Je, Staking ni nini?

what-is-the-point-of-buying-ada-and-staking-in-cardano-hero-image
Lend us your voice!
Audio recordings make content accessible to more people
Record Article

Wanadamu wanamotishwa na kusukumwa na masilahi ya kibinafsi, ndiposa Cardano ikajengwa kutambua na kujipatanisha na ukweli huu. Mtandao wa Cardano hutuza washiriki na kugatuza madaraka. Hii inafanikishwa kupitia kazi ya sarafu yake ya dijitili, ADA, na mchakato unaoitwa 'staking'. Matokeo yake ni mfumo ambo uko imara na wenye usawa.

Mtandao
Mtandao wa Cardano ni hivyo tu: Mtandao wa nodi za kompyuta zilizounganishwa. Kila nodi hutunzwa na mwendeshaji wa Stake Pool. Wakati kuna shughuli kwenye mtandao wa Cardano, bila mpangilio 'pool' huchaguliwa kunyakua rundo la shughuli, rundo hili kisha huthibitishwa na kuwekwa kwenye bloki ambalo huhalalishwa na nakala yao ya hifadhidata ya blockchain ya ulimwengu. Ifuatayo, kila kompyuta nyingine kwenye mchakato wa mtandao huthibitisha na kupakua sasisho. Kushiriki majukumu huondoa hitaji la kuamini benki kuu au serikali. Kwa kuwa kila nodi ina nakala yake ya blockchain, haiwezekani kwa nodi moja kuongeza rekodi ambazo hazijakubalika na wote. Hakuna mtu anayeweza kudai pesa ambazo hana haki ya kupata; shughuli za ulaghai zinakataliwa na mtandao wote na kulazimisha pool lililochaguliwa kwa hiari kufuata sheria.

The Pools
Cardano hufikia usalama wa pamoja na uwajibikaji wa pamoja kwa kuhamasisha mtandao dhabiti wa washiriki. Kwa nini mwendeshaji wa pool kutaka kufanya kazi ya kudumisha pool kwenye mtandao? Kwa sababu kuna pesa ndani yake, bila shaka! kila siku tano, pool ambazo hufanyia blockchain kazi yake, hupokea kiasi fulani cha ADA kama tuzo.

Staking
Sio kila mtu ambaye anataka kushiriki katika mazingira ya Cardano anaweza kuendesha na kudumisha seva ya kompyuta. Hapa ndipo staking inakuja: unaweza kukabidhi ADA yako kwenye pool. Halafu, wakati pool hilo litalipwa, unalipwa pia, sawia na kiwango cha stake/hisa yako. Hii ni kama riba inayopatikana katika akaunti ya akiba ya benki. Wakati benki inashikilia pesa zako, wanaifanyia kazi kwa kukopesha wengine, na kukusanya riba. Kwa hivyo unapata sehemu kidogo ya mapato hayo kwa njia ya riba kwenye akiba yako. Kwa 'staking' unaruhusu uwekezaji wako ukufanyie kazi. Tofauti na benki za jadi, kila mtu anaamua sheria za mazingira, sio wachache. Kwa hivyo, mapato ni ya kutia moyo na ya haki zaidi kuliko yale utakayopata katika benki.

Wakati kiwango cha wastani cha riba kwenye akaunti ya akiba katika U.S. ni .04%, Cardano ambayo iko"staked" inapata 5.5% kila mwaka katika tuzo.

Ikiwa utawekeza katika Cardano na uchague kuto'stake', ni kama kuficha akiba yako chini ya godoro. Kwa kweli ni mbaya zaidi! 'exchange' ulipowekeza ADA ndio wana'stake' kwa niaba yako, na kuweka asimilia yote (100%) ya tuzo. Wala haupaswi ku'stake' kwenye 'exchange'. Katika visa hivi, 'exchange' bado ndiyo mshindi mkubwa. Wanadhibiti chaguo ya 'pool' inayopatikana, na ada wanayokusanya ni kubwa zaidi.

'Staking' haina hatari na ina malipo
Unaweza fanya biashara, au kutumia ADA yako wakati wowote unataka. Wakati ADA yako iko 'staked', unastahiki kupata tuzo. Pia, uwekezaji wako unawezesha usindikaji kwenye mtandao. Kupitia mpangilio huu wa kijanja, Cardano imeunda mfumo ambao unadumisha usalama na usawa wa hali ya juu, kwa kulinganisha maslahi ya kibinafsi na sheria za mtandao.

Previous in series

What is Cardano

Next in series

How to buy Ada

No comments yet…

avatar
You can use Markdown
close

Playlist

  • EP2: epoch_length

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 3 se. 24
    Darlington Kofa
  • EP1: 'd' parameter

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 4 se. 3
    Darlington Kofa
  • EP3: key_deposit

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 3 se. 48
    Darlington Kofa
  • EP4: epoch_no

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 2 se. 16
    Darlington Kofa
  • EP5: max_block_size

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 3 se. 14
    Darlington Kofa
  • EP6: pool_deposit

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 3 se. 19
    Darlington Kofa
  • EP7: max_tx_size

    Authored by: Darlington Kofa

    d. 4 se. 59
    Darlington Kofa
0:00
/
~0:00