadi taasisi ndogo ya Kirusi, ambayo inakwenda Iran, na kisha kuenda America. Hii ni hali tofauti kabisa. Hata kama kiasi cha fedha ni sawa, idadi ya uhamisho, watu ambao wameigusa, asili ya mashirika, kwa muda gani wamekuwa wakifanya biashara …. Hii yote ni metadata. [Kwa hivyo, metadata hiyo inaweza kutumika kualika umakini zaidi wa udhibiti kwa shughuli hii.]

Tatizo ni kwamba metadata ni ya kibinafsi sana. Ni ya faragha sana. Kwa hivyo tuna shida nayo katika nafasi ya cryptocurrency kwa sababu shughuli za blockchain ni za kudumu na za uwazi.Ikiwa tutaunganisha metadata kwa shughuli kwenye blockchain, tunaweza kufichua taarifa ya nyeti kwa umma. Kwa hivyo mojawapo wa malengo ya mradi wa Cardano ni kutambua ni wapi, lini, na jinsi gani tunaweza kuweka metadata kwenye blockchain. ** Tunataka manufaa ya ukaguzi, kutobadilika na uwezo, na wakati wa kupiga kura kwenye blockchain, huku tukitambua umuhimu wa Metadata kwa baadhi ya matukio **. Hizi zinahitaji kushughulikiwa kwa njia ya kuwajibika - labda kwa usimbaji fiche, au labda kwa mpango maalum unaoruhusu watu fulani kuiona, ilhali wengine hawawezi.

2) Sifa

Sifa ni kuhusu utambulisho - kutaja watendaji wanaohusika katika shughuli. Ni juu ya kujua mahali ambapo fedha zimetoka, na ni wapi zinaenda. Ni sehemu ndogo ya metadata, lakini ni muhimu sana na inastahili kuzingatiwa . Ni muhimu sana kwamba Cardano imeamua kujenga njia ya kuongeza sifa kwa shughuli, ikiwa inatakwa, kwa njia iliyoratibiwa na rahisi. Ugumu wa kufanya hivi ni kuanzisha mtandao wa uaminifu, au aina fulani ya daraja la utambulisho.

Mojawapo ya sababu zinazofanya mtandao kutumia nywila nyingi na majina mengi ya watumiaji ni kwa sababu hatuna njia nzuri ya kuwatambua watu kwenye mtandao. Ingekuwa vyema ikiwa kila mtu angekuwa na ufunguo wa umma, na ikiwa kungekuwa na njia rahisi ya kusambaza na kuthibitisha funguo hizi. Hili lilikuwa mojawapo ya malengo ya mradi wa PGP, lakini haikufanikiwa. Kwa hiyo, tunachoshughulikia kwenye mtandao ni tatizo la dystopia ambapo kila mtu ana jina la mtumiaji na nywila. Hizi ni kawaida huwa ni rahisi kubahatisha, rahisi kudukuliwa, na kwa kawaida hutumiwa miongoni mwa tovuti nyingi tofauti. Hii yote husababisha matatizo mengi.

Kwetu, jambo la kipekee katika blockchain ni kwamba cryptocurrencies ni vizalishaji vya kryptograhia vya siri. Tofauti na mtandao wa sasa, Cryptocurrency inatupa uwezo wa kupanga, kusimamia, na kuhifadhi funguo za kipekee na kuendeleza mtandao wa uaminifu. Kwa hivyo, lengo moja la mradi wa Cardano ni kuchunguza jinsi tunavyoweza kuimarisha mambo haya. Hivi sasa tunazitumia kwa ajili ya kuhifadhi na kuweka kiwango cha pesa fulani kando kwa matumizi ya baadaye, lakini pia zinaweza kutumika kututambulisha, lini na jinsi tunavyotaka. Matumaini ni kwamba hii inaweza kutumika wakati watu wanahitaji kutoa sifa za shughuli. Kwa mfano, wanapotuma thamani kwa au kutoka kwa shughuli za kubadilishana, wanaweza kufanya hivyo kwa njia nzuri na rahisi.

3) Uzingatiaji

Uzingatiaji ni ujenzi wa kanuni na sheria mbalimbali zinazotawala shughuli za kifedha. Kwa mfano:

+ KYC:Know Your Customer (Jua mteja wako) + Aml: Anti Money Laundering + ATF: Anti Terrorist Financing (Ufadhili wa kupambana na ugaidi

Haya yote yanatokana na swali moja la msingi: shughuli imefanyika. Je, ni halali?

Hili ni jambo ambalo halizingatiwi sana katika ulimwengu wa crypto. Hata hivyo, ni muhimu sana kwa taasisi za fedha za jadi. Iwe ni kubadilishana, benki, au biashara yoyote ya huduma ya fedha, kuna kanuni na viwango vya juu sana vya kimataifa.

Kwa hivyo, kuhusiana na hili, tumaini letu ni kwamba Cardano inaweza kupata usawa. Hatua mbili za kwanza ni kuunda kitambulisho cha kriptographia kilicho sambazwa na kutoa metadata. Kisha, hizi mbili zinaweza kuwekwa pamoja kwa njia ya ubunifu, kwa msingi wa hairi na kwa njia ya moja kwa moja. Kisha, wakati mtu katika ulimwengu wa Crypto anataka kufanya biashara katika ulimwengu wa urithi, wana uwezo wa kuongezeka shughuli kutoka kwa shughuli ya kawaida ya cryptocurrency hadi ule ambao benki inaweza kutambua na kuridhika nayo. Kwa mfano, chukua hali ambayo tulitoa mwanzoni kuhusu uuzaji wa tokeni. Sasa hebu fikiria kuiweka ili njia pekee ambayo mnunuzi anaweza kutuma shughuli za ununuzi ni ikiwa imewekwa mhuri wa baadhi ya metadata na maelezo ya utambulisho, yanayoweza kupatikana na muuzaji. Kwa hiyo muuzaji anapokwenda kwenye benki, wanaweza kufichua maelezo hayo kwa benki. ** Kumbuka kwamba jambo la msingi ni kufanya hivyo kwa njia inayolinda faragha, na isiyo wafanya watu kuwa walinzi wa data **. Kama tulivyoona na udukuzi wa Equifax mambo mengine kama hayo, uhifadhi wa taarifa zinazoweza kumtambulisha mtu binafsi ni tatizo kubwa!

Cardano - gundi.

Tunapotafuta majibu ya swali la uingiliano, tunagundua kriptographia kipya, wazo la metadata ya hiari, na vitu kama vifaa vya kuaminika. Hizi zinaweza kutoa njia salama za kuhifadhi vitambulisho, kutoa hakikisho kwamba data imeharibiwa baada ya muda fulani, na vitu kama kuweka tagi ya kijiografia. Ikiwa tutafanikiwa, Cardano itakuwa gundi ambayo inawezesha mtandao wa blockchains. Bitcoin inaweza baki kuwa Bitcoin, ethereum inaweza baki kuwa ethereum, na benki za jadi si lazima zibadilike sana. Cardano itatoa daraja hilo muhimu ambalo sio kati na sio tete. Badala yake, ni mtandao mkubwa uliogatuliwa, ambao unaanzisha enzi hii mpya ya uingiliano.

Get more articles like this in your inbox

tafadhali toa maoni

Or leave comment
Share

No comments yet…

avatar
You can use Markdown
close

Playlist

  • EP2: epoch_length

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 3 se. 24
    Darlington Kofa
  • EP1: 'd' parameter

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 4 se. 3
    Darlington Kofa
  • EP3: key_deposit

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 3 se. 48
    Darlington Kofa
  • EP4: epoch_no

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 2 se. 16
    Darlington Kofa
  • EP5: max_block_size

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 3 se. 14
    Darlington Kofa
  • EP6: pool_deposit

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 3 se. 19
    Darlington Kofa
  • EP7: max_tx_size

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 4 se. 59
    Darlington Kofa
0:00
/
~0:00