Tafakari ya mwaka wa 2021 na mwaka ujao: na Charles Hoskinson
Katika gumzo la YouTube la mkesha wa krismasi, Mwanzilishi wa Cardano Charles Hoskinson alitafakari juu ya mafanikio na changamoto za mwaka wa 2021, na akatazamia kitakachokuja katika mwaka wa 2022.
Cryptocurrency - mtazamo wa jumla wa mwaka wa 2021
2021 ulikuwa mwaka wa mafanikio kwa mfumo mzima wa ikolojia wa cryptocurrency. Bitcoin, ethereum, Cardano, na zingine zilionyesha ukuaji mkubwa. Cardano ilianza mwaka kwa dola 0.18, na kumaliza kwa takriban dola 1.36, baada ya kuchezea kwa dola 3 mapema mwezini Septemba. Ulimwengu wa NFTS ulichipuka: kila mtu sasa amesikia kuhusu aina hii mpya ya mali ya kidijitali, hata kama bado hatujui ni kwa nini tunaitaka! Nafasi ya DeFi kwa ujumla imeongezeka kutoka soko la bilioni 10, hadi soko la bilioni…